VETA na Changamoto. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

VETA na Changamoto.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pascal Mayalla, Dec 14, 2009.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280

  Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi, VETA, imepewa changamoto ya kupanua wigo wa elimu kujitegemea, kwa kuongeza stadi za ujasiliamali, biashara na usimamizi wa fedha, huku ikipanua elimu ya ufundi stadi kufikia kiwango cha ngazi ya Diploma ya FTC na kuongeza idadi ya vyuo hivyo kufikia angalau kila wilaya iwe na chuo kimoja cha VETA.

  Changamoto hiyo, imetolewa leo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Standi linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Corridor Spring mjini Arusha.

  Prof. Maghembe amesema vyo hivyo vya kila wilaya, vitatumika kama chachu ya kuondoa umasikini, kwasababu elimu inayotolewa na VETA, huwapatia vijana stadi za maisha kuweza kujiajiri na kujitegemea.

  Prof. Maghembe amesisitiza VETA, isiishie kwenye utoaji wa elimu tuu na kuwapatia vitendea kazi, bali pia iwapatie jinsi ya kupata mitaji na namna bora ya kutafuta masoko ya bidhaa zao, hivyo mhitimu akimaliza VETA, anaanza kujitegemea moja kwa moja.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Veta, Prof. Idrissa Mshoro, amesema VETA, imeishaanza kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto zilizoko mbele yake, ikiwemo ya kuboresha mafunzo wanayoyatoa kwa kuanzia na kuwajengea uwezo walimu ili kupata walimu bora watakaotoa wahitimu bora.

  Prof. Mshoro amesema VETA imeshaanza mkakati wa kujisambaza kila wilaya, kwa kuanzia, imeshagharimia andiko na mchanganuo wa vyuo kila wilaya, na tayari imeishatenga Shilingi Bilioni Nne katika bajeti yake kujenga vyuo vipya viwili katika wilaya ya Makete na Ludewa na kuviboresha vyo vya Karangwe, Korogwe na Mwanga.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Veta, Eng. Zebadiah Moshi, amesema lengo la kongamano hilo la siku mbili ni kupokea taarifa za utekelezaji wa malengo waliojiwekea kwa mwaka huu toka kanda zote 9 za Veta na kujadili changamoto zinazoikabili Veta pamoja na ufumbuzi wake.

  Kongamano hilo, linahudhuriwa na wenyeviti na wajumbe toka kwenye kanda zote 9 za VETA,Wenyeviti wa Kamati za Kiufundi za Ushauri (TACs) na wadau mbalimbali muhimu wa VETA.
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hapa nadhani watakua wanaingilia IFM !
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,531
  Trophy Points: 280
  Wande, 'biashara na usimamizi wa fedha' hii ni kuhusu wahitimu wao, wanafundishwa kutengeneza bidhaa, hawana marketing skills matokeo yake biashara zinadoda, hawana financial management matokeo yake wakikopeshwa mtaji unazama na waliofanikiwa wakishika milioni, basi ndio 'mwajuma atanikoma' au 'leta kama tulivyo'

  hii ni tofauti na biashara za CBE, IFM etc, huu ni ujuzi wa biashara ndogo ndogo.
   
Loading...