Sasa baada ya lile picha, Eliza ulizungumza kwa furaha sana, nakumbuka ulikuwa ukitabasamu sana bila kuchelewa ulisema tuende Mwenge sehemu tulivu tupige stori mbili tatu, jamaa yangu na yule dada niliyekuwa nae walikuwa wameshaanza kuusoma mchezo sasa, bahati nzuri mchizi naye alikuwa mjanja sana hakubabaika kabisa, kila ulilomuuliza alisema yah yah na hakuweka neno la ziada as alikuwa hajui kabisa ajibu nini, tukiwa ndani ya gari jamaa alikuwa akinitumia text akinisihi sana nikwambie ukweli kwani nilimweka kwenye wakati mgumu sana, nilimwambia nitakuambia tukifika Mwenge.
Duh hali ilikuwa ngumu sana kwa jamaa yangu kwa sababu uliendelea kumpigisha stori azizozijua kabisa!!
Mbaya ni pale ulipompigia mdogo wako, ambaye niliwahi kuzungumza nae ukimsimulia jinsi ulivyoniona na jinsi nilivyo, maskini ulikuwa unaongea na mdogo wako juu ya mtu asiye sahihi na yule uliyezoea kuongea nae kila siku.
Bahati nzuri mimi na rafiki yangu ni warefu tuliendana ila kidogo tu.
Tulifika Mwenge ukatupeleka sehemu na ukasema tuseme chochote...
And that time nahisi ulikuwa umeshaanza kupata mashaka kwani kuna point ulimuuliza jamaa yangu akaikosea majibu kabisa,
Ulimlalamikia kidogo ukimuuliza umesahau haraka hivyo? Ulijitahidi sana kuelezea lakini mchizi ilibidi amute tu as alikuwa haelewi kabisa hiyo habari.
Ukimya ulitawala kidogo then ukatext ukasema ''Derick ur so handsome''...
Leo nimedhibitisha nilichokuwa nakiamini.
Roho na mwili wangu vimefurahi sana kukuona. Niliisoma kijanja wala siku ijibu.
Ulinitext tena ukiniambia ningekuambia mengi but not here coz of ur friends presence sitaweza, karibu sana nyumbani kwetu.
Hapa nilijibu tu thanks!
Tuliendelea na stori nyingi nyingi as ulikuwa main speaker ulituambia sana habari zako...
Hapo sisi wengine watatu tulikuwa wasikilizaji tu, jamaa yangu alinitumia ujumbe akaniambia nikusaidie kumwambia ukweli? Nilimzuia nikamwambia nitakuambia mwenyewe.
Yule dada mwingine alishauelewa mchezo tayari na aliniandikia pia akinisisitizia nikuambie ukweli ili mshikaji wangu awe huru.
Kuna muda ulipiga simu home kwenu kwa mdogo wako, na ukataka aongee na mimi, mshikaji alipata wakati mgumu na kiukweli sauti zetu hazikuwa zinaendana.
Nilijipanga kukuambia ukweli ila nilikosa kabisa gia yakuanzia. Eliza ulikuwa mwongeaji sana, ulitusifia sana ila ndiyo hivyo nilikudanganya, wakati wakuondoka ulifika na kwa mara nyingine ulimkumbatia tena jamaa yangu kwanza then ukatuhagi na sisi at last ulihag the right person.. wewe ukaelekea Boko sisi tulielekea Mlimani ( udsm) jamaa yangu alikuwa anasoma pale.
Nakumbuka dakika kumi na tano hazikuisha uliniandikia meseji ndefu kama waraka, ukielezea tu jinsi ulivyoniona na ulivyofurahi niliwaonyesha marafiki zangu ule ujumbe, kiukweli walinilaumu sana.
Niliujibu ujumbe wako kwa kifupi tu.
Uliandika tena ukiniuliza nimekuonaje then mbona hukuwa na raha most of the time?
Nilijibu nikijaribu kukusifia na mimi ili zile sifa ulizonipa ziendane kidogo...
Tuliendelea na mawasiliano na uliniomba sana nifike kwenu kabla sijarudi Dodoma...