Ventilation on MCC move is primed on wrong assumptions

Aisee kumbe tuna watu wenye akili sana nchi hii ila hatuwatumii vizuri, angalia mzee alivyochambua na kujenga hoja kwa watu wenye uelewa mzuri watachukua ushauri huu
 
Tutakukumbuka Kikwete daima.
granted. lakini huyo Kikwete wenu alitengeneza mazingira ya kuonekana tunafanikiwa kiuchumi kwa kuvuta hii mikwanja ya (aka kuhongwa na) wazungu. which was never going to be sustainable.

ona sasa amemwangushia mwenziye jumba bovu. hata kuhusu Zanzibar yeye ndiye aliye-engineer ule u-Jecha.
Kikwete simply didn't care one iota about this country.....it was all about him and the crowd around him. basi.
 
Kikwete tutakukumbuka daima.
Yaani daktari aliyeshindwa kumpima mgonjwa na kujua ugonjwa aendelee kukumbukwa na kuheshimiwa dhidi ya daktari aliyethubutu kumpima mgonjwa, kupata majibu, kumweleza ukweli na kumpangia dozi ya kumponya!
Tukumbuke kifungu cha 'Zanzibar ni nchi' kiliingizwa wakati wa utawala wa nani.
 
Kama huna maoni ya msingi YEHODAYA ni bora tu ukacheze pool labda utakuwa mshindi lakini kwenye hoja hii unajivua nguo tu na kutuonyesha nguo ya ndani iliyo chafu na yenye matobo
 
Kikwete tutakukumbuka daima.

Kikwete si ndio chanzo cha yote haya.
Huu sasa ndio unafiki.
JK akiwa rais na mwenyekiti wa CCM jecha ndio alifuta uchaguzi,Huyu mwingine kaingia kakuta tatizo lipo.

Acha unafiki.
 
Ila inamuruhusu amri jeshi mkuu kupeleka majeshi yake kusimamia uchaguzi wa Zanzibar
 
Hakika kama JPM angekuwa , Rungu la kuamua hatma za zbar aneungana na Dr Shein mwanzoni kabisa na kumtangaza Maalim awe Rais yaishe! Prof JK ndio amecheza game hii chafu kwa kuogopa historia ; JPM bado ana nafasi ya kuongea na Shein na kumaliza huu mgogoro! Achana na historia wala siasa! Acha ukweli uwe ukweli! Turudi pale pale.......na kusema ukweli tupate kusonga mbele
 
unapotengeneza mabilionea wengi hiyo ndo maendeleo,hao mabilionea watainvest katika viwanda,kilimo etc na wataajiri malaki kama si mamilion.
Nchi kama marekani ,china etc zinajisifia kuzalisha mabilionea wengi,
mambo ya ukominist yalishapita
 

Ni kweli mkuu wewe una akili sana hata Jecha alipofuta uchaguzi alitumia sheria kuufuta yeye kama yeye si tume akili za kuambiwa changanya na zako.Yale magari ya deraya TPDF yalikuwa pale kwa niaba ya muungano ikiwa uchaguzi ni batili kwanini tulishiriki katika ubatili ?.
 
Mufuruki anaongea kama kibaraka wa MCC.

CUF walishiriki uchaguzi wa marudio na wakapata kura chache.CCM ikashinda.Utaongeaje na mtu aliyeshindwa sanduku la kura?

CUF walishindwa kwenye uchaguzi wa matokeo yaliyotangazwa na tume YA UCHAGUZI.
Duh! umeandika kwa uelewa wako au kwa shinikizo? aisee, tunasafari ndefu!
 
Mkuu umenena vyema kabisa,wengi watakaomponda Mafuruki ni wale ambao ni wafata mkumbo.Tukae tutafakari kwa kina suala hili.Isije ikatukuta kama yaliyotukuta wakati ule wakina Margareth Thatcher na beberu mwenzie Ronald Reagan walivyotufanyia kipindi kile cha vita baridi.
 

There is a reason why they say 'sometimes you gotta throw the rule book to do the right thing'. Emotions won't do you any good on this one. Just protect the best interests
 
unapotengeneza mabilionea wengi hiyo ndo maendeleo,hao mabilionea watainvest katika viwanda,kilimo etc na wataajiri malaki kama si mamilion.
Nchi kama marekani ,china etc zinajisifia kuzalisha mabilionea wengi,
mambo ya ukominist yalishapita


Nakubaliana na wewe ila sasa tengeneza Mabilionaire ambao wataleta faida katika nchi sio unatengeneza mabiliionaire hela zao wanaziweka benki za nje...

hawaweki fedha kwenye mabenki ya nyumbani kinachosababisha mabenki kukosa mitaji


hivyo basi watu wakienda kukopa kwa ajili ya kuanzisha biashara zao wanazungushwa saana huku na kule
 
Ila inamuruhusu amri jeshi mkuu kupeleka majeshi yake kusimamia uchaguzi wa Zanzibar

Majeshi unayoyaona zanzibar hayajawahi hata siku moja kupelekwa na amiri jeshi mkuu.Yamepelekwa kule na katiba ya jamhuri ya muungano wa TAnzania acha kupotosha.
Katika mambo ya muungano tuliyokubaliana ni maswala ya ulinzi na usalama.Na wanapotekeleza majukumu yao hayo majeshi hayahitaji kibali toka kwa amiri jeshi mkuu kupiga risasi,nondo au mabomu ya machozi kibaka yeyote awe wa CCM AU CUF aliyeko Tanzania bara au Zanzibar.

Katika utendaji wake yaweza toka kwa wingi kutoka zanzibar kwenda bara au yakatoka kwa wingi kutoka ZANZIBAR kwenda BARA kwa ajili ya mazoezi au kazi zao bila kibali cha raisi wa muungano kwani hizo ni kazi zao za kila siku za kawaida.

Wako miaka yote Tanzania bara na Zanzibar
 
Magufuli ana kazi na uozo wa mtangulizi wake!
uozo upi?
After magufuli alitakiwa aanze na kushukughulika na awamu yake,sio kufuatilia mambo yaliyotokea awamu iliyopita wakati nchi ikiwa chini ya mtu mwingine,
haya ya kukamata watu walikula rushwa miaka mitano kabla hajawa rais yanapaswa kuwa nyongeza tu,
katika awamu yake anatakiwa sasa asile rushwa hata mtu mmoja ,ili baada hata ya miaka miwili bila hata mtu mmoja kula rushwa ndo tutajua kumbe kweli KAZI IPO HUKU
 
Ali Mufuruki hapa anaonyesha woga tu kwa wazungu, kwa kifupi ni hila tu wanaleta baada ya JPM kupitisha fagio la chuma CUF wamesusa kwa hiyari yao na misaada bado imeshindwa kuleta maendeleo yaliotarajiwa. Ali asiogope sana manake miaka 50 ya misaada bado hali zetu ni tia maji tia maji, yeye na wenzake wenye biashara ndio wataumia Zaidi lakini wagonga nyundo walio wengi bado wanaona nyota tu. Yeye maoni yake sawa ila akubali na watu wengine wafikiri tofauti na yeye na wachukue hatua hata kama watakosea hawawezi kukosea Zaidi ya G. Bush aliyeua maelfu ya watu kusaka silaha za maangamizi na bado hajazipata.
 
Blah blah tu....yaani tusiamue mpaka tuwashirikishe mabwana wakubwa?
 
Toka MCC wamejitoa kila kiongozi yuko bize kulaani na kutuaminisha kua misaada ya MCC haikua lolote.Ni wapuuzi wachache ndio wanaweza kuamini kua kuanzia sasa tunaweza kwenda bila support ya donors.Sikatai TZ inaweza kujitegemea but sio kirahisi na gafla kama watawala wanavyotaka kutuaminisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…