Vazi la taifa la Tanzania ni lipi?

Vituka

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
2,257
1,247
Habari ndugu zangu,

Kuna kipindi kulikuwa na mchakato wa kutafuta vazi la taifa, je ulifikia wapi? Tafadhali tujuzane kwa mwenye kufahamu hili.

Nadhani ni wakati muafaka tuwe na vazi la taifa ili itusaidie wananchi hasa tunapoenda kwenye ofisi za umma kupata huduma kwa kuwa kumekuwa na kero nyingi za kukataliwa kupata huduma wananchi kwa sababu ya mavazi yao.

Ni heri tuwe na vazi linalojulikana na kila mwananchi ili itusaidie kutuepusha na dhambi tunazozipata kutokana na kadhia hii.

Kwa anayejua vazi la Tanzania atujuze.

Ahsanteni.
 
Kuna mkubwa mmoja alianzisha mchakato wa vazi la taifa, mwingine alianzisha muziki wa taifa, sijui waliishia wapi.
 
kama bado hatujapata vazi la taifa tutembee uchi ili kuharakisha mchakato
pamoja na kuonesha uhitaji wa hili vazi
 
Ule mchakato wa vazi la taifa haukufikia mwisho na vazi lenyewe halikupatikana
 
Kuna mkubwa mmoja alianzisha mchakato wa vazi la taifa, mwingine alianzisha muziki wa taifa, sijui waliishia wapi.
Hee kumbe hadi muziki wa taifa ulitafutwaga? Nadhani ni vizuri nao upatikane ili hata wasanii wajue nyimbo gani zinatakiwa sio kujiimbia imbia tu kama wehu hahahaha
 
Ule mchakato wa vazi la taifa haukufikia mwisho na vazi lenyewe halikupatikana
Sasa tunafanyaje jamani?? Tunapata shida tukienda kuata huduma huko maofisiniiii!! Unawakuta watu wametunisha misuli getini wanazuia watu wasiingie kupata huduma kwa sababu ya mavazi yao. Tunakoma mbona??
 
Nchi hii inamambo ya ovyo sana heti vazi la Taifa kwa hiyo matatizo waliyonayo wananchi wakaona vazi la Taifa ndo Tatizo kubwa
 
Kwani vazi la taifa kwa akina mama si KANIKI tu inatosha

Kwa wale wa pwani nafikiri mtakuwa mmeelewa
 
Sasa tunafanyaje jamani?? Tunapata shida tukienda kuata huduma huko maofisiniiii!! Unawakuta watu wametunisha misuli getini wanazuia watu wasiingie kupata huduma kwa sababu ya mavazi yao. Tunakoma mbona??
Mwenyewe juzi nimepata hii kadhia ya kutimuliwa Ofisi ya manispaa pale kisa mavazi yani imekua kero
 
Mwenyewe juzi nimepata hii kadhia ya kutimuliwa Ofisi ya manispaa pale kisa mavazi yani imekua kero
Pole ndugu mwenyewe limenikuta leo Wizara fulani looh!! Yaani ni shida sijui tuvae nini
 
Back
Top Bottom