Vatican: Papa Francis aondoa 'usiri' katika uchunguzi wa unyanyasaji wa kingono unaofanywa na makasisi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Papa.jpeg

Papa Francis ametangaza mabadiliko makubwa kwa jinsi Kanisa Katoliki linavyoshughulikia kesi za unyanyasaji wa kingono kwa watoto na kukomesha kanuni ya "usiri" ambayo iliwaficha makasisi waliokuwa wakitenda vitendo hivyo hapo awali.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani ameondoa 'usiri wa Kipapa' katika kesi za manyanyaso ya kingono dhidi ya watoto wadogo zilizotendwa na makasisi. Pia, amefanya uhalifu wa umiliki na usambazaji wa picha chafu zinazohusisha watoto chini ya umri wa miaka 18 kuwekwa katika kundi la delicta graviora, yaani makosa mabaya zaidi.

Kwa maana hii, amefanya kuwa na uwezekano wa upatikanaji wa ushuhuda wa kesi kwa wachunguzi wa kiserikali.

Pia ameondoa siri zinazohusiana na utoaji taarifa, mashitaka na michakato ya maamuzi kuhusu kesi za dhuluma na vitendo vya kingono vilivyofanywa chini ya vitisho au matumizi mabaya ya mamlaka; kesi za unyanyasaji wa kingono wa watoto au watu walio katika mazingira magumu; kesi za ponografia ya watoto; kesi kuhusu kukosekana kwa kuripoti na kuficha wanyanyasaji kwa upande wa maaskofu na wakurugenzi wakuu wa taasisi za kidini.

=======================

Pope Francis is now making testimony collected in canonical processes available to legal authorities.

Two documents are destined to make a lasting mark: Pope Francis has abolished the pontifical secret in the case of sexual violence and the abuse of minors committed by members of the clergy. He has also decided to change the norm regarding the crime of child pornography by making the possession and dissemination of pornographic images of children under the age of 18 which fall under the category of delicta graviora – the most grave delicts.

The first and most important document is a Rescript signed by the Cardinal Secretary of State, Pietro Parolin. This Rescript communicates that, last 4 December, the Pope decided to abolish the pontifical secret connected with reporting, trials and decisions regarding the crimes listed in the first article of the recent Motu Proprio Vos estis lux mundi, that is: cases of violence and sexual acts committed under threat or abuse of authority; cases of the sexual abuse of minors or vulnerable persons; cases of child pornography; cases regarding the lack of reporting and the cover-up of the abusers on the part of bishops and superiors general of religious institutes.

The new instruction specifies that such information be “treated in such a way as to ensure its security, integrity and confidentiality” established by the Code of Canon Law to protect the “good name, image and privacy ” of those involved. But this “confidentiality”, the instruction also states, does “not prevent the fulfilment of the obligations laid down in all places by civil laws” including the possible obligation to report, and “the execution of enforceable requests of civil judicial authorities”. In addition, those reporting the crime, the victims and witnesses “shall not be bound by any obligation of silence” regarding the facts.

With the second Rescript, also signed by Cardinal Parolin as well as by the Prefect for the Congregation for the Doctrine of the Faith, Cardinal Luis Ladaria Ferrer, the modification of three articles of the Motu Proprio Sacramentorum sanctitatis tutela (published in 2001 and modified in 2010) were made known. It establishes that falling under the most grave delicts reserved for judgment by the Congregation for the Doctrine of the Faith are “the acquisition, possession or distribution by a cleric of pornographic images of minors under the age of eighteen, for purposes of sexual gratification, by whatever means or using whatever technology”. Up until now, the age limit had been established at 14 years.

Finally, in another article of the same Rescript, it is now permitted that, in cases regarding these more grave delicts, any member of the lay faithful holding a doctorate in canon law can perform the role of “Advocate or Procurator”, and no longer only priests.


Chanzo: Vatican News
 
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameuondoa mfuniko uliokuwa unafunika siri juu ya kashfa za udhalilishaii wa kingono kwa kufuta kanuni inayozuia kufichuliwa na kuchunguzwa kwa uhalifu huo.
1576730282001.png


Papa Francis amechukua hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kwamba kanuni hiyo ilikuwa inatumika kwa ajili ya kuwalinda wahalifu na kuwanyamazisha waliofanyiwa uhalifu wa kingono na pia ilitumika kuwazuia polisi kuchunguza uhalifu.

Watu waliotendewa uhalifu pamoja na mawakili wao wameushangilia uamuzi wa Papa Francis na kwa mtazamo wao, hatua hiyo ilipaswa kuchukuliwa mapema zaidi. Hata hivyo wametahadharisha kwa kusema kwamba ufanisi wa hatua hiyo utathibitishwa pale ambapo kanisa litakapolazimishwa kukubali uchunguzi ufanyike katika nchi husika na nyaraka zote juu ya wahalifu zitolewe hadharani. Juan Carlos Cruz aliyekuwa mhanga wa udhalilishaji wa kiongono kutoka Chile, ambaye sasa ni wakili amesema tamasha la siri sasa limezimwa.

Kwa mujibu wa sheria mpya Papa Francis ameeleza kuwa habari zinazohusu uhalifu wa kingono zitalindwa na viongozi wa kanisa lakini ameeleza wazi kwamba kanuni ya kanisa kuficha siri haitatumika tena.

Mchunguzi maarufu wa uhalifu wa kingono Askofu Mkuu Charles Scicluna amesema sheria hiyo mpya ni hatua muhimu ya kihistoria itakayorahisisha uratibishaji wa sheria na kufungua njia za mawasiliano na watu waliofanyiwa uhalifu wa kingono.

Mageuzi hayo mapya yalizinduliwa jana Jumanne ambapo Baba Mtakatifu alitimiza umri wa miaka 83. Kiongozi huyo wa kanisa katoliki amekuwa anasongwa na malalamiko kutoka duniani kote na kutakiwa kuyashughulikia huku mkazo ukiwa katika kuweka mambo bayana.

Asasi ya kutetea haki za wahanga, SNAP, imesema mageuzi hayo yanaashiria hatua muhimu inayoelekea upande sahihi. Hata hivyo asasi hiyo imesema mageuzi hayo bado hayajaanza kutekelezwa kwani bado ni maandishi tu, kinachotakiwa sasa ni hatua thabiti. Mnamo mwezi May kanisa katoliki lilitoa sheria nyingine kueleza wazi kwamba waliotendewa uhalifu wa kingono hawawezi kunyamazishwa na kwamba wanayo haki ya kujua matokeo ya kesi zao.

DW
 
Back
Top Bottom