tanganyika yetu
Member
- Nov 23, 2011
- 45
- 17
Kwanza napenda ijulikane kabla serikali haijaingiza vat kwenye utalii tayari mgeni/mtalii analipa vat kwa kuzunguka (indirect); kila mtalii anayekuja Tanzania analipa vat, analipaje? akilala kwenye hoteli zetu anakuwa ameshalipa vat, akipanda ndege ameshalipa vat, akipanda boat ya azam ameshalipa, akipanda Dar express ameshalipa nk. sasa hii vat ingine iliyoingizwa kwenye utalii maana yake nikwamba mtalii alipe vat double (direct na indirect) kwenye hoteli ndege, boat, bus nk. hii si sahihi kwani tunawahitaji sana watalii kuliko wanavyohitaji kuja nchini kwetu. Kwa kweli ni vizuri kushirikisha wadau kabla ya kupanga na kuamua jambo lolote ambalo linaloweza kuleta madhara kwa Taifa na watu wake. Japokuwa kuweka vat si tatizo sana, tatizo ni kwamba bidhaa yako ni bei gani kabla hujaiongeza kodi ingine, kama bei iko chini na ukaiongezea vat bado ikawa sawa au chini ya washindani wako basi hilo ni sahihi Lakini kama iko juu na bado unaongeza kodi hilo ni tatizo na hatari la kupoteza wateja. Mtalii hangalii kama kuna vat au hakuna; anachoangalia ni bei (safari cost) akiona bei iko juu anatafuta mbadala anaenda mahali (nchi) pengine. Na ni vizuri kuangalia na kutambua bidhaa ina ubora gani au uzuri gani ukilinganisha na mwenzeko au jirani yako mwenye bidhaa kama hiyo hiyo na anaitoa kwa bei nafuu! Tusifike mahali tukajisahau na kujivuna sana kuwa tuna bidhaa bora na tofauti kuliko washindani zetu. Tunaomba serikali iwe makini kwani utalii unagusa na kusaidia kila mtu; awe mdogo, wa kati, wa juu na Taifa kwa ujumla. Mungu ibariki Tanzania.