Hizi ndio kampuni zetu za kibongo kwa sasa,wenzao wakenya wanajipanga vizuri sana,wakati hapa kwetu kila kampuni ni kuzururisha watu mitaani.
Na ndio maana jamaa kasisitiza wanawake,maana anajua wanaume issue hizo watazinguana kwa mshahara hewa.
Inamaana usipouza imekula kwako,na ndio maana hakuna mshahara kamili.
Huku Zanzibar waliletwa kibao kutoa Dar,walikuwa wanatembea mpaka unawaonea huruma na wanunuaji hakuna,hatimae 75% wote wamerudi na waliobaki wengine wamepata wanaume hukuhuku kwa maisha yalivyokuwa magum,we unatembea bila kula mpaka usiku.kwenye kuajiri uongo mwingiiiiiiiii.
Acheni Biashara za kuwazururisha watu hembu badilikeni,pelekeni pale kwenye Demand tu.
Mmekuwa kama wafugaji wakitanzania,mtu anahama na mifugo hajui wapi itakuwa hatma yake,wakati wenzao wanazalisha chakula kwa mifugo yao kwa tija na bila kuhama