V6 Versus I4 cylinder engine. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

V6 Versus I4 cylinder engine.

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Jaluo_Nyeupe, Apr 17, 2012.

 1. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wakuu,
  Naomba kujuzwa na wataalam wa magari kati ya gari zenye injini ya I4 cylinder na V6 cylinder. Je ni kweli gari zenye injini ya v6 zinatumia mafuta mengi kuliko I4? Mfano nina gari lenye injini ya ukubwa wa 2.0L moja ni V6 na lingine I4, je zinaweza kuwa na tofauti gani ya kilometa kwa lita moja?
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Gari ya 4c kama RV4, Suzuki Vitara n.k ni tofauti ulaji na 6c kwa sababu moja kuu.

  Ile cylinder ina diamater zake kama 10cm kwa kila moja, zikiwa sita ina maana utakuwa na cylinder sita zenye diameter inayofanana na kila ukiwasha gari zote zinapelekewa mafuta.

  Ulaji wa gari hii ni lazima uwe tofauti kidogo na gari yenye 4c kwa diatemer inayofana kwa sababu ukiwasha engine ni 4c zinapelekewa mafuta japokuwa siku hizi kuna kitu kina kitu kinaitwa VVTi.

  Halafu ukubwa wa CC unaendana na body weight hivyo gari nyingi zimewekewa CC kubwa ili kuaccomodate weight inapokuwa inakimbia.
   
 3. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Naomba ufafanuzi kuhusu VVTi....na mie nijue...nimeanza kusikia kitu hii.
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sina maelezo ya kitaalamu sana ila wanasema ni teknolojia mpya inafanya gari kutokula mafuta mengi sana kwa kuongeza asilimia kubwa ya hewa inayopelekwa katika injini na kidogo ya mafuta.
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,264
  Trophy Points: 280
  V6 na 4cyilinder kunatofauti 6 cyilinder yake diagram yake nindogo na ulaji ni mdogo!4cylinder diagram ya nikubwa na ulajiwake ni mkubwa,speed ya 6 niharaka sana na ikivuka 110kph inavungu vulve za ziada inaanza kula wese ili ilikumantaine speed!
   
 6. N

  Namtih58 JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 236
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kujibu swali, ni kwamba bila kuzingatia mengine, ni kweli gari la V6 lina ulaji wa mafuta zaidi ya I4.

  Ijapokuwa engine zote ni 2.0L, moja ina cylinder 6 na ingine ina 4, kwa hivyo yenye 6 inachoma zaidi kwa cylinder 2.

  Ukiangalia, tuseme I6 na V6 kwa sababu siku hizi ni vigumeu kupata V4, utaona tofauti ya engine hizi. I6 chamber zake zimepanga foleni moja nyuma ya mwenzake, kwa hiyo huwa ndefu na konda.

  Kwenye V6, chamber zake ni kama vile ukiangalia foleni mbili za chupa za soda kwenye kreti, kwa hiyo haziwi na urefu wa I6 lakini ni pana kidogo.

  V huwa na advantage ya kuwa na nguvu kuanzia rev za chini, hii ni kwa sababu piston zake zina sukuma kutoka pande mbili tofauti, wakati I inasukuma kutoka juu pekee.

  Zaidi ya hapo inakubidi, uangalie specs za gari, kwani vitu kama turbo charger vinaongeza ulaji wa mafuta, VVTI amabyo ni teknolojia inayo wezesha engine kuchelewesha ama kufungua valve mapema, kulingana na mahitaji, yaani kama unavyo endesha gari inahitaji nguvu zaidi au ulaji nafuu wa mafuta. VVTI/VTEC ina weza kupunguza au kuongeza ulaji kulinga na unavyoendesha gari.

  Lingine ni kama gari ina injectors ama ni ya kabiurata. Ya kabiurata ukilinganisha na ya injekta ina ulaji mkubwa. Na pia uzito wa gari, sababu ukiangalia gari mbili zenye engine aina moja, ikiwa moja ni nzito kuliko ingine, basi ulaji wake unkuwa wa juu kuliko hiyo nyingine.

  La mwisho ambalo huwa naona watu hawazingatii. Watu wengi huleta magari kutoka ngambo, kisha sababu ya mabarabara yetu mekanik anawashauri wabadilishe tires kuweka kubwa, hapo unapobadilisha tu basi ujue lazima engine ita fanya kazi zaidi ya hapo awali kuyazungusha, matokeo yake ni ulaji zadi wa mafuta.
   
Loading...