Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi?

Uzuri wa mwanamke upo wapi? Ni upi?

View attachment 144639Ndugu zangu, wapenzi
Leo naleta hoja nzito kidogo. Najua baadhi ya akina dada watakwazika. Kwa hiyo, naomba mnisamehe.

Siku hizi limezuka wimbi la akina dada na hata akina mama kujilemba kwa namna mbalimbali kuanzia rangi ya mwili, nywele, kucha, midomo na wengine wamefikia hatua ya kunywa au kupaka dawa za kichina za kuongeza makalio na maziwa. Wengine wanasuka nywele ndefu na wanaongea kwa mbwembwe huku wanatikisa vichwa vyao na kushikashika nywele kama wafanyavyo wanawake wa kizungu. Wengine wamefikia hatua ya kubadili hata sauti na namna ya kuongea!!

Najua dada zetu wanafanya hivyo kwa lengo la kupendeza na wengine lengo lao ni kuwavutia wanaume. Lakini mimi binafsi sijui ni nini kimenitokea! Inawezekana ndiyo abnomality hiyo. Kadri mwanamke anavyojilemba zaidi ndivyo hamu ya kuendelea nae kimahusiano inapungua.

Ukweli ni kwamba nikiwa mausiano na mwanamke ambaye ni natural yaani mwenye nywele za kawaida anayesuka mtindo wa 'twende kilioni' au amezibana tu, wowowo, chuchu na sauti natural huwa napata fraha ikilinganishwa na mwanamke mwenye kucha za bandia, nywele za bandia, na midomo iliyopakwa rangi nyingi.

Sijui ni ugonjwa au ni jambo ambalo hata wanaume wenzangu huwa linawakumba?

Tafadhali karibuni kwa mawazo

ni hali tu ya kawaida mkaka...kila mtu ana interests zake...huwezi kuwa kama yule......endeleza msimamo wako huo huo....
 
mwanamke kujiremba ... natural tuachie misitu babueeeee... tunapendwa bado na bandia zetu
 
Uzuri wa m/Mke ni mwenye maadili na mwenye kumuogopa Mungu(Dini) asiwe Pepsi Fanta au full artificial
 
wanawake wengi wanaofanya artificialities kwenye miili yao, hata uzuri wanaoupata ni wa muda tu, hata wanapopendwa, hupendwa kwa muda tu, hata wanaume huwatumia wanawake hawa kwa muda na kuachana nao. Wale ambao hawataki makuu kwenye miili yao ndio hudumu kwa kila kitu; maumbo yao hudumu, sura zao nzuri hudumu, tabia zao nzuri hudumu hivyo mara nyingi hudumu kwenye penzi, ndoa na kadhalika. Mimi naamini kila mtu aliumbwa kwa dhumuni maalumu, hivyo unapojaribu kujibadilisha unaharibu hilo kusudi la kuumbwa kwako. Turidhike na namna Mungu alivyotuumba!
 
Back
Top Bottom