Uzuri wa magari ya automatic na manual...!!

Binafsi nilikuwa napendelea sana kutumia automatic nilipokuwa Ughaibuni kwa sababu nilikuwa kila siku natembea km 160 hadi 200 yaani nakaa mji mwingine nafanya kazi mji mwingine, nilipokuja kununua Subaru impreza wrx ndio nikaanza kuzipenda gari za manual, kwani injini yake ilikuwa ina turbo na ilikuwa very powerful na ilikuwa ina gia sita sasa kwenye highway za wenzetu unaweza ukakimbia hadi speed 200, yaani safari zangu za kila siku niliona kama zimepungua umbali vile maana ukianza kutupia namba mbili itataka ya tatu na jinsi injini inavyolalamika ndio mzuka unavyopanda kutupia nyingine na nyingine na hapo turbo ndio ishafunguka unasikilizia mruzi wake yaani ni raha iliyoje, lakini nilivyorejea hapa Bongo niliona hali ni tofauti kidogo kutokana na foleni zetu ni mateso ukiendesha manual


Sent from my iPhone 4S using JamiiForums app
 
Kama unaishi Dar ni bora auto, nadhani mnaelewa sababu ni nini.
 
Manual ni nzuri zaidi ya automatic. Unakuwa na full control ya gari. Unabadilisha gear pale unapoamua sio kusubiri revolution. Battery ikiwa low ni rahisi kusukumwa na kuwasha wakati huwezi kufanya hivyo kwa manual. Hata ukiangalia bei za manunuzi utaona kuwa gari za aina moja say RAV4 zinazolingana sana ila zikatofautiana transmission utaona kuwa manual in bei kubwa zaidi.

My take: Go for manual transmission
 

2po pamoja
 

Saaaafi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…