Uzungu kwenye mawazo ya Marais wa Afrika

Machepele

Senior Member
Jun 28, 2019
183
250
Nianzie mbali kidogo ili hoja yangu ieleweke.

Historia ya mtu mweusi kutamani kuukwaa urais wa Marekani haijaanza na Obama. Mnamo 1848, Frederick Douglass alikua mgombea wa kwanza wa urais wa mwenye asili ya kiafrika (African- American) huko marekani, hakufua dafu system ikamtema.

Mnamo 2009, Barack Obama alikuwa mgombea wa kwanza wa urais aliyeteuliwa na chama kikuu, ambacho ni Democratic. Alikuwa Mmarekani-mweusi wa kwanza kuchaguliwa (na kuchaguliwa tena kwa awamu mbili) kuwa rais wa Marekani mwenye asili ya kiafrika tena si tu kiafrika bali kiafrika mashariki, si ni hapo tu Kenya bhana kwa Mzee Kenyatta, kwa Kinauhuru.

Lakini hivi karibuni(2021) tumeshuhudia tena katika historia ya marekani ikipata makamu wa kwanza wa rais mwenye asili ya kusini-Mashariki mwa Marekani (India), hapa ninamzungumzia Kamala Harris.

Obama bila shaka aliiongoza Amerika siyo kwa bahati mbaya. Maana ninachokijua wamarekani hususa ni zile taasisi zinazo husika kufanya vetting ya viongozi wa ngazi za juu kama Rais wapo makini sana. Haikuwa bahati mbaya hata kidogo kumchangua Obama kuanzia kwenye chama(Democratic) hadi kwenye kura(Ballot Paper).

Kufupisha story
KILICHOMFANYA OBAMA kuchukua urais wa marekani ukiachilia mbali vigezo vya kielimu, kukubalika chamini nk.. Lakini yalikuwa ni mawazo ya kimarekani. NIKAZIE HAPA (yaani Obama ni Mwafrika mwenye mawazo ya kimarekani)ndiyo maana hata zile mission kubwa kubwa za kijeshi zilizo leta matokeo chanya kwa marekani zilifanikiwa chini ya Obama alipata support kutoka kwenye system za kijeshi nchini marekani.

TURUDI AFRIKA
Kuna marais wa Afrika(Ni waafrika, kimwonekano, rangi ya ngozi na nywele na kwa sura Lakini kiuhalisia siyo waafrika) ndiyo maana wameweka bond uhai wa kiuchumi, kimaendeleo na kielimu katika mikono ya wazungu.

Ninachoweza kusema ni kwamba Afrika tunaweza tusiwe na rais mwenye asili ya kizungu, (kama wapo mtanisaidia kuwataja), kama ilivyo kwa marekani kuwa na rais mwenye asili ya kiafrika (kama ilivyokuwa Obama).

Let say leo, Tanzania ipate rais mwenye asili ya Kimarekani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom