che wa Tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2011
- 277
- 71
Wadau nina wazo la kuanzisha biashara ya kuuza juice ya miwa....naomba kujuzwa juu ya gharama za mashine hiyo. Ile ya kuzungusha kwa mkono na ile ya kutumia mota. Nawakilisha wadau
MASWALI ZAIDI KUTOKA KWA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
==============================================
bbwaoy ameuliza
Niliwahi kuishi Tanga kipindi flani hapo nyuma, nilikua kikazi huko takribani miezi kama mi 5 hivi.
Kuna sehemu 1 jamaa amefungua kijisehemu chake ana saga juice ya mua, jinsi alivyo kua ana pokea hizo 1000 moja na 500 tano.
Kwa siku yule jamaa na uhakika halali nje ya elfu 30. Kwa week laki 2 hamkosi . Any way point yangu hii hapa.
Nahisi nahitahi kufungua hichi kiji biashara hapa Mwanza. Walau nipate kipato nje ya mshahara.
Kuna challenges gani kwenye hii biashara? Faida zake je? DOES IT PAY HII BIASHARA?
Hasa challenges ndio mimi nataka ili nipambane nazo sasa kisawasawa.
Asante!
=====================
MAJIBU KUHUSU BIASHARA HII
===========================================
=============================================
Juisi ya Miwa: Biashara yenye faida maradufu
Biashara ya kutengeneza juisi ya miwa imekuwa maarufu sana katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania. Hii inatokana na kinywaji hicho kuwa na manufaa mengi katika mwili wa binadamu. Moja kati ya kazi kubwa za juisi ya muwa ni kusafisha mkojo, figo na kutibu homa ya manjano.
Vile vile, juisi ya miwa ni kiburudisho ambacho hukata kiu hasa wakati wa joto. Pia miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa. Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo. Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Biashara ya juisi ya miwa ni moja kati ya biashara ndogo inayoweza kuanza na mtaji mdogo lakini ikakuletea faida kubwa kama mjasiriamali kulingana na uhitaji wake. Ili kuanza biashara hii mambo yafuatayo ni ya msingi kuzingatia:
1) Mashine ya kukamua miwa – Tsh 300,000-400,000
2) Glasi nzuri za ujazo tofauti – Tsh 20,000
3) Chujio – Tsh 5,000
4) Beseni – Tsh 8,000
6) Ndoo 2 – Tsh 5,000
7) Jaba kubwa la uchafu – Tsh 12,000
8) Mtaji wa kununua miwa –Tsh 50,000
9) Tolori la kusafirisha – Tsh 60,000
10) Vifaa vingine – Tsh 40,000
Jumla ya mtaji wa kuanzia Tsh 640,000/=
Muwa mmoja unaweza ukatengeneza lita 4 za juisi na muwa mmoja unaweza ukaununua kwa Tsh.300/= kwa bei ya jumla. Lita moja ya juisi utauza 1,000/= hivyo kwa muwa mmoja unatengeneza Ths 4,000/=.
Mjasiriamali anaweza akaongeza ubunifu kwa kuongeza tangawizi au limao katika juisi yake ya miwa ili kuongeza ladha. Biashara hii ni nzuri hasa inapofanyika sehemu yenye mzunguko wa watu wengi kama stendi ya mabasi, masoko, n.k
CHANGAMOTO
Faida za juice ya miwa kwa binadamu:
1. Uwezo wa kuipa miili nguvu kwa haraka "instant kick of energy"
Juisi ya miwa inauwezo mkubwa wa kuipatia miili nguvu kwa haraka na kukata kiu ya maji. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari "sucrose" ambayo kazi yake kuu ni kutengeneza nguvu mwilini. Kwahiyo wakati mwingine ukiwa na nguvu au uchovu, badala ya kunywa vinywaji vya viwandani tafuta juisi ya miwa.
2. Juisi ya miwa ni nzuri kwa watu wenye Kisukari
Ingawa jusi ya miwa ina utamu inafaa sana kwa watu wenye kisukari. Hii ni kwa sababu juisi ya miwa ina sukari halisi ambayo ina uwezo mdogo wa kuzidisha kiwango cha sukari mwilini au kitaalamu inaitwa "Low Glycemic Index". Kutokana na hilo jusi ya miwa inashauriwa kutumiwa kama mbadala wa vinywaji vingine vya viwandani. Ni mhimu pia kwa watu wenye kisukari kutumia juisi hii kwa kiasi kidogo au kulingana na ushauri wa daktari.
3. Juisi ya miwa inasaidia kupunguza matatizo ya kansa
Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium, magnesium, potassium, chuma n manganese. Madini haya yana uasili wa ualkali ambao husaidia kupunguza uwezekano wa kupata kansa kama vile kansa ya Tezi dume "Prostate cancer" na kansa ya maziwa "Breast Canser"
4. Juisi ya miwa huipatia miili protein
Juisi ya miwa inasaidia kuongeza kiwango cha protein mwilini na ku-imarisha ufanyaji kazi wa figo.
Juisi a miwa iliyochanganywa na maji ya Nazi husaidia kupunguza maumivu hasa yanayosababishwa na maambukizi ya ngono "STDs" na kidney stones.
5. Juisi ya miwa inasaidia kupambana na maambukizi na kuimarisha kinga ya mwili.
Juisi ya miwa husaidia kulinda maini yasipate maambukizi. Hii ndo maana Ma-daktari hushauri matumizi ya juisi ya miwa kwa watu wenye ugonjwa wa Homa ya Manjano,
6. Juisi ya miwa husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula.
Juisi ya miwa ina kiwango kikubwa ch madini ya potassium ambayo husaidia kuimarisha mmeng'enyo wa chakula. Vilevile juisi ya miwa husaidia kuzuia maambukizi katika tumbo na utumbo. Vilevile husaidia katika kutibu matatizo ya choo kigumu au kitaalamu inaitwa "constipation".
7. Juisi ya miwa husaidia kuzuia kuoza kwa meno
Uchunguzi unaonyesha juisi ya miwa husaidia kuzuia meo kuoza na matatizo ya kupumua kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha madini. Kwa hyo kama unafikiria kwenda kwa daltari kung'arisha meno yako, kunywa juisi ya miwa mara kwa mara.
8. Juisi ya miwa husaidia kuimarisha ngozi.
Juisi ya miwa husaidia katika kupambana na mabaka mabaka na kung'arisha ngozi. Juisi ya miwa huweza kutumika kama " face mask na scrub" kwa kuipaka kwenye ngozi na hivyo kusaidia katika kuing'arisha na kuiimarisha.
Hitimisho
juisi ya miwa inafaida nyingi mwilini, ni muhimu kuhakikisha usafi katika utengenezaji wake. Juisi ya miwa isiyokuwa salama inaweza ikawa ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya tumbo na kuhara.
kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi maeneo tofauti tofauti Nchini mwetu na mitaa tofauti tofauti wanaouza juisi ya miwa.
Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa.
Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya.
Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi.
Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya

Mashine waweza pata sido zile zisizotumia nguvu zinauzwa 1.5M lakini pia zipo za kutembeza zenye matairi zinatuma mota ni 2M
Glasi zinapatikana kariakoo
Nasikia biashara ina faida
Nami soon nitakuwa muuzaji ila nitanunua ya kutembeza
=============================================
Juisi ya Miwa: Biashara yenye faida maradufu
Biashara ya kutengeneza juisi ya miwa imekuwa maarufu sana katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania. Hii inatokana na kinywaji hicho kuwa na manufaa mengi katika mwili wa binadamu. Moja kati ya kazi kubwa za juisi ya muwa ni kusafisha mkojo, figo na kutibu homa ya manjano.
Vile vile, juisi ya miwa ni kiburudisho ambacho hukata kiu hasa wakati wa joto. Pia miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa. Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi.
Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo. Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Biashara ya juisi ya miwa ni moja kati ya biashara ndogo inayoweza kuanza na mtaji mdogo lakini ikakuletea faida kubwa kama mjasiriamali kulingana na uhitaji wake. Ili kuanza biashara hii mambo yafuatayo ni ya msingi kuzingatia:
1) Mashine ya kukamua miwa – Tsh 300,000-400,000
2) Glasi nzuri za ujazo tofauti – Tsh 20,000
3) Chujio – Tsh 5,000
4) Beseni – Tsh 8,000
6) Ndoo 2 – Tsh 5,000
7) Jaba kubwa la uchafu – Tsh 12,000
8) Mtaji wa kununua miwa –Tsh 50,000
9) Tolori la kusafirisha – Tsh 60,000
10) Vifaa vingine – Tsh 40,000
Jumla ya mtaji wa kuanzia Tsh 640,000/=
Muwa mmoja unaweza ukatengeneza lita 4 za juisi na muwa mmoja unaweza ukaununua kwa Tsh.300/= kwa bei ya jumla. Lita moja ya juisi utauza 1,000/= hivyo kwa muwa mmoja unatengeneza Ths 4,000/=.
Mjasiriamali anaweza akaongeza ubunifu kwa kuongeza tangawizi au limao katika juisi yake ya miwa ili kuongeza ladha. Biashara hii ni nzuri hasa inapofanyika sehemu yenye mzunguko wa watu wengi kama stendi ya mabasi, masoko, n.k
CHANGAMOTO
- Changamoto zinazomkabili ni upatikaji wa bidhaa hiyo kwa msimu huku baadhi ya watu kutoamini maji anayotumia kutengenezea juisi kama ni salama kwa afya zao.
- Serikali imepiga marufuku vinywaji visivyo pimwa na TBS hivyo wakati mwingine ni usumbufu kwa mjasiriamali mdogo wa biashara ya juisi ya miwa.
- Wajasiliamali wa biashara hii wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa mazingira bora ya kufanyia kazi zao. Mfano uwepo wa wadudu kama nzi na nyuki mahali zinapofanyika biashara hizi.