Uzoefu ambao sitausahau……..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,379
Mnamo Juni mwaka 2009 nilivamiwa na vibaka nyumbani kwangu na kuibiwa vitu fulani fulani pamoja na kujeruhiwa mimi na familia yangu. Tukio lile tuliliripoti Polisi, lakini kutokana na majukumu yangu kikazi, nilizimika kusafiri, hivyo siku ya pili baada ya tukio lile nilisafiri na kumuacha mke wangu akiendelea kushirikiana na askari wa upelelezi ili kufanikisha kupatikana kwa wahalifu hao.Baada ya kuulizwa sana kama kuna watu anadhani au anawahisi kuhusika na uhalifu ule mke wangu, hakuwa na jibu lakini lakini askari yule wa upelelezi alimuuliza kama kuna mtu yeyote mgeni aliwahi kufika hapo kwetu siku za karibuni, ndipo mke wangu akawataja vijana fulani waliotupakia rangi nyumba tuliyokuwa tunaishi juma moja lililopita. Vijana wale walifanya kazi ile kwa siku tatu na walipiga rangi hadi vyumbani ambapo waliona kila kitu tunachomiliki. Kutokana na maswali mengi ya Kipolisi mke wangu alishawishika kuwataja wale vijana watatu na mahali wanapoishi.

Nakumbuka tuliwafahamu wale vijana kupitia kwa rafiki yetu ambaye alitufahamisha kwamba ni mafundi wazuri wa kupaka rangi na wametoka kijiji kimoja. Baada ya vijana wale kutajwa Polisi walikwenda kuwakamata na kuwaweka ndani na kufuatia mkong'oto mkali ili wakiri kwamba ndio waliohusika kufanya mchongo wa kutuletea vibaka watuibie ili wagawane. Bahati nzuri nilirudi siku mbili baadae tangu vijana wale wakamatwe na nilipopata taarifa zile nilikwenda mara moja Polisi na kuwauliza kama walifanya upelelezi na kujiridhisha kama wale vijana walihusika au waliwakamata tu na kuwaweka ndani, Polisi wakadai kwamba wako kwenye upelelezi na wanaendelea kuwahoji watuhumiwa. Nilishirikiana na yule jamaa yangu kuwashikia dhamana wale vijana kisha nikawaomba radhi kwa yote yaliyotokea. Mwezi mmoja baadae nikiwa na rafiki yangu mwingine mahali fulani tukipata vinywaji rafiki yake mmoja alijumuika na sisi, na katika mazungumzo yetu, tukajikuta tukizungumzia wimbi la Taxi bubu zinazotumika kupora watu, yule rafikiye akatusimulia kuwa mwezi uliopita mdogo wake aliona Taxi moja mida ya alfajiri maeneo ambayo siyo mbali sana na ninapoishi wakipakia vitu ambavyo alivituhumu kuwa ni vya wizi, alivitaja vitu hivyo nikahisi kuwa inawezekana vikawa ni vya kwangu kwani mwezi huo ndio na mimi niliibiwa.

Tulimpigia mdogo wake simu akaja na tukamdadisi zaidi. Kwa bahati alikuwa amenakili namba za Taxi ile. Nilikwenda na yule kijana hadi Polisi na kuwapa zile taarifa. Siku tatu baadae nilipigiwa simu kwamba vitu vyangu vimekamatwa na watuhumiwa walioniibia wako ndani. Nilikwenda polisi na mke wangu na kuvitambua vitu vyetu vilivyoibwa.

Tukio hili lilinifanya niwatafute wale vijana kwa mara ya pili na kuwaomba radhi.
 
pole kwa mkasa...lakini kwa sasa hongera kwakua umepata mali zako...
nimejifunza kitu kwako:ww c mtu wa kukurupuka,unafanya vitu kwa utaratibu...swafi mkuu..
 
Afadhari kama ulipata vitu vyako
Mie waliniibia vitu vya thamani sijapata mpaka leo
Mijizi yenyewe iliiba mchana kweupe nikiwa kazini sijui majirani zangu hawakuona tukio na hizi nyumba za mbalimbali ni tatizo...mpaka kesho eti upelelezi unaendelea
 
pole kwa mkasa...lakini kwa sasa hongera kwakua umepata mali zako...
nimejifunza kitu kwako:ww c mtu wa kukurupuka,unafanya vitu kwa utaratibu...swafi mkuu..

Ni kweli, mimi sio mtu wa kukurupuka, lakini nilisikitishwa sana na utaratibu wajeshi letu la Polisi.
Mimi nadhani upo wa umuhimu wa kuangalia historia ya mtuhumiwa kabla ya kuwekwa ndani na kuteswa ili tu akiiri kama alihusika. kwa wenzetu especial nchini Marekani upo utaratibu wa kuangalia rekodi ya mtuhumiwa kwa undani na wakati mwingine huwauliza majirani wa mtuhumiwa kama wanafahamu mwenendo wake kiundani kisha huanza kufuatilia nyendo zake hata kwa wiki nzima mpaka wajiridhishe kwamba huyu anahusika katika kufanya uhalifu huo ndipo hukamatwa kwa ajili ya kuhojiwa zaidi na sio kuteswa na kulazimishwa akiri kosa ambalo pengine mtuhumiwa hakuhusika kulifanya.
 
Pole baba,
Hawa viumbe huwa wanatia hasira sn,
Yani mie hata nikiona wanashuhulikiwa wala siwaonei huruma,walishaniliza siku moja sina hamu nao kbs!
 
Nimecheka utadhani mazuri, pole FL1 ndio polisi wetu wanavyofanya kazi
Wenyewe waambie kuua raia tu wasio na hatia ndo kazi wanayoiweza

Afadhari kama ulipata vitu vyako
Mie waliniibia vitu vya thamani sijapata mpaka leo
Mijizi yenyewe iliiba mchana kweupe nikiwa kazini sijui majirani zangu hawakuona tukio na hizi nyumba za mbalimbali ni tatizo...mpaka kesho eti upelelezi unaendelea
 
Ni vyema kuwa umepata thamani zako zilizoibwa. Utaratibu wa polisi wa bongo ni kuripuwa kazi haraka. Mara nyingi wanakamata wasiohusika. Jaribu kwenda mahabusu na utakuta wengi humo ambao wameswaga ajili ya taarifa za uongo au za mtu abaye ana uadui.

It was a very gentleman of you to ask for a pardon from those painters. Keep up your good heart.
 
bora wewe umepata vitu vyako
mie niliibiwa na taarifa nikatoa
na jinsi wa kuwakamata wahusika nilikuwa nao...
Ila nilifuatilia polisi hadi nimesamehe bure
sikupata ushirikiano hata kiduchu
 
Afadhari kama ulipata vitu vyako
Mie waliniibia vitu vya thamani sijapata mpaka leo
Mijizi yenyewe iliiba mchana kweupe nikiwa kazini sijui majirani zangu hawakuona tukio na hizi nyumba za mbalimbali ni tatizo...mpaka kesho eti upelelezi unaendelea

halafu wewe.....
Mbona story yako kama yangu...

Bora hata weww unafuatilia
mie hata alopewa kesi yangu kufuatilia sijawahi kumtia machoni......
Kila nikimtafuta naambiwa yupo busy...
Nikaamua kuipotezea tu....
 
dah! huku uswahilini kwetu wanakwara kila kitu ukiacha ndala mlangoni wanaiba,ukianika nguo wanabeba!!kha. mi nimeibiwa ndala mpya za batabata mpaka leo sijaziona .......mkuu kwani watuhumiwa walikua akina nani?
MP.
 
dah! huku uswahilini kwetu wanakwara kila kitu ukiacha ndala mlangoni wanaiba,ukianika nguo wanabeba!!kha. mi nimeibiwa ndala mpya za batabata mpaka leo sijaziona .......mkuu kwani watuhumiwa walikua akina nani?
MP.
Walikuwa ni vibaka wa Mabibo mkuu.....................
na walikuwa na mkubwa wao wanamuita BRIGEDIA MANYOTA
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom