security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
DKT. MUHAMMED SEIF KHATIB
Niliwahi kusoma kitabu cha riwaya cha mwandishi maarufu wa Kiswahili wa Zanzibar kiitwacho “SIRI YA SUFURI”. Pia nikatamani mwandishi mwingine atokee na aandike riwaya yenye jina “Siri ya Arubaini”. Nambari “Arubaini” inatumiwa na watu wengi na huwa na kisa, kiroja na mikosi. Tena namba hii hutumika ikihusisha dini, madhehebu, maisha, imani ya ndoa, talaka na misiba. Wapo wanaona kuwa ni bidaa kwa maana ya uzushi. Wapo wanaoamini ni sehemu ya utamaduni na desturi. “Arubaini” hii, haipo kwa Waswahili bali tu ipo kwa jamii nyingi duniani. Hebu tuone mifano michache ya siri ya “Arubaini”. Katika dini ya Uwisilamu, Nabii Mhammad alipata utume alipotimia miaka arobaini. Aidha mmoja ya mitume maarufu, Nabii Nuhu, alitengeneza safina, jahazi ingawa wakati huo hakukuwa na mito wala bahari katika eneo lake. Hata hivyo, safina hiyo ilichongwa kwa miaka “arubaini”. Lakini ikatokeya mvua ya ajabu ya gharika ambayo ilinyesha kwa siku “arubaini”. Nuhu aliwachukua watu wake, wanyama, ndege ndani ya safina hiyo! Waisrael au Mayahudi nao walikaa utumwani huko Misri kwa muda wa miaka “arubaini”. Nabii Mussa alipanda juu ya mlima kwenda kupokea amri kumi za Mungu aliposhuka mlimani aliwaona Mayahudi wakiabudu sanamu la ng’ombe. Mungu aliwapa adhabu na walisafiri jangwani na nyikani kwa mguu na kwa muda wa miaka “arubaini”. Nabii Mussa aliwasaidia Mayahudi na kwenda Sinai. Inaaminika kuwa ule mnara mkubwa wa ajabu wa Babel ulijengwa kwa mkono na vifaa duni kwa miaka “arubaini”. Aidha Nabii Issa au wengine humwita “Bwana Yesu Kristo” alifunga saumu kwa siku “arubaini” na pia alipaa kwenda mbinguni baada ya siku “arubaini”. Sikukuu ya Pasaka nayo huadhimishwa baada ya siku “arubaini”.
Kwa upande mwingine, wafuasi wadhehebu ya Shia, wao huomboleza kifo cha Sayyidna A-Hussein kwa muda wa siku “arubaini” na huvaa nguo nyeusi. Kwa hili katika maombolezo yao wao hufanana na Wakristo. Shia pia huenda Hija yao huko Karbala na siyo Makka kama Waisilamu wengine au kwenda Israel kama Wakristo. Wakiwa huko Karbala na Najaf hija yao Shia huchukua siku “arubaini”. Imani ya siku “arubaini” haipo katika dini, madhehebu na utamaduni tu bali hata katika mambo mengine ya maisha Mama mzazi huku Uswahilini akisha kujifungua, inabidi akaye ndani kwa siku “arubaini”. Baada ya siku hizo ataoga, kuosha nywele na kutoja hina na ataruhusiwa kutoka nje. Kutoka nje huko wengine husoma maulid ya kutoka “arubaini”. Wapo watu wengine hawampi jina rasmi mtoto wao ila baada ya kufika siku “arubaini”. Hata watoto wachanga wengine huwa hawanyolewi nywele mpaka wafike siku “arubaini”. Siku hizi watoto wachanga wengi wanaume hutahiriwa hospitali wakifika siku “arubaini”. Katika misiba ya kufiliwa watu na wapenzi wao watu hukaa matanga na kubaki katika maombolezo kwa siku “arubaini”. Siku ya “arubaini” ikifika husomwa maulid au hitima ya kuondosha matanga. Hata jambo la wizi au uovu watu hukamatwa baada ya siku “arubaini”.
Mwakani Chama Cha Mapinduzi nacho kitatimiza uhai wake wa miaka “arubaini”. Chama hiki cha siasa ni kikongwe, kikomavu chenye hazina ya viongozi wazoevu na wababevu. Umri huu hautaji usuli wa vyama vianzilishi vya Afro-Shirazi Party kilichozaliwa mwaka 1957 na Chama cha TANU kilichozaliwa mwaka 1954. Miamba hii ya vyama vya ukombozi ndiyo iliyokomboa nchi na kuwatimua Waingereza na Masultani kwa nguvu za umma. Miaka “arubaini” ya Chama Cha Mapinduzi kilichozaliwa 1977 kule Zanzibar imechangia sana maendeleo ya taifa letu kupitia awamu mbalimbali za utawala. Miongoni mwa hayo mazuri yalosimamiwa ni kuzijenga sekta mbalimbali za kiafya, kielimu, kijamii na kiuchumi. Hatua iliyofikia taifa hili ikilinganishwa na miaka mingi ya kutawaliwa ni kubwa sana. Chambilecho kama italinganishwa utofauti ni sawa mlima Kilimanjaro na kichuguu. Chama hiki katika miaka “arubaini” kimesimamia amani na utulivu. Chama hiki kimeimarisha uzalendo na utangamano. Chama hiki kimeimarisha utangamano na kuzuia mgawanyo wa kikabila, kirangi, kidini na kieneo. Chama hiki kimejenga hazina ya viongozi shupavu, jasiri, waadilifu na wachapa kazi. Chama hiki kimeruhusu mfumo wa vyama vingi wa siasa na kuulea kwa ajili ya usitawi wa taifa. Bila ya shaka Chama hiki hakiendeshwi na malaika na kwa hivyo hakiwezi kuwa kitakatifu. Mwakani kinatimiza miaka “arubaini”. Kitajitathmini, kujitakasa na kujipanga upya kwa ajili ya usitawi wake na taifa kwa miaka “arubaini” mingine ijayo.
Tumeona jinsi dini ya Kiisilamu, dhehebu la Shia, Ukristo na dini ya Kiyahudi wameipa uzito “arubaini” kiimani. Nao Waswahili katika mila na desturi zao wamehusisha mambo yao na nambari “arubaini” Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi nao wanapaswa kuwekea uzito wa miaka “arubaini” ya uhai wao. “Arubaini” inabeba mambo mazito na muhimu katika maisha.