Uzinduzi wa Ripoti ya Sita ya Tathmini ya kila mwaka ya Kujifunza nchini

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Taasisi ya Utafiti ya Twaweza kuzindua Ripoti ya Sita ya Tathmini ya kila mwaka ya Kujifunza nchini kutoka Uwezo Tanzania.

Uzinduzi huu utafanyika siku ya Kesho Jumatatu tarehe 10 Aprili ukumbi wa Hazina, Dodoma.

Je Ripoti hiyo itaonesha nini?

TUJIKUMBUSHE:

Screenshot from 2017-04-09 13-49-27.png


Hii ni moja ya ugunduzi katika Ripoti ya Tano ya Tathmini hii ya Uwezo.

Je hali hii itabadilika? Na je utoro utaongezeka au kupungua hasa kwa wakati huu ambao watumishi wengi wa umma wanalalamika hali ni ngumu?

Yote haya tutayajua hapo kesho. Fuatilia Uzinduzi moja kwa moja kutoka JamiiForums ambapo tutakuletea matokeo ya utafiti pamoja na majadiliano na uchambuzi wa Ripoti hiyo.
 
Walimu hawana motisha, hakuna nyongeza, malimbikizo hakuna, madaraja kupanda hakuna. Walimu wananyanyaswa sana sasa suala la utoro kwa walimu haliwezi kwisha.
 
Back
Top Bottom