Uzinduzi wa noti mpya BoT 2010

Sio mimi napenda kujua, bali pia na wananchi wenzangu. Hizo note mpya hazina tofauti ya uthamani ukilinganisha na na current notes. Dhumuni lao ni nini lakubadili? hakuna maelezo ya namna hiyo. Kubadilika kwa note basi kungeambatana na ongezeko la noti za elfu hamsini ''50,000'' na laki moja ''100,000''. Suala ni kukubali kuwa bado thamani ya pesa Tanzania iko chini na inazidi kuwa chini.

Ngoja niwastue wadanganyika wenzangu maana hili jambo watu wanalichukulia juu juu lakini ni issue kubwa na inahitaji ijadiliwe kwakina kwani inawezekana kuna motives hazifahamiki na muhimu zikajulikana. Kuna sababu za ziada kama tatu au nne zinaweza kuwa zimepelekea kubadilisha sarafu za wakubwa hawa lakini hawasemi :-

a. Kuondoa pesa chafu kuna uwezekano kuwa pesa feki zimezidi katika mzunguko na wao hawafahamu au wameshindwa kupambana nazo. Hili linaweza kuondolewa only by introducing new currency ili kuziondoa hizo pesa chafu. Hayo yamewahi kutoka hata katika developed countries mfano UK walipata tabu na £50 , £20 currency notes wakachapisha mpya kwakuwa watu walikuwa wanachapisha pesa feki za UK zikawa ngumu kutoka wakatoa notes mpya ili kuzifuta na kuziondoa zile pesa feki.

b. Quantitative easing. Kuingiza pesa katika mzunguko wa fedha nchini. Kutokana na serikali kuzidiwa na haina pesa wanaweza kubadilisha pesa ili wakiziingiza sarafu mpya waongeze mzunguko wa pesa katika nchi. Njia hii inaweza kufanyika vilevile kujaribu kucontrol sarafu ya Tanzania isishuke. This could be a smart move by the central bank but itaweza kuwork out kama wanaplan vp wanaweza kumaintain sarafu ya shilingi isishuke once mzunguko wa pesa ukifika katika uchumi. Hii nina maana purchasing power ikiwa kubwa na inflation pressure ikazidi tunaweza kuona thamani ya sarafu inatetereka na matokeo ni shillingi kukosa mwelekeo.

c. Kubadilisha pesa huku pia kunawezekana kuwa dili la wakubwa wachache maana gharama zake za kuchapisha pesa mpya ni kubwa sana. Hivyo ni wema wakubwa watujulishe imekuwaje na watufafanulie na sio Professa Ndulu kutwambia gharama zake hajazijua mpaka sasa. Hili litasaidia wabunge wa upinzani kufatilia na kuhakikisha hakuna mianya ya ufisadi haijapita katika kujadiliwa swala kama hili.

Hapa natumai nimewafumbua kidogo.......
 
In africa you just don't ask anything coz the men in the government does everything for you in good faith! teh teh...
 
Back
Top Bottom