Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezindua rasmi kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 kupitia tiketi ya CCM leo, Agosti 28, 2025, katika Viwanja vya Tanganyika Peckers, Kawe, Dar es Salaam.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho amesema, "Najua kulikuwa na maneno eti utaratibu umekiukwa na mimi nililaumiwa kwa jinsi nilivyosema kwenye Mkutano Mkuu, lakini waliokuwa wanasema hayo ama hawafahamu utaratibu wa chama chetu, au labda wamesahau, au wanajifanya hamnazo"
"Tumejiwekea utaratibu kwamba Rais wetu aliyepo madarakani anapomaliza kipindi cha kwanza na akataka kipindi cha pili huwa anapewa nafasi pekeyake".
"Rais Samia ni kiongozi mwenye maono ya mbali, 4R zake zimeimarisha Amani, Umoja na Muungano wetu"
==
Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliichukua nchi ya Tanzania katika kipindi kigumu kilichohusisha majanga matatu — ugonjwa wa Corona, kifo cha Rais John Pombe Magufuli, na anguko la kiuchumi la dunia."
"Kwahiyo Rais Samia anachukua uongozi wa nchi katika mazingira hayo ya majanga matatu, nchi ilitikisika, na kulikuwa na mawazo mseto na hofu."
==
Mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM, Samia Suluhu, amesema, "Kwa upande wa mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, Serikali imejitahidi kuimarisha taasisi za mdhibiti, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili ziweze kufanya kazi zake kwa umahiri."
Akaongeza, "Kwa upande wa ukaguzi wa hesabu za serikali mwaka 2021 tulikuwa na hati chafu 10 na hati zenye mashaka 81. Leo, miaka minne baadaye, hati chafu imebaki moja tu, na hati zenye mashaka zimepungua hadi kufikia 5."