Uzinduzi wa kampeni za CCM Chalinze wadoda

Uzinduzi wa kampeni za CCM Chalinze wadoda

Status
Not open for further replies.

chadema kote

Senior Member
Joined
Feb 17, 2014
Posts
177
Reaction score
25
Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Chalinze umedoda.Hamasa kubwa iliyofanywa kwa kutumia magari ya matangazo na mashangingi imepata mwitikio mdogo.Mbaya zaidi Mvua kubwa inanyesha muda huu na kuzima kabisa ndoto ya kupata wahudhuriaji angalao wachache wa kusikiliza hotuba za ufunguzi.CCM wanafanya mkutano wao eneo la Miono ambapo ni nyumbani kwa Mbunge aliyetangulia Said Bwanamdogo.

Wazigua na wa Kwere wenye msimamo wa wastani wamesusia mkutano huu kwa kuwa hawaridhishwi na mazingira ya kifo cha Mbunge wao ambaye anaaminika kuwa alifanyiwa hujuma kwa sababu za kisiasa ili mtoto wa mwenyekiti wa chama arithi jimbo aliloshikilia baba yake kwa sasa kabla ya baba yake kuondoka madarakani.

Pia hoja kubwa ni kuwa baba yake mgombea wa CCM alikua Mbunge kwa muda mrefu na hakufanya kitu,iweje Said Bwanamdogo aliyejitahidi miezi 12 ya kwanza kufanya kazi za maendeleo akwamishwe na wakubwa na kisha kumuondoa kabisa duniani halafu leo aibuke mtoto wa Mwenyekiti na kutoa ahadi kuwa atamalizia ahadi za Marehemu Said BwanaMdogo? Wazigua na Wakwere wenye msimamo wa wastani wanasema hii ni laana kwa mujibu wa mila na tamaduni zao.
 
Kazimue kwanza na pombe za asubuhi kisha urudi hapa tuongee! Tuachie Chalinze yetu huijui wewe.
Hicho ulichokiandika inawezekana kikawa kinawakilisha ule usemi wa kuwa UKWELI UNAUMA maana ulichotakiwa kujibu hapa ni kuuelezea umma wa JF kama mleta mada alichoandika ni uongo au kweli. au kwa kuwa tunaambiwa huko kwenu wengi mna vichwa vya nazi basi na wewe kichwa chako ni cha NAZI.
 
Kwa mtu yoyote mwenye akili timami anajuwa duhahiri Ridhiwani ndio atatakuwa mbunge wa chalinze kinachofanyika sasa ni political process tu.
 
Tulikuwepo na vyombo vya habari vilikuwepo! Angalieni. Taarifa ya habari ndiyo mtajua mtoa uzi muongo.
 
tatizo ndugu zangu mnajiaminisha vibaya kuwa mtt wa rais nae nirais aya mambo yalikua enzi za mkoloni kwasasa vijana wanawai kubalee na wanajua umuimu wa kiongozi kwaiyo ata wewe matola mulize uyo rizi kama apa nipalaini kama unavyo fikiri najiulize wewe lini baba yako atakuwa mwana siasa ili upewe nafasi yakugombea kwani tunaona sasa ni stail arumeru mtt wa marehem sioi kalenga mtt wa marehem god chalinze mtt wa kikwete wewe je usiwetu mshabiki jiulize wewe kesho itakuwaje
 
Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za CCM Chalinze umedoda.Hamasa kubwa iliyofanywa kwa kutumia magari ya matangazo na mashangingi imepata mwitikio mdogo.Mbaya zaidi Mvua kubwa inanyesha muda huu na kuzima kabisa ndoto ya kupata wahudhuriaji angalao wachache wa kusikiliza hotuba za ufunguzi.CCM wanafanya mkutano wao eneo la Miono ambapo ni nyumbani kwa Mbunge aliyetangulia Said Bwanamdogo.

Wazigua na wa Kwere wenye msimamo wa wastani wamesusia mkutano huu kwa kuwa hawaridhishwi na mazingira ya kifo cha Mbunge wao ambaye anaaminika kuwa alifanyiwa hujuma kwa sababu za kisiasa ili mtoto wa mwenyekiti wa chama arithi jimbo aliloshikilia baba yake kwa sasa kabla ya baba yake kuondoka madarakani.

Pia hoja kubwa ni kuwa baba yake mgombea wa CCM alikua Mbunge kwa muda mrefu na hakufanya kitu,iweje Said Bwanamdogo aliyejitahidi miezi 12 ya kwanza kufanya kazi za maendeleo akwamishwe na wakubwa na kisha kumuondoa kabisa duniani halafu leo aibuke mtoto wa Mwenyekiti na kutoa ahadi kuwa atamalizia ahadi za Marehemu Said BwanaMdogo? Wazigua na Wakwere wenye msimamo wa wastani wanasema hii ni laana kwa mujibu wa mila na tamaduni zao.

Vita ya Chalinze ni kati ya Mtandao wa Lowasa na Kikwete!!
Wakati ule wa Arumeru Lowasa alijaribu kumutetea mkwe wake Sioi Sumari kwenye jimbo laki klaini Ridhiwani kikwete alitumia Nguvu ya Ikulu kwa Mgongo wa Baba yake na Kumokomoa Lowasa leo yametimia .Ridhiwani anagombea nyumbani kwao ambapo anamrithi Baba yake Kikwete ni dhahiri kwamba vita ina endelea!!
 
Kwa mtu yoyote mwenye akili timami anajuwa duhahiri Ridhiwani ndio atatakuwa mbunge wa chalinze kinachofanyika sasa ni political process tu.

Matokeo tayari anasubiri kutangazwa mshindi tu.
 
Chopa 3 kata 3....sasa muziki wa kalenga unaenda kuchezwa chalinze...ni kijani tuuuuuuuuuu
 
Wakwere wako hoi chalinze, wapende wasipende mtoto wa jakaya ndo mbunge wao mpya! Wajiandae kulishwa pilau na wali kwa kubadilishana na kura zao!
 
Bilq picha mkuu unanifanya nikutilie mashaka.

Ili tuwaonyeshe magamba hali si nzuri kwao weka picha.
 
Wakwere wako hoi chalinze, wapende wasipende mtoto wa jakaya ndo mbunge wao mpya! Wajiandae kulishwa pilau na wali kwa kubadilishana na kura zao!

Hivyo vikabila ni vya wapumbafuuu tu hawanaushawishi wa Maendeleo
 
Mtoto wa rais ni raisi tumawapima WAKWERE NA WAZIGUA.Bado mna mfumo wa machifu na kurisishana uongozi.
 
viongozi wa ccm wamelewa madaraka.kikla kukicha hawatamani kujua kuwa wanachama wote wana fursa sawa. Nawapeleka tu katika historia ambapo uchaguzi wa Arumeru alisimamishwa Sion, udiwani wa majuzi sombetini Arusha alisimamishwa mtoto wa aliyekuwa diwani Mzee Musa Mkangaa, Ubunge wa bunge la Africa Mashariki mtoto wa mwinyi, Waziri aliyeonekana mtoto David Mathayo ni mtoto wa Mzee Cleopa Msuya,Watotot wa kawawa wamefanya bunge ni ofisi ya nyumbani maana yupo Vita Kawawa na Zainabu Kawawa mbapo mdogo wao anagombea 2015.Ukija familia ya Kairuki ndo usiseme kila mtu amewekwa sekta nyeti. najiuliza mtoto wa Kabwela ni nani atakaye niona????Unless niwe snitch, niuze unga kama wao,au kaka ama dada yangu ajitose kingono kwenye koo zao. Ona sasa Rais Jakaya, shemeji yake waziri wa mambo ya nje, binamu 3 wabunge, mama Chiku mkurugenzi, mama fatma mkurugenzi, na wengine wewe. Wewe kijana uliye ndani ya ccm baba yako sio hata kiongozi wa serikali za mtaa utatokea wapi???Wakwere wenzangu mtaendelea kucheza ngoma wenzenu wananeemeka.Ona watu wa pwani tulivyo masikini, elimu duni,ajiri ndoto,tunabaki kula ubwabwa wakati wa Idd na wakati wa kampeni. Loooo sitaki tena
 
Waswahili safari hii CDM itawaelimisha hivyo hivyo japo kuwa wajinga ni wengi na wamekumbatia dhiki na hawataki kuziachia. Tutaenda nao hvyo hivyo kibishi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom