Uzinduzi wa Halotel: Tusaidiane Kukonekti Dots

Uzinduzi wa Halotel: Tusaidiane Kukonekti Dots

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,278
Hivi ndivyo ninavyofikiria: Siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu.Mtandao mpya wa simu unazinduliwa. Watanzania wengi wanailalamikia sana mitandao iliyopo; Voda, Tigo, Airtel n.k. Wapo wengi watakaopenda kujiunga na mtandao mpya: Halotel.

Ukinunua line ya mtandao lazima ujiandikishe. Katika kujiandikisha wapaswa kutoa kitambulisho. Mojawapo ya kitambulisho kinachokubalika ni kile cha kupigia kura. Kwa hiyo mteja mpya wa mtandao atatoa kitambulisho chake cha kupigia kura. Na uchaguzi ni siku kumi au tisa baada ya kununua line mpya. Konekti dots hapo.

Naomba kama unataka kununua line ya mtandao wowote, fanya hivyo baada ya uchaguzi.

Wapo watakaonielewa sana na wapo watakaotoka kapa kwenye thread hii.
 
Tumekusoma mkuu ni moja ya zile mbinu zao ambazo mwezi huu zinadunda na naskia mmiliki ni IGWE. Hapa shida tu
 
Nimesikia huu mtandao ni wa CCM.
Na cha ajabu wamejenga ofisi kila mkoa hata huduma hawajaanza kutoa.
Kwa mkoa wa pwani nadhani hata wateja 200 hawajafikisha ila wana ofisi moja matata sana. Hata hawa kina voda na tigo hawana.
 
Tumekusoma mkuu ni moja ya zile mbinu zao ambazo mwezi huu zinadunda na naskia mmiliki ni IGWE. Hapa shida tu

Upo sawa mkuu mmiliki halisi ni IGWE alitaka pia kuinunua na Sasatel.
 
Ngumu kumeza ila kuna kitu cha kujifunza hapa........

Baada tu ya uchaguzi 2010, mwanzoni mwa 2011 alijitokeza babu wa Loliondo. Nae alikua ameanza 'mradi' kama mwezi hivi kabla ya uchaguzi. Nasubiri kwa hamu picha la Halotel (au lolote lingine) baada ya uchaguzi huu ikiwa kwa miujiza CCMscrow itashinda.......
 
Take it from ombeni lowassa ashinde!
Akishinda tu ofisi zao zote yatabaki magofu! ! IGWEEEEEEEEEEEEEE
 
Hii thread inauzito mkubwa sana!! 83.5% true
 
UKAWA kuanza kutafuta kila aina ya sababu ni dalili za kushindwa, natanguliza pole kwenu
 
Nimesikia huu mtandao ni wa CCM.
Na cha ajabu wamejenga ofisi kila mkoa hata huduma hawajaanza kutoa.
Kwa mkoa wa pwani nadhani hata wateja 200 hawajafikisha ila wana ofisi moja matata sana. Hata hawa kina voda na tigo hawana.

Arusha wamechukua firstflour ya jengo fulani hapa Arusha jirani na Posta. Huduma zao very expensive cheap.
 
Daftari lishatolewa hivyo hapatakuwa na mabadiliko yoyote yale
 
Acheni propaganda nyie...mimi nimenunua line na nimesajili kwa kitambulisho changu cha uraia....au nyie ni mawakala wa baadhi ya mitandao...!
 
Sasa copy ya kitambulisho wakishachukua itakuzuia vp kupiga kura! Matokeo na majina yatakuwa pale kituoni. Acheni ulofa.
 
Mi nadhani kitambulisho sio lazima cha kura hata leseni ya udereva , cha uraia , so hapo kidogo nashindwa kuconnect dot.
 
Back
Top Bottom