warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,273
- 18,422
UZINDUZI wa albamu ya saba ya mkongwe wa Muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura a.k.a Jide, iitwayo Woman utafanyika katika viwanja vya Jeshi vilivyopo Lugalo maarufu kama Golf Ground, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa mwanamuziki huyo, Seven Mosha, alisema jana kuwa wamechagua eneo hilo kwa sababu ya ukubwa wa uwanja wake, sehemu nzuri ya kuegesha magari na bila kusahau kuwa usalama wa kutosha.
“Tumeangalia vigezo vingi katika kufanya uchaguzi wa sehemu ya kufanyia shughuli hiyo, unajua tunategemea watu wengi kulingana na mtu mwenyewe, albamu itakuwa na nyimbo kumi na katika siku hiyo, atapiga karibu nyimbo zake zote zilizompatia umaarufu ndani na nje ya nchi,” alisema Seven, ambaye pia anamsimamia Kiba.