Mtzed Wakiafrika
Member
- May 8, 2018
- 6
- 1
Kutoa habari zisizo za ukweli na uhakika, Watumiaji mbalimbali huposti taarifa zisizo za ukweli na nyingine zakichonganishi kutokana na kutokujali matokeo ya taarifa hizi.
Wengine hata kulipwa na kushawishiwa na vyama gombea kueneza sifa mbaya juu ya serikali iliyopo madarakani. Hapa utaona nimeviita vyama upinzani vyama gombea kwani ni kweli na naamini ni harakati tu za kukizidi chama tawala walakini basi tuangalie uhalisia wana nchi yetu hata na nchi zilizoendelea; baada ya uchaguzi ni mwendo wa “Majority Rule, Minority Right”.
Hivyo sio muda wakuendelea na kampeni/ siasa dhidi ya chama tawala kilichoshinda uchaguzi waliopambania wote bali ni muda wa vyama vyote; Waliowengi kutawala na waliowachache kupata haki yao kushirikiana. Ushirikiano wa kulijenga taifa kwa kuleta hoja za maendeleo bungeni na utendaji nyakinifu kulijenga taifa ikiwa ni pamoja na kutunza amani na usalama nchini.
Nikikumbuka trend za mada ya maandamano yaliosemekana kuwa ni ya Mange Kimambi kutokana na taarifa kadha wa kadha alizotoa kupitia mtandao wakijamii unaojulikana kama Instagram. Aliwafikia wengi na kufikia kiwango cha kuongelewa na viongozi wa Tanzania na balozi mbalimbali nchi za nje ikiwemo Sweden, Uingereza, Australia yaani taswira nzuri ya nchi kuchafuka ulimwenguni kote!
jE Tunajenga tunabomoa?