Uzi mchungu kuliko yote humu MMU

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Nimekosa Heading ya kuweka hapa ndugu zanguni

Just imagine, wanakaa kitako kuwajadili waume zao. Boya mmoja anapiga simu kwa mkewe kuulizia maendeleo yake na mwanae, anawekwa loud speaker, baada ya maongezi simu inakatwa, wanaangua kicheko kwa pamoja, kisha mwanamke anatia maneno, "Msimuone anazungumza kwa busara kwenye simu, kitandani hakuna kitu, akinitutumua sana ni kifo cha mende" wakaangua kicheko, akajazia "unadhani pesa anayo, hana pesa, huyo siyo type yangu, basi tu". Mwenzie ndipo kudakia, "Mimi mume wangu ana pesa sana, sema simpendi hata kidogo, nilipenda pesa zake tu, yaani hata akinipumulia kwenye sikio nahisi mabomu ya mbagala". Wakacheka saaana
________________________

Huyo mwenye mtoto anawaambia mashosti wake, nishikieni mwanangu kuna mahala naelekea. Mashosti wanaangua kicheko cha kiswazi, mmoja wao anasema, "Naona unakipeleka kwa Mudy", anajibu, "Yaani kama vile unalala na mimi, wacha akakipondeponde, tulipewa bure, wacha kikafanye kazi yake". Binti anaondoka hivyo. Wanaangua kicheko cha kinafki na kuanza kumhurumia mumewe kwa huruma za kashfa

Muda huo niko kwenye gheto langu nawasikilizia tu
N.B: Kibarua changu kiliota nyasi
_________________________

Mara naisikia sauti ya kibinti kimoja hivi machepele, cheupe, sauti ya kukifu isiyo na vituo, bila kusahau hakina hata choo

"Kile kikaka kichora tatoo, japo nafanya kupretend mapenzi, kinanisaidia matumizi madogo madogo, kipo ladhi kisile, kilale na njaa ili tu mimi nile, halafu mpaka waleo sijawahi kukigea mzigo", wanaangua kicheko kizito. Mmoja wao anazungumza, "Wanaume ni wapumbavu sana, wadhaifu, wacha tuwapeleke kindakindaki, kuna boya moja huwa linabeba zege linapata 10k kwa siku, lilivyo lijinga linanigea 5k, lina familia halafu mama yake analitegemea". Wanaangua kicheko ndoige kiasi kwamba mmoja wao anabanja kabisa, wanacheka kwa mara ya pili kumcheka mwenzao
_______________________

Mmoja wao akadakia, achaneni na huyo, hivi hiki kikaka kinachotabasamu kama kimeona bia za ofa kipo? "Kimetoka, lakini siku hizi hakina mchongo, kimechanganyikiwa sana". "Hivi huwa kinaitwa kinani vile!!?". Wakaaangua kicheko tena, kisha mmoja wao akasema, "Unataka kutuambia, umemsahau mpenzi wako jina?" Mmoja akadakia, "Aha, mnamsemea Melki?" Wakaangua kicheko, binti akasema, "Siezi deti na vitoto mimi, kijana mwenye 30 yrs hapaswi kuwa kwenye mahusiano na mimi, huwa wanaendekeza wivu sana". Wakaangua kicheko, "Laiti angewajua watu anaoshare nao penzi, sijui ingekuwaje". Kukasikika ukimya kidogo, baada ya hapo nilisikia neno "Tobba", wakaangua kicheko tena kwa nguvu, yaani kicheko Pro Max, "Ndo hivyo, atafute hela"

Conclusion:
Kuanzia sasa sintopenda tennna, naanza kuhudhuria zile kambi zetu pendwa, wazo la kuoa nimefuta, nikikuta wanawake wamekaa vikundi nacharaza bakora wote

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom