Uzi kwa wanaume wote

Mkuu, ukitaka kufanya hayo unayoandika oa mwanaume wako.
Lakini kama unasubiria nikutongoze, nikatafute mbuzi na hela nilete kwenu Tena wengine wazazi wenu wanapanga Hadi mil 10 siku hizi.
Yaani mahari tu unanunua uwanja na kusimamisha msingi!!
Ndio maana unahamishwa kwenu kuja kwetu. We own you kwa muda huo.
Ndio maana hata nikifa Mimi utaendelea kwenda kwetu na ukifa unazikwa na familia yangu.
Vinginevyo ingekuwa tukikutana tunaendelea kuishi bila hata Mambo ya mahari ndio ingewezekana.
 
Jisemee nafsi yako mkuu na ndo maana nikakwambia wapo wanaume wameoa wanawake ambao hadi sisi wanawake wenzao tunawaonea huruma hao wanaume tunasema hivi pale walifuata nini? Hakuna mwanamke anayependa kuwa mjeuri kwa mumewe ila sasa kama wananyanyaswa?

Unadhani kuna binadamu anayependa kunyanyaswa? Hakuna halafu hapo kwenye swala la kusema eti mnatumiliki kisa mnatoa mahali yaani hapo ndo umepuyanga kabisa yaani millioni kumi ndo zifanye umtese mtoto wa watu?

Kwanza wanaume wengi siku hizi hawatekelezi majukumu yao kama wanaume wanataka kila kitu wasaidiwe na wake zao mahitaji ya nyumbani wanatoa nusu kwa nusu ada za watoto wanatoa nusu kwa nusu yaani kila kitu nusu kwa nusu bado tena mwanamke amhudumie mume

Yaani hadi mnakufa mnajikuta mke kashailipa mahari yote uliyomtolea na hela imezidi kwa sababu tu ya kusaidia majukumu ya mume kwahiyo kama mnaona mnatumiliki sababu ya mahari mnazotoa basi pia timizenu majukumu yenu kwa wake na watoto wenu vinginevyo mtaendelea kulalamika tu na hao wanawake mnaosema hawafai kuolewa ndo kila weekend tunahudhuria harusi zao wanaume wenzenu wanawaoa
 
Ndio maana kesi za kudai talaka zimekuwa nyingi.
Kwa sababu wanaolewa hata waliotakiwa kuwa wajakazi.
Sio wanawake wanatakiwa kuwa kwenye ndoa.
Kwa sababu ya bahatisha bahatisha inayotokea Basi taasisi ya ndoa imeingiliwa hata na makahaba.!!
 
Ila kwa wanaume unataka kusema kwamba hata wale wanaume wahuni wasiojielewa nao wanatakiwa kuoa si ndiyo?
Ndio maana kesi za kudai talaka zimekuwa nyingi.
Kwa sababu wanaolewa hata waliotakiwa kuwa wajakazi.
Sio wanawake wanatakiwa kuwa kwenye ndoa.
Kwa sababu ya bahatisha bahatisha inayotokea Basi taasisi ya ndoa imeingiliwa hata na makahaba.!!
 
Yap kam mm wakwangu ni "Kasuku" ila cku mojamoja narud kw maEx wangu"Dettlo & Medicated Soap"..Nazan kada watiifu mmenielewa...CHAP.....Oyeee!
NOTE.Tunatest mitambo tu,hamuachw Mamy jus is BRN(Big Result Now)
 
Ila kwa wanaume unataka kusema kwamba hata wale wanaume wahuni wasiojielewa nao wanatakiwa kuoa si ndiyo?
Ujue mkuu nature is very clever.
If we let things happen naturally bila kuwekeana sheria anayetakiwa kuoa mitala kulingana na uwezo wake ataoa na asiyekuwa na uwezo ataoa mke mmoja.
Mwingine hataoa kabisa kwa sababu hajielewi.
Na mwanamke ataolewa na mwanaume anayemuhitaji kwa kutoshelezwa mahitaji yake.!!
Miaka yote ya huko nyuma almost Africa nzima kumekuwa na practise ya kuoa mke zaidi ya mmoja na hakujawahi tokea imbalance kwamba Kuna upungufu wa wanaume.!
Mlipoanza kuja na sheria za kufikirika ndipo shida ya watu kushinda makanisani kuombewa waolewe zikaanza.
Na wengine wamegeuzwa vimada wa wachungaji na hawaoni kuwa Ni dhambi.
Ila akiolewa ndoa ya mitala kwake ndio dhambi.
Dini zenyewe mmekaririshwa tu baadhi ya vipengele ndio mnataka kusimama na kuongea kuwa "biblia inasema"
Ha ha ha ha
 
Wanaume bwana mnasema nyie ndo waamuzi wa mwisho kwenye hii dunia na kila mnachoamua wanawake wanatakiwa wafanye sasa nashangaa huu mfumo wa haki sawa mnaosema umeanzishwa na wanawake mbona hamjaupinga

Matokeo yake mnaishia kulalamika tu iko wapi ile nguvu yenu na mamlaka yenu mliyopewa juu ya wanawake ya kuwaamrisha badala ya kuwalalamikia na nyie siku hizi mmekuwa walalamikaji kama sisi tu halafu bado mnataka kujifananisha na wanaume wa zamani jamani
 
Ukiona mwanaume analalamika Sana kuhusu mwanamke ujue kalelewa na mama Sana.
Mwanaume aliyekuzwa na baba hawezi lalamika wakati anajua mamlaka Ni ya baba.
Ni kutoa maagizo na kukagua utekelezaji.
Yale ya kiume anayafanya mwenyewe mpaka yanatekelezeka.
 
Basi ndo uone sasa kwamba siyo wanaume wote wapo kama mnavyojisifia yaani mimi kitendo cha kuwepo tu baadhi ya hao wanaume tayari nafurahi sana maana wanaume mnajiona miungu watu
 
Basi ndo uone sasa kwamba siyo wanaume wote wapo kama mnavyojisifia yaani mimi kitendo cha kuwepo tu baadhi ya hao wanaume tayari nafurahi sana maana wanaume mnajiona miungu watu
Ha ha ha.
Mkuu unaonekana Ni mtu wa biblia, decent fulani Ila uko spoiled na maneno ya wapigania haki sawa.
Wanaume wa hivyo hawawezi kukosekana.
Ndio maana wengine wamehama kambi kabisa na kuwa mashoga.
Wengine wamekuwa transgender.
Usishangae. Lakini wanaume wenye masculine male character bado tupo wengi Sana tu. Na tunaendelea kufaidi ambavyo wengine wamevikimbia.
Ukitaka kuwa na ndoa yenye amani na furaha Kama umeolewa, play your part as a woman.
Kama mama wa nyumbani kaa nyumbani uhakikishe familia inastawi.
Usilete kero zisizokuwa na miguu kwa mumeo.
Kama unafanya kazi maana Kuna majukumu huyafanyi ya nyumbani na mbadala wake Ni hiyo kazi.
Basi mumeo aone matunda ya hiyo kazi unayoihangaikia asubuhi mpaka jioni.
Sio mtu familia inatunzwa na house girl aafu hata matunda ya kazi yako hayaonekani.!! Acha kazi ukae nyumbani uone Kama hutatunzwa.
Na Kama hujaolewa nakuonea huruma Kama unatamani kuja kuolewa ni hiyo misimamo ya haki sawa. Hakuna mwanaume anavumilia huo ujinga.
Labda Kama utaamua kuwa mkabaji wa waume wa wenzio ili wakuridhishe na kukuzalisha, hiyo haina shida.!!
 
Sasa mkuu ulikuwa wapi kuongea haya yote muda wote huo yaani tumezunguka kote huko ila mimi nilikuwa nataka hili jibu tu kwamba mwanamke kama anafanya kazi za ndani zote peke yake basi hatakiwi kabisa kutafuta pesa ila kama anatafuta pesa basi hatakiwi kabisa kufanya kazi za ndani sasa hapo ndo tumeelewana

Ila bado kuna wanaume vichwa ngumu wanataka hata kama mwanamke anatafuta pesa basi kazi za ndani bado azifanye kama kawaida kwa maana kwamba mwanamke ndo atakuwa amebebeshwa majukumu mengi kuliko mwanaume

Sasa hapo wazo la kwamba sisi ni wasaidizi wenu litakujaje ikiwa majukumu mengi ndo tunafanya sisi kuliko nyie yaani ni sawa na makamu wa rais afanye majukumu mengi kuliko rais sasa hapo atakuwa msaidizi tena?

Ndo maana hata utii unakosekana kwenye ndoa sababu ya majukumu wanaume kiujumla ndo mna majukumu mengi kuliko sisi ambao tuliumbwa kuwasaidia tu hivyo huo utii unakuja baada ya kutimiza majukumu yenu yote ipasavyo na siyo kutegea mke ndo afanye kwa kiasi kikubwa
 
Kwanini ziumie ikiwa yeye anapata utamu hapo ndipo ninapowashangaaga wanaume yaani mtu kitu amekubali kufanya kwa hiari yake mwenyewe useme anaumia unless otherwise awe amebakwa
Shangaa hata wewe
 
Wala hujakosea mkuu
 
Napita tu, naelekea kula IDD.....!
[emoji124][emoji124][emoji124]
 

Okay mine is more like the same with you, ila mimi najikutaga nawala tena tukimit...ila hilo la ugomvi mimi sitak kwanza hata utafute sababu ya ugomvi hautapata, hata utume mitusi january december me nakausha kau, yan ndio kwanza nakuomba msamaha na hii inaipaga advantage sababu wanawake wanakuaga very open kwangu, yan wanafunguka...MTIHANI MKUBWA NI WAKIINGIA KWENE 18 nashindwa kuwaacha sijui kwanini...
 
Hahaha
Mkuu, Kuna kazi za baba ndani ya ndoa na majukumu ya mama.
Ukiona baba anakwepa majukumu makuu Basi ana shida.
Mama Ni msaidizi.
Hili neno Lina maana kubwa Sana.
Na Kuna mistari kwenye biblia inaongelea kabisa kuhusu mama kutafuta chakula Cha familia.
Kama unafanya kazi Basi unatakiwa umsaidie mumeo baadhi ya vitu vya kutatua. Sio pesa yako inaishia kwenye mawigi.
Unataka pesa ya baba ijenge nyumba, inunue gari, isomeshe watoto, isaidie ndugu.
Hata mboga ndani ya nyumba inasubiririwa pesa ya baba.!!
Unafanya kazi ya Nini!?
Kaa nyumbani ili uitunze vizuri familia.
Maana kutakuwa hakuna utofauti.
 
Ndiyo mwanamke anayetafuta pesa anatakiwa asitumie peke yake bali amsaidie mumewe endapo tu mke huyo hatafanya kazi za ndani na kama akifanya kazi za ndani basi wafanye wote na mumewe

Ila tofauti na hapo jamii itaendelea kulalamika kuwa wanawake ni wabinafsi eti sababu pesa ya mke ni ya mke na ya mume ni ya wote ndiyo sasa kama mke anatafuta pesa na kazi zote za ndani anafanye peke yake mume anataka afanye nini zaidi ya kuhudumia familia nzima peke yake hakuna namna
 
Aiseee!!
Nimekuambia mawazo yako yako spoiled.
Kwa hiyo unataka tugawane majukumu ya ndani ya nyumba.?
Iwe 50/50?
Ujue huwa hatuwaoi ili mje tusaidiane majukumu yoyote ya familia.
Kuna kazi za mama na kazi za baba.
Usiingilie majukumu ya baba. Utabebeshwa mzigo.
Muachie baba majukumu yake na wewe fanya yako kama mama.!!
Mbona kwenye biblia unayoisoma wametenganisha hivyo vitu?
 
Sasa mkuu kwani si ndo nilichosema au? Kwamba kama baba anatafuta pesa na kuhudumia familia peke yake basi hata mama naye afanye kazi za ndani na kulea familia peke yake ila hicho unachosema wewe hakipo kwenye dunia ya sasa kwa sababu

Familia nyingi sasa hivi baba na mama wanatafuta hela na kuhudumia familia 50/50 tena familia nyingine mama ndo kamzidi kipato baba sasa kwenye familia kama hizo kwanini baba naye asisaidie majukumu ya mama? Tatizo ndo hilo wanaume kufanya kazi za ndani huwaga mnaonaje sijui yaani sijui mnahisi mnatabadilika jinsia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…