Patriot
JF-Expert Member
- Feb 11, 2008
- 5,703
- 4,697
Nimekuwa nikipita kona nyingi za ofisi za TRA nakuta mihangaiko ya watu wakibadili TIN number kwa amri ya TRA. TRA inawapa watu deadline wakati ni wao wenyewe walitoa hizo TIN za mwanzo.
Siyo mara ya kwanza kwa TRA kujipangia mambo yao wenyewe na kuwaingiza garama wananchi ambao ni wateja wao. Miaka ya nyuma walibadilisha namba za usajili wa magari kwa sababu zao na kuwaingiza wamiliki kwenye matumizi yasiyo ya lazima. Baadaye mitaani wakaipa kampuni moja kutengeza number plates na ikachukuwa muda mrefu wakifukuzana na watu mitaani.
Haya ni mazoea mabaya na binafsi naona kama uzembe wa kiutendaji, bila kujali lengo lao ni lipi. Kuna tatizo la uwezo wao kuamua na mambo kwa masrahi ya wananchi. Acheni kuwapa dealine wananchi kwa makosa yenu.