Uzembe: Ujumbe kutoka CRDB bank!

Uzembe: Ujumbe kutoka CRDB bank!

Chemiker

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2013
Posts
506
Reaction score
108
Ndugu Mteja,

HENRY JOS*** MALU**.Sasa unaweza jiunga na SIM Banking. Namba yako ya siri ni ****(reserved).Kupata SIM Banking , piga *150*03#

sender: CRDB Bank. 21:55:53 HRS. July 2013.

Ujumbe huu uliingia kwenye simu yangu,
Je, umakini wa kitengo cha I.T katika bank hii upo wa kutosha?

Je, ujumbe huu ungetumwa kwa mhalifu huyo mteja fedha zake zingekuwa salama?

Je,bank husika inafahamu kama imefanya kosa la namna hii?

Je, hii ni moja ya sababu zinazopelekea watu kuchelewa kupata/ kuunganishwa kwenye huduma za kibenki kutokana na makosa/uzembe wa namna hii?

Mwisho: Omba M/Mungu akuepushe na janga kama hili!

NB: Nimeweka hizo **** kuepusha shari, maana wengine wanapokea taarifa kwa hisia tofauti. Pengine mhusika anaweza kuwepo humu JF akaona taarifa hii akashtuka sana! :A S-fire1:
 
Bado kuna usalama sipo kama unavyofikiria

Kupokea ujumbe mfupi kwenye simu ni hatua ya kwanza ya kujiunga ktk SIM Banking

katika stage hiyo hapo juu huwezi kutoa wala kuweka pesa kwenye account yako

Kisha unatakiwa uende mwenyewe kwenye tawi ulipofungulia accounti kwa ajili ya ku activate ukiwa na Tembo kadi yako.

Baada ya ku actvate utatakiwa usubiri kwa muda wa saa 24 ndo uweze kufanya muamala

Napenda kuwakilisha ila Watu wa CRDB Mnaweza kujitokeza kutoa ufafanuzi
 
Wengi wametumiwa ujumbe kama huo. Kwako tatizo ni lipi?
 
Bado kuna usalama sipo kama unavyofikiria

Kupokea ujumbe mfupi kwenye simu ni hatua ya kwanza ya kujiunga ktk SIM Banking

katika stage hiyo hapo juu huwezi kutoa wala kuweka pesa kwenye account yako

Kisha unatakiwa uende mwenyewe kwenye tawi ulipofungulia accounti kwa ajili ya ku activate ukiwa na Tembo kadi yako.

Baada ya ku actvate utatakiwa usubiri kwa muda wa saa 24 ndo uweze kufanya muamala

Napenda kuwakilisha ila Watu wa CRDB Mnaweza kujitokeza kutoa ufafanuzi
Inawezekana unachosema ni kweli, sina trust na huduma za kibenk za aina hii hapa Tz.
 
ok nadhani apo kama nimekuelewa ni kuwa iyo sms si yako, haraka nimefikiria kuwa either iyo namba ilikuwa recorded kwenye sysytem wakati unafungua akaunti au aliyefungua akaunti aliitumia kama referee endapo hakuwa na simu au masuala ya simcard owners like tigo na voda kufungia line zisizotumika na kuziuza kwa wengine ,mwishowe unakuta iyo namba ilikuwa documented crdb kuwa ni ya mteja wao. Kama sikosei bank network system inapick izo namba kutoka kwenye system yao na kutuma huo ujumbe, hakuna jinsi yoyote system inaweza kuota namba yako. Hata ivo bado pesa iko salama kwa kuwa kama hauna kadi, hauna pin namba , hauna account, au kimoja wapo hapo haitoshi kuwaibia crdb kwa vyovyote vile...kutumiwa iyo sms kama haikuusu ni sawa na kumuona batamzinga juu ya mti,haitoshi umemwona bado si wako, ukirusha jiwe atakimbilia kwa mwenye nawe, au hata bandani. Hapo hamna uzembe, may be tuseme uzembe uko kwenye uwezo wako wa kufikiria na ku analyse. I stand to be corrected, CRDB leteni majibu apa.
 
Bado kuna usalama sipo kama unavyofikiria

Kupokea ujumbe mfupi kwenye simu ni hatua ya kwanza ya kujiunga ktk SIM Banking

katika stage hiyo hapo juu huwezi kutoa wala kuweka pesa kwenye account yako

Kisha unatakiwa uende mwenyewe kwenye tawi ulipofungulia accounti kwa ajili ya ku activate ukiwa na Tembo kadi yako.

Baada ya ku actvate utatakiwa usubiri kwa muda wa saa 24 ndo uweze kufanya muamala

Napenda kuwakilisha ila Watu wa CRDB Mnaweza kujitokeza kutoa ufafanuzi

KU-activate siyo lazima uende bank. Ukishapata ujumbe kama huo una-activate mwenyewe. Isingekuwa rahisi kuchukua hela kwenye account ya mhusika kwenye stage ya ujumbe kama aliopata Chemiker kwa sababu katika ku-activate angelazimika kuingiza digits zote 16 za kadi yake pamoja na mwaka wa ku-expire.
 
Last edited by a moderator:
ok nadhani apo kama nimekuelewa ni kuwa iyo sms si yako, haraka nimefikiria kuwa either iyo namba ilikuwa recorded kwenye sysytem wakati unafungua akaunti au aliyefungua akaunti aliitumia kama referee endapo hakuwa na simu au masuala ya simcard owners like tigo na voda kufungia line zisizotumika na kuziuza kwa wengine ,mwishowe unakuta iyo namba ilikuwa documented crdb kuwa ni ya mteja wao. Kama sikosei bank network system inapick izo namba kutoka kwenye system yao na kutuma huo ujumbe, hakuna jinsi yoyote system inaweza kuota namba yako. Hata ivo bado pesa iko salama kwa kuwa kama hauna kadi, hauna pin namba , hauna account, au kimoja wapo hapo haitoshi kuwaibia crdb kwa vyovyote vile...kutumiwa iyo sms kama haikuusu ni sawa na kumuona batamzinga juu ya mti,haitoshi umemwona bado si wako, ukirusha jiwe atakimbilia kwa mwenye nawe, au hata bandani. Hapo hamna uzembe, may be tuseme uzembe uko kwenye uwezo wako wa kufikiria na ku analyse. I stand to be corrected, crdb leteni majibu apa.

nakubaliana na wewe kuwa asingeweza kuchukua hela kwenye account ya mhusika bila ku-activate, na ku-activate anahitaji namba ya kadi na details zingine za kadi, lakini uzembe upo tena mkubwa. Taarifa za ki-bank hazihitaji kubahatisha, information ziende kwa mhusika na si vinginevyo. Huoni kama mtu aliyekusudiwa apate huo ujumbe atakuwa anasubiri ujumbe umfikie ili aendelee na huduma wakati ujumbe umeenda kwa ndiye siye? Uzembe mkubwa. Hata hivyo, ninavyojua mimi kabla ya kujiunga na sim banking lazima bank ijilidhishe kuwa namba unayotumia sasa ndo ile uliyoiandika wakati unafungua account, kama siyo lazima utawape namba unayotumia kwa sasa.
 
mimi niliwahi kutumiwa kitu kama hicho nika ignore na baadaye inakenda crdb na walichoniambia ni kwamba namba zangu za siri zinabakia hivyo na huyo alienitumia ujumbe huo ningefuata maelekezo yake ningekwisha.
Kwa tahadhari jaribu kwenda kwenye tawi la crdb kwa uthibitisho.
wizi wa mtandao sasa hivi umetanda moto
 
Back
Top Bottom