Uzembe huu wa kushindwa kuilinda mipaka ya Tanzania hauvumiliki!

siyabonga

Senior Member
Jan 25, 2012
125
35
Wakuu,

Nimesoma kwa mshangao na mshtuko taarifa iliyotolewa na Waziri S. Sitta mbele ya kamati ya mambo ya nje naushirikiano wa kimataifa inayoongozwa na Edward Lowasa na kuripotiwa na gazetila Mtanzania la tarehe 29/03/2013 kuhusu kutwaliwa maeneo ya Tanzania kienyejina nchi jirani.Waziri Sitta anasema kuwa mawe ya mipaka yameng'olewana nchi jirani na hivyo kuyafanya maeneo hayo kuwa sehemu ya nchi hizo!

Tenakwa kuwa anayajua maeneo hayo anayataja kuwa ni Murongo mpakani na Uganda,Horiri kwa upande wa Kenya na hapo nyuma kidogo alipokuwa na ziara katika mkoawa Kagera alishuhudia uvamizi wa wageni hawa katika maeneo ya Tanzania na bilakuchukuliwa hatua yoyote!
Hakika huu ni uzembeuliopitiliza. Sidhani kama hao wenye jukumu la kulinda mipaka yetu na Kamandawao mkubwa hawaelewi kinachoendelea.

Kwa staili hii, sio rasilimalitu, bali hata kumbe hata Nchi inavamiwa na kuchukuliwa, halafu kiongozi wangazi ya Uwaziri anaishia kuripoti as if hakuna mamlaka ya kuchukua hatuastahili kwa jambo hilo.
Yaelekea viongozi wakuutulionao hawajui wanachokifanya na hasa jukumu lao la msingi la kulinda mipakana raia wa Nchi hii, hawajali tena kuwa Nchi hii si yetu peke yetu. Hawafikiriimbali, wanajali maslahi yao tu.Halafu, bila aibu WaziriSitta anasema, nakukuu:-

"Baada ya Serikali ya Tanzania kubaini mipakakung'olewa iliamua kufanya mazungumzo na kufanikiwa kurudisha mawe hayo katikabaadhi ya maeneo lakini mengine yalishindikana…"
Hivi ni kweli kuwa mipaka yanchi hii haifahamiki? Kamati za ulinzi na usalama katika maeneo husika zinakazi gani? Mtu anapovamia na kutoa nguzo za mipaka anakuwa ana nia gani? Huyuni mtu wa kuzungumza naye kweli? Wakati anatoa mawe hayo ya mipaka mpakakujenga makazi ya kudumu wenyeji tulikuwa wapi? Tulichukua hatua gani? Tunatoapicha gani kwa wanaotuangalia tukibaki watu wa kulialia wakati kwa ujingatunashindwa kusimamia rasilimali zetu?

Hakika viongozi wazembe waaina hii hawatufai. Hii ni staili yake,huyu bwana anajificha nyuma ya pazia na kuonyesha kiujanja ujanja kupingakwake, anajua anachokifanya, lakini angetueleza kwanza kuwa alishamueleza AmiriJeshi wake ambaye hakuchukua hatua ndio maana akaamua kuweka mabo hadharanikupitia kamati! Bado, usanii huu hauondoiuzembe waao wa kushindwa kulinda na kutetea Taifa hili.

Iwapo wao hawawezi,wajue kuwa maeneo yote wanayogawa yatarudi.
Ninaamini kuwa yeye nawenzake, bado wanakumbuka maneno ya Mwalimu JK { RiP }, aliposimama kidete paleIdi Amin, alipovamia kijeshi Tanzania, Mwalimu alisema atoke kwanza nje ya mipakayetu ndio mengine yafuate! Wao wanashindwa nini kwa hawa wanaoingia polepolekwa rushwa, tena mchana kweupe na wote wanawaona? Tusipokuwa werevu kidogotutagombana na jirani zetu wote. Hatuwezi kuwa tunaacha vitu vinazagaa zagaaovyo mpaka majirani wanajichukulia, iwapo ni mali yetu, tuonyeshe kuwatunavimiliki.
 
Wameshindwa linda raia na mali zao ndio hiyo mipaka???sasa hivi wanalinda CDM tu
 
Jamani hayo mambo ya mipaka na usalama wa raia, mbona ni mambo madogo !!! Wasira mshauri wa Rais alishasema kazi kubwa ya serikali ni kupambana na CHADEMA kuhakikisha ifikapo mwaka 2015 kiwe kimefutika nchini.
 
Siku hizi hatutambui mipaka ya nchi kwa mawe. Hii ni njia ya zamani sana. tuko ki-digitali zaidi na huko kwenye analogia tulihama kitambo
 
Wako busy na CDM mpaka ing'oke ..Jakaya Kikwete wewe kweli ulitumwa na Mungu,yaani ww ni janga tena la kutupwa.
 
Back
Top Bottom