Uzee mwisho chalinze! Slogan ya kipimbi kabisa

Uzee mwisho chalinze! Slogan ya kipimbi kabisa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,453
Reaction score
872,059
Utaukanaje uzee wako? Utaukataaje? Tena mchana kweupe? Uzee mwisho wake ni kifo na sio chalinze! Pale panaitwa Chalinze Mzee full stop!
Utajifarijije kuwa uzee mwisho chalinze wakati tayari jua linazama? Nyama zimeshuka na kulegea? Meno ndio hivyo tena ukila nyama utafikiri unakula bumunda! Kipochi manyoya unakichafua au kukibariki tuu? Mgosi mpaka aamshe popo la sivyo...! Kuchele..! Tena kuchele kweli
Haya ni maneno tu ya mjini yaso maana yoyote! Uzee haukimbiliki, hauzuiliki, unatisha na kuogofya hasa kama umeoa kigoli..! Utachapiwa tuu..! Najitazama nilivyo umri unasonga kwa kasi mvi zinatamalaki kichwani na hata huku! Zile triceps na biceps mikononi kwishney, six packs tumboni hakuna tena, Bali kuna kitu chenye kuchukiza mno KITAMBI tena kina matoleo! Ujana woote unanyauka halafu Leo uniambie uzee mwisho chalinze mfyuuu...!
Tunautamani ujana lakini tukumbuke ujana ni maji ya moto! Yashapoa na fainali uzeeni Tuukubali huu ukweli japo mchungu! Hakuna tatu bila tena wala kuunganisha route wala kula mdondo...!!!
WE LIVED ONCE BUT WE ARE NO LONGER N WE CANNOT TURN BACK THE TIME

SADLY CONTEMPLATING

mshana jr
 
Last edited by a moderator:
umenena kweli tupu, hasa hapo uliposema kuwa wazee walioa vigoli ndo full stress... maniner zao watachapiwa sana

Wazee wa mjini tunadanganywa na vibinti nasi twadanganyika tuu, tunakata mikwanja, tunahudumia halafu utamu wanaenda kufaidishwa Serengeti boys!!! Ndo maana Mimi najisemeaga ...nguruwe pita wewee....!
 
wanavyosema uzee mwisho chalinze nadhani wanamaanisha wale wazee wenye hela,kama hana hela atakuja kukubaliwa na mrembo gani.

Mfano Mengi uzee wake mwisho chalinze,si unaona kamtuliza miss Tanzania na kazaliwa mapacha
 
Viol kwanza umeadimika mno...! Pili ile ni coincidence tuu! 90% tunaishia mauvivu na kulambwa visogo kama si kung'ong'wa
 
Last edited by a moderator:
Viol kwanza umeadimika mno...! Pili ile ni coincidence tuu! 90% tunaishia mauvivu na kulambwa visogo kama si kung'ong'wa

mkuu mi nipo ila kuna mambo yananifanya busy.
kuhusu kung'ong'wa hiyo ni kweli kwani warembo wengi wanawatumia wazee ili tu wapate hela,si unajua wazee wanavyohonga wanajua washazeeka,vijana kama sisi tunatafuta maisha sasa kuhonga tena?
 
Ni mambo yetu yale ya kupata jiko? Tunakuombea sana
 
Back
Top Bottom