Uzanzibari + Utanganyika = Utanzania


Warudi kwao, waende wapi?
 
Ni walalamishi sana,
Sehemu yenye watu milioni na nusu Bunge la ina wabunge wengi kuliko Mwanza yenye watu zaidi ya milion tatu,

Na wanalipwa sawa na mbunge kawe yenye watu zaidi ya milioni,
Dah hatari mkuu imagine ukifika pale feri yao lazima uulizwe kitambulisho kama Huna basi barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa au hata card ya benk kutoka kwao kuja huku bara unapita tu sasa sijui maana ya muungano ipo wapi.
 
Wana haki, asilimia zaidi ya 90 zanzibar ni waislamu, sasa unategemea asiekua muislamu ajichomeke mule! Kumbuka zanzibar ina rais wake, na ni nchi na sio mkoa ama jiji.
Sasa kama wanajua wana serikali,rais na nchi yao kwanini wasitulie kwao??Wanalalamika nini ??Kila mtu akae kwao,sasa tumewachoka wanatakiwa kulitambua hilo.
 
Hv kati ya Tabora na Zanzibar ipi ni kubwa kieneo.?
Tabora?! Hivi upo serious kabisa unafananisha ukubwa wa tairi la toroli na tairi ya nyuma ya trekta?!

Zanzibar ndio mkoa mdogo kuliko miokoa yote hapa Tanzania.

Hata Dar es salaam tu ukifananisha na Zanzibar havifikiani hata nusu. Dar inakuwa ni kubwa sana.

Zanzibar ni makelele tu ila hakuna nchi pale. Maana hata tukitengana nao watajikuta mikononi mwa taifa jingine na watageuzwa wilaya kabisa bila mamlaka yoyote.
 
Sasa kama wanajua wana serikali,rais na nchi yao kwanini wasitulie kwao??Wanalalamika nini ??Kila mtu akae kwao,sasa tumewachoka wanatakiwa kulitambua hilo.

Kumbuka huo ni muungano, na wanapoona dhulma inatendeka wana haki ya kusema. Hata wewe ungelikua ni mzanzibar usingekaa kimya.
 
Kumbuka huo ni muungano, na wanapoona dhulma inatendeka wana haki ya kusema. Hata wewe ungelikua ni mzanzibar usingekaa kimya.
Wanatendewa dhuluma gani! Kila siku ni kulalamika tu na kudeka deka kama vitoto vya miaka miwili!

Kwa nini sasa wasijitegemee kwa kila kitu? Jana nilikuwa naangalia mechi yao ya kirafiki na Uganda; eti wana mpaka wimbo wao wa Taifa!!!

Sasa wanashindwa nini kujiondoa kutoka Tanganyika kwa 100%!!! Wajitenge hata kesho halafu waone kama kuna Mtanganyika atakufa njaa kutokana na huko kujitenga kwao.
 

Huenda wapo tayari kujitenga, lakini mamlaka yenyewe ndio inatia ugumu(Tanzania bara+Zanzibar)
 
Kumbuka huo ni muungano, na wanapoona dhulma inatendeka wana haki ya kusema. Hata wewe ungelikua ni mzanzibar usingekaa kimya.
Sasa dhulma inatendeka wapi kama Zanzibar wana rais wao pia wana rais anayetawala Tanganyika hadi nafasi ndogo za Tanganyika wamezishika wanzazibar pia ardhi wanamiliki bila kizuizi wakati huo watanganyika ni wakiwa hawana serikali, rais wala kiongozi wa kuwatetea na mtanganyika hawezi kuishi Zanzibar bila uraia wa zanzibar.??Pia hawezi kumiliki ardhi zanzibar,Pia kizuri cha mtanganyika ni cha wote ila kizuri cha zanzibar ni cha wazanzibar.
 
Kwanza wewe ismail jussa sio mzanzibari ila muhindi tu. Sijui nia yako kuihamisha zanzibar india au uarabuni? Hadi umezeeka unalia na zanzibar huru umeshindwa kukubali wazanzibari karibu wote asili yao tanganyika. Ni wandengereko, wamakonde, wazigua, wadigo, wazaramo, wamatumbi. Wee piga kelele tu hadi mwisho. Mwenzako maalimu seif kapiga kelele hadi mwisho😆😆😂
 
Watu mukishindwa hoja munakimbilia kwenye Ubaguzi.
 

Bhebhe nang'ho!

Tangu umeanza kujitambua mpaka hii leo umepata faida gani kuwachukia/kuwabagua watu weupe!! Au uliambiwa na wapumbafu wasiojielewa kuwa ukimbagua asie mwafrika utatajirika ama kuishi milele!! Jitathmini upya!
 

Mwinyi ni mtu wa Mkuranga, sasa unasemaje Mtanganyika hawezi kugombea Zanzibar? Acheni uwongo. Na majeshi yenu kila uchaguzi yanauwa na kutesa Wazanzibari. Hujawahi kusikia Wazanzibari wanauwa na kutesa Watanganyika.
 

Hivi kama jambazi lenye silaha likivamia nyumbani kwako, kati yako wewe mwenye nyumba na hilo jambazi ni yupi amefanya makosa na ni yupi anatakiwa kuondoka?
 
Kila siku kelele tu simuuvunje huo muungano wenyewe sijawahi ona Hata faida yake kwanza,muondoke mtuachie nchi yetu!!! #Mungu ibariki Tanganyika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…