Uzalendo wa Serikali awamu ya 5 na ripoti ya CAG upo wapi?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wadau Tulitangaziwa na CCM kuwa Magufuli ni Mzalendo wa kweli Rais wa Wanyonge Rais Mwenye Uchungu na Nchi yake je kwa Mfululizo wa REPORT za CAG zenye kuonesha UBADHILIFU wa KUTISHA kila SEHEMU mpaka Wilayani Kwake.

Je, CCM inataka Tuendelee kuamini kuwa Magufuli alikuwa kweli MZALENDO zaidi ya NYERERE?

Kama kweli CCM inahubiri kupambana na UFISADI basi REPORT ya CAG wakabidhiwe TAKUKURU waachiwe waifanyie KAZI bila kuingiliwa au KULINDANA ili Wahusika bila kujali VYEO VYAO WAKAMATWE kinyume chake UFISADI utazidi kuendelea kwa KASI kama ulivyo.
 
Changamoto ya kwanza ni kuelewa dhana ya ukaguzi kwa muktadha wa CAG. Anachowasilisha mkaguzi ni Audit Queries ambazo anaona zinahitaji maelezo. Kwa kutaka Takukuru wahusike nakupongeza hata hivo nabiwa ripoti ya CAG huambatana na ile ya Takukuru hoja hapa ni hao takukuru una waamini? Manake wanasiasa mnashida.
 
Lisu mpaka leo analelewa ubelgiji, DJ amegeuka ombaomba wa mitaa ya kariakoo
hoja ni dhana ya uzalendo na wizi na ubadhirifu awamu ya tano wewe unakuja na hoja ya kijinga....lakini ngoja nikusaidie kidogo

Mbowe kupita mitaani wasio werevu wanaona upande mmoja tu wa kuchangisha pesa. Werevu hata walio ndani ya ccm wanaiona kwa sura tofauti kabisa, ni tishio kwao.
1- CHADEMA inapima na kujua joto la mapenzi ya watu kwa chama chao ukizingatia uharamia waliotendewa na magufuli.
2-Inajizatiti zaidi kwa kuwatembelea watu mashinani mitaani na mwitikio unaonekana wazi. Hakuna mtu wa ccm hata mmoja, hata mwenyekiti wa ccm, anaweza akafanya hivyo watu wakamwendea ikiwa hawajalipwa kwenda kuhudhuria kimkutano chake. Wanafunzi tu ndiyo huenda pasipo kulipwa kwa sababu hulazimishwa.

Kamuulize Samia, Kinana, katibu mkuu na hata halmashauri kuu yote ya ccm na TUME YA UCHAGUZI watakwambia chadema ilivyo tishio kwa ccm.
 
Awamu ya 5 kaondoka mtu mmoja tu...
wengine wote wapo, ingekua vyema na wao wakaulizwa role yao na km hawakua na uzalendo then waachie ngazi...
tukianza na wale jamaa wawili pale jumba jeupe.

Mmoja alikua msaidizi wa karibu/mtia saini na mwingine alikua na dhamana na pesa na mtia saini vile vile. Then tushuke kwa mwenye dhamana ya pesa kwasasa maana yy alikua na dhamana ya mikataba enzi hizo akiwa waziri wa Katiba na sheria(ofc ya AG ipo chini yake).

Hebu tuache unafiki na chuki za kijinga, Haiwezekani team ikifungwa lawama apewe team captain peke yake ilihali team ina wachezaji 11 utadhani uwanjani alikua anacheza pekeyake.

We need a collective responsibility na serikali nzima iliyokuepo.
 
Mbona kama umeuza match!! Haka kamkakati ni kabaya sana kwa CCM! Jamaa anaingia kitaa anapata pesa na ufuasi!
 
hahahahaha....hii mechi hata ukiwauzia hawaiwezi. wako taabani na tume yao ya uchaguzi
 
Awamu ya 5 kaondoka mtu mmoja tu...
wengine wote wapo, ingekua vyema na wao wakaulizwa role yao na km hawakua na uzalendo then waachie ngazi...
tukianza na wale jamaa wawili pale jumba jeupe.

Mmoja alikua msaidizi wa karibu/mtia saini na mwingine alikua na dhamana na pesa na mtia saini vile vile. Then tushuke kwa mwenye dhamana ya pesa kwasasa maana yy alikua na dhamana ya mikataba enzi hizo akiwa waziri wa Katiba na sheria(ofc ya AG ipo chini yake).

Hebu tuache unafiki na chuki za kijinga, Haiwezekani team ikifungwa lawama apewe team captain peke yake ilihali team ina wachezaji 11 utadhani uwanjani alikua anacheza pekeyake.

We need a collective responsibility na serikali nzima iliyokuepo.
Magufuli alikuwa dereva wa basi, wengine walikuwa makonda na utingo. Basi likipata ajali kwa uzembe, dereva ndiye mhusika mkuu. Wengi waliojaribu kumwambia endesha kwa uangalifu, jibu lake lilikuwa, mimi ndiye dereva, hakuna wa kunibabaisha. Na ukijifanya unanishauri, ndiyo umeharibu kabisa, nitaendesha vibaya zaidi. Fikiria huyu utingo atafanya nini, na anajua kabisa dereva wake kuna wakati kichwani huwa zinaruka.
 
Back
Top Bottom