Uzalendo vs ukweli. Nachagua ukweli

Uzalendo vs ukweli. Nachagua ukweli

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,700
Reaction score
1,853
Mbunge Musukuma alisikika akiunguruma Hatuna chochote cha kujifunza kutoka Kenya! Waakenya tunawazidi kwa kila kitu: akili, siasa ....!

Kwa Musukuma kudai ana akili kubwa.....ni kichekesho cha mwaka huu. Wakenya walidukua saiti yake mtandaoni wakakuta alifeli la saba, tena la Tanzania! Ikawa kicheko cha wiki nzima!

Musukuma acha uzalendo wa kijinga, Kenya wametupita kwa mengi.

Uchumi: GDP ya Kenya 2023 ni $ 135 Billion, na Per Capita kwa kila Mkenya ni $ 1,945 Tanzania GDP bado ni $ 112 Billion Per Capita ni $ 1,200! Kibaya zaidi ni kwamba Kenya inazidi kutupita. Kwenye miaka ya 70-80-90 tofauti yetu ilikuwa ndogo sana. GDP yetu ilipokuwa $65 Billion, utakuta Kenya ni $70 Billion tu. Na wakati mmoja katika miaka ya 90 miaka miwili mfululizo tuliwapita ikawa GDP yetu ni 70 B na wao 69 B! Yaelekea ikiendelea hivi, uchumi wa Kenya utakuwa ni mara mbili ya wetu katika miaka mitano ijayo! Bila shaka statistics hizi hazimhusu Musukuma, anayeshikilia Uzalendo wa CCM!

Kenya kuna Watanzania wanaokadiriwa 600,000 wengi wakijishughulisha katika uchuuzaji, kazi za majumbani, kulea wazee, watoto, gereji bubu nk....wakati Wakenya walioko Tanzania wengi wana kazi za maana kama wakuu wa mashamba, ma director au wahudumu wa hoteli za kitalii , Mapilot nk.

Kenya inatuuzia bidhaa zilizotengenezwa viwandani, sisi bado tunawauzia mali ghafi za shambani. Ndiyo maana hata kama bidhaa zetu kwenda Kenya ni nyingi zaidi kwa ujazo, lakini wanatushinda kwa thamani ya bidhaa. Mashirika Makubwa ya Kimataifa yana makao Nairobi. Kwetu ukimwona 'international staff' labda ni kwenye migodi, kupora!

Mwisho, kwa ujinga wetu, tunaona Wakenya wakiandamana ni kuwa wana shida! Siyo kwamba wana uhuru zaidi ya wetu ambapo kwetu ukitoka nje tu utarudi na kilema!

Ni kweli, hata kwao hakuna uhuru kamili, lakini Kenya mtu hauawi kwa kuwa tu ni mwanachama wa chama fulani, au kaandika kitu fulani mmtandaoni au kamwita rais jina fulani....stage hiyo wameipita miaka ya themanini! Mwadanganywaaaa!
 
Back
Top Bottom