Kutokana na tabia iliyojengeka ya ushindani kati ya klabu mbili kubwa za mpira nchini yaani Simba na Yanga; uzalendo wa nchi umekua ukikosekana hasa pale timu yetu ya ndani inapokua inacheza na timu kutoka nje ya nchi.
Si ajabu kukuta shabiki wa Simba akiwa amelipa kiingilio na kununua jezi ili kushangilia timu kutoka nje ya nchi na mashabiki wa Yanga hivyo hivyo. Mashabiki wa Simba walishangilia TP Mazembe zama zile, na Yanga nao wameshangilia Nkana juzi kati.
Nadhani ni muda muafaka wa kuacha tofauti na ushabiki wetu wa ndani zinapokuja mechi za kimataifa kama ilivyo leo Simba wanapocheza na A Ahly ya Misri.
Chonde chonde wanaYanga, anza kuonesha uzalendo wenu kwa kuishangilia Simba pale uwanjani kwa mchina leo itakapokua ikimenyana na Mafarao ili uwe msingi wa uzalendo na utaifa wetu.
KILA LA KHERI SIMBA.