Uzalendo katika michezo(TAIFA KWANZA)

Full 8

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
313
271
Kutokana na tabia iliyojengeka ya ushindani kati ya klabu mbili kubwa za mpira nchini yaani Simba na Yanga; uzalendo wa nchi umekua ukikosekana hasa pale timu yetu ya ndani inapokua inacheza na timu kutoka nje ya nchi.
Si ajabu kukuta shabiki wa Simba akiwa amelipa kiingilio na kununua jezi ili kushangilia timu kutoka nje ya nchi na mashabiki wa Yanga hivyo hivyo. Mashabiki wa Simba walishangilia TP Mazembe zama zile, na Yanga nao wameshangilia Nkana juzi kati.
Nadhani ni muda muafaka wa kuacha tofauti na ushabiki wetu wa ndani zinapokuja mechi za kimataifa kama ilivyo leo Simba wanapocheza na A Ahly ya Misri.
Chonde chonde wanaYanga, anza kuonesha uzalendo wenu kwa kuishangilia Simba pale uwanjani kwa mchina leo itakapokua ikimenyana na Mafarao ili uwe msingi wa uzalendo na utaifa wetu.

KILA LA KHERI SIMBA.
 
hakuna iyo leo lazima al ahly apate mashabiki, tuwashangilie mkishinda muanze tambo zenu leo naombea mpigwe 3+
 
simba ni timu inayo milikiwa na mhindi akishirikiana na waarabu, nawashangaa sana 'wamatumbi' wanaojipendekeza pendekeza kwenye hili litimu,
 
Kutokana na tabia iliyojengeka ya ushindani kati ya klabu mbili kubwa za mpira nchini yaani Simba na Yanga; uzalendo wa nchi umekua ukikosekana hasa pale timu yetu ya ndani inapokua inacheza na timu kutoka nje ya nchi.
Si ajabu kukuta shabiki wa Simba akiwa amelipa kiingilio na kununua jezi ili kushangilia timu kutoka nje ya nchi na mashabiki wa Yanga hivyo hivyo. Mashabiki wa Simba walishangilia TP Mazembe zama zile, na Yanga nao wameshangilia Nkana juzi kati.
Nadhani ni muda muafaka wa kuacha tofauti na ushabiki wetu wa ndani zinapokuja mechi za kimataifa kama ilivyo leo Simba wanapocheza na A Ahly ya Misri.
Chonde chonde wanaYanga, anza kuonesha uzalendo wenu kwa kuishangilia Simba pale uwanjani kwa mchina leo itakapokua ikimenyana na Mafarao ili uwe msingi wa uzalendo na utaifa wetu.

KILA LA KHERI SIMBA.
Usianze mechi ya leo ila zijazo msimu huu ukiisha, uzalendo gani unalipia mechi? Pambaneni na hali yenu.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom