Uza kitabu chako/nunua kitabu kwa app ya Vitabu (Google Playstore)

Kabota

Member
Aug 15, 2009
63
10
Vitabu App ni application maalum ya simu ambayo itatumika kama sehemu ya
kuuzia vitabu ya aina mbalimbali. Ni app iliyo chini ya kampuni ya Mindtap
Tanzania Limited inayomilikiwa na watanzania.

App hii imetengenezwamahsusi kama njia mbadala ya wachapishaji wa vitabu na waandishi kuuzakazi zao kwa watumiaji wa simu Tanzania na nchi zingine duniani.
Inafahamika kuwa Tanzania hakuna platform thabiti ya uuzaji wa vitabu kwa
mfumo wa djitali kama ilivyo Kindle Amazon ambayo kwa bahati mbaya
haipokei kazi za Kiswahili.

Hivyo, wachapishaji na waandishi wameendelea kutegemea mfumo mmoja tu wa
vitabu vilivyochapishwa. Katika nyakati hizi ambapo matumizi ya
smartphones na internet yameongezeka kwa kiasi kikubwa hapa nchini, kuna
fursa kubwa wachapishaji kama Mkuki na Nyota kuweza kuwafikia wateja
wengine wengi zaidi.

INAVYOFANYA KAZI

Vitabu vitawekwa kwenye application kwa mfumo wa PDF. Msomaji atapewa
kurasa chache za mwanzo (walau 10 – 15) kwaajili ya preview ambayo ni
bure. Anapotaka kununua kitabu, atalipa kwa njia ya M-Pesa, Tigo Pesa na
Airtel Money. Atatumiwa token maalum kwaajili ya kutumia kudownload
kitabu. Kitabu kitahifadhiwa kwenye maktaba ya kwenye simu ambacho
atakisoma katika muda wowote anaotaka kwa urahisi na muonekano bora.

USALAMA

Vitabu hivi vitawezwa kusomwa kwenye app hiyo pekee. Hakuna uwezekano wa
mtu mmoja kumtumia mtu mwingine (no sharing). Maana yake ni kwamba mtu
anaponunua kitabu kwenye app, ni sawa na yule anayenunua kitabu cha
kawaida. Pia kwa mwenye simu, pale anapopoteza simu au kuiformat, vitabu
vyake alivyonunua vitarejea kwenye maktaba yake.

UKAGUZI NA USIMAMIAJI WA UNUNUZI

Mchapishaji atapewa akaunti maalum ambayo ataweza kukagua kila hatua ya
manunuzi yanayofanyika ya vitabu vyake. Hiyo itampa access ya moja kwa
moja kufuatilia mauzo yake. Biashara itakuwa ya uwazi wa hali ya juu.

WATU WA NCHI ZINGINE WANAWEZA KUNUNUA?

Kwa sasa, wasomaji wa Kenya wanaweza kununua vitabu kwenye app kwa kutumia
M-Pesa. Zambia na UGANDA wataweza kununua kwa kutumia mtandao wa MTN. Baadaye
tunafanya utaratibu malipo yaweze kufanyika dunia nzima.

Kama una kitabu na unapenda kukiuza, tafadhali piga simu 0766173514. Email, vitabu@mindtaptz.com
index.jpg
 
unauhakika watu hawataweza kushare hicho kitabu? fafanua kidogo hapo.

Hawawezi kushare sababu kitabu kinapopakuliwa kinahifadhiwa kwenye virtual library ya kwenye app ambayo haikuwezeshi kushare. Hakibaki kwenye simu
 
mpaka sisi mna vitabu vingapi? avatar yako imekaa kitapeli.
Hawawezi kushare sababu kitabu kinapopakuliwa kinahifadhiwa kwenye virtual library ya kwenye app ambayo haikuwezeshi kushare. Hakibaki kwenye simu
poa mkuu. ngoja niedit kitabu changu mwezi ujao tufanye business. mnavyovingapi mpaka sasa?
 
Hii itasaidia sana. Maana nishapotezaga hard copy nyingi sana kwa kuazimisha,mbaya zaidi kuna vitabu imekuwa shida kuvipata tena.
 
Ahsante sana nitafanya hivyo, ila pia toa website yenu au toa maelezo yanayojitoshereza juu ya aina za vitabu na kwa lugha zipi, na vipi kuhusu royalty na hati miliki. Mie nimepublish vitabu vitatu kupitia create space na kindle direct ya amazon. Waweza vipata kwa kusearch kwa kutumia jina la mwl. Frank Philemon
 
Back
Top Bottom