PreGE2025 UWT Lindi wamshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa Shule ya TSh. Bilioni 4.1

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) mkoa wa Lindi, wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Kanda ya Kusini katika eneo la kata ya Kiwalala Halmashauri ya Mtama inayogharimu kiasi cha Tsh 4.1 Bilioni .

1742802507055.png
Akizungumza wakati wa ziara ya kama ya utekelezaji wa UWT mkoa wa Lindi, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Kuruthumu Runje alisema kuwa kujengwa kwa shule hiyo kutasaidia kukuza sekta ya kwa watoto wa kiume kwa mikoa ya kanda ya Kusini.

Runje alisema kuwa kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi Trilioni 1.324 katika mkoa wa Lindi kwa ajili ya miradi ya Maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Maji, kilimo,madini, nishati,miundombinu na miradi mingine.

1742802520543.png
Aidha mwenyekiti wa UWT Runje aliwataka Wanawake wote wa mkoa wa Lindi kuhakikisha wanapigia kura za kutosha ili Dkt.Samia Suluhu Hassan ashinde kwa kishindo kutokana na kazi kubwa aliyoifanya.

Snapinst.app_486033011_18342489919156445_6273031557482961196_n_1080.jpg
 
Hivi jamani Serikali ilikufa au?
Mbona kila kitu ni raisi/mama na sio Serikali?
Ni maamuzi ya CCM au imetoka wapi??
 
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) mkoa wa Lindi, wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Kanda ya Kusini katika eneo la kata ya Kiwalala Halmashauri ya Mtama inayogharimu kiasi cha Tsh 4.1 Bilioni .

Akizungumza wakati wa ziara ya kama ya utekelezaji wa UWT mkoa wa Lindi, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Kuruthumu Runje alisema kuwa kujengwa kwa shule hiyo kutasaidia kukuza sekta ya kwa watoto wa kiume kwa mikoa ya kanda ya Kusini.

Runje alisema kuwa kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi Trilioni 1.324 katika mkoa wa Lindi kwa ajili ya miradi ya Maendeleo katika sekta za Afya, Elimu, Maji, kilimo,madini, nishati,miundombinu na miradi mingine.

Aidha mwenyekiti wa UWT Runje aliwataka Wanawake wote wa mkoa wa Lindi kuhakikisha wanapigia kura za kutosha ili Dkt.Samia Suluhu Hassan ashinde kwa kishindo kutokana na kazi kubwa aliyoifanya.

Ametoa wapi hela zote hizo! Kama vipi mshawishi anipe hata bilioni moja tu ni boost biashara yangu ya kuuza nazi.
 
Back
Top Bottom