UWT-CCM vurugu tupu

UWT-CCM vurugu tupu

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Mtafaruku mkubwa umeibuka na kusababisha kikao cha UWT kuvunjika, habari za uhakika toka ndani ya jumuiya hiyo zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sofia Simba, ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa kikao hicho majira ya saa 4:45 juzi usiku.

Majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa Taifa, Sophia Simba ya nani ateuliwe kushika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu Bara na Zanzibar ndiyo yaliyozusha vurugu na mabishano makali huku baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakipinga uteuzi huo.

Sofia Simba aliingia kikaoni akiwa na majina mawili mkononi la Salama Aboud Talib kutoka Zanzibar na kwa upande wa Bara alipendekeza jina la Ever Kiwele. Majina hayo yaliwafanya wajumbe kukataa kuyapitisha kwa madai kuwa hila zilitumika kuyateua.

==Nipashe==
 
nipashe nini,kama ni gazeti la lini au kuzusha ni sifa bainisha zaidi ukweli wako huu ni uongo.
 
Angalau umewasaidia kina Mzee Mwanakijiji habari, maana toka juzi inaonesha JF imeishiwa habari.

Haya hammy-D kusanya magamba wenzako wa buku sabasaba uje hapa kuifanyia kazi buku saba ya Lumumba, usimsahau kumpitia Ritz nyumbani kwao kule jangwani chini kwenye mabanda ya udongo yasio hata na umeme.
 
Last edited by a moderator:
Nipashe haijawah kumsema vzur sofia smba wanatumiwa na Mama Kilango Malechela toka ashndwe na komred mama sofia smba huyu msus wa knondon mama kilango haishi kutokwa mapofu ameshasalmu amr kwa lowasa baada ya ziara ya obama symbion kujikuta anapanga folen kumpungia lowasa huyu mama kilango malechela chz ata tundu lisu altaka kumtandka makofi
 
Sijui muambiwe na nani ndio muamini; labda Jibril. Tanzania Daima nalo limeandika HIVYO HIVYO. Haya, semeni ni gazeti la Mbowe kama kawaida yenu. Habari kamili hii hapa: CCM waumizana
 
nipashe nini,kama ni gazeti la lini au kuzusha ni sifa bainisha zaidi ukweli wako huu ni uongo.
UWT hapatoshi, wamtolea uvivu Sofia Simba

7th July 2013 Wakataa majina aliyopendekeza

Mtafaruku mkubwa umeibuka na kusababisha kikao kuvunjika, wakati wa kikao cha kamati ya utekelezaji ya taifa ya Jumuiya ya Wanawake ya CCM (UWT) kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Dar es Salaam, NIPASHE Jumapili imebaini.

Habari za uhakika toka ndani ya jumuiya hiyo zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Sofia Simba, ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa kikao hicho majira ya saa 4:45 juzi usiku.

Kikao hicho kiliitishwa huku ajenda kubwa ikiwa ni kupokea majina yatakayopendekezwa kwa ajili ya uteuzi wa manaibu Katibu wa UWT Zanzibar na Bara ambao watafanya kazi katika kipindi cha miaka minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mabishano yalianza kujitokeza muda mfupi baada ya majina mawili kutangazwa kwa wajumbe kuwa ndiyo yatakayozingatiwa katika uteuzi, likiwamo la Salama Aboud Talib kutoka Zanzibar na Ever Kiwele kushika wadhifa huo Tanzania Bara.

Chanzo cha habari kimesema baada ya majina hayo kutangazwa, wajumbe walianza kuguna na kuanza kumtolea uvivu Mwenyekiti wao kwa kumueleza wazi wazi kuwa majina hayo hawayataki.

Hoja kubwa ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji ni kuwa sifa, vigezo vya kitaaluma na uadilifu havikuzingatiwa kabla ya majina hayo kupendekezwa na kutaka waangaliwe wanajumuiya wengine watakaokuja na fikra, mawazo mapya na mageuzi ya kiutendaji na kiufanisi kwenye jumuiya hiyo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa pamoja na Mwenyekiti Simba kutaka kutumia rungu la cheo chake na kushinikiza wajumbe wa kikao hicho wapokee majina na kuyaidhinisha, waliendelea kumgomea na wengine kuanza kuinuka kwenye viti na kumzomea.

‘Wajumbe naomba kuwasilisha majina mawili ya Salama Aboud na Ever Kiwele kuteuliwa na kupigiwa kura kuwa manaibu Katibu wakuu Bara na Zanzibar, natumai mtaheshimu uteuzi wangu na kuyapitisha kwa maslahi ya Jumuiya yetu,"alisikika Simba.

Mjumbe toka mkoa wa Kanda ya Mashariki (jina linahifadhiwa) alisimama na kutoa rai kuwa majina ya manaibu katibu mkuu yaliopendekezwa , uwezo wao kiutendaji ni hafifu pia kwa wakati huu ingefaa kuwapata watendaji wenye kiwango cha elimu ya juu, uzoefu na uadilifu katika usimamiaji wa kazi zao za kila siku kwa faida ya jumuiya.

Aidha mjumbe huyo alitoa mfano kuwa kuna taarifa za upotevu wa mali za jumuiya na uuzwaji wa nyumba ya UWT Zanzibar katika mazingira ya kutatanisha na hadi sasa hakuna maelezo ya kuridhisha, hivyo haitakuwa busara kulipitisha jina la Salama kushika nafasi hiyo.

Mvutano huo ulisababisha baadhi ya wajumbe kuanza kutoa vitambaa na kufuta machozi, kufuatia Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi, kulazimika kutoka nje ya kikao huku akionekana kutokubaliana na mapendekezo ya bosi wake.

Kundi kubwa la wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wameegemea upande wa Makilagi lakini na madai yao ni kutoridhishwa na utendaji wa manaibu katibu mkuu, huku zikiwamo tuhuma za ubinafsi na utendaji usio na tija na ufanisi wa jumuiya hiyo.

Aidha wajumbe hao walimtaka Mwenyekiti Simba kufuata nyayo za Mwenyekiti wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete aliyefanya mabadiliko makubwa ya sekretarieti ya halmashauri kuu ya Taifa na kuwaingiza watendaji wapya akiwamo Abdulrahaman Kinana, Asha Rose Migiro, Zakia Megji na Dk. Mohamed Seif Khatib.

Wajumbe walidai kabla ya kupokea majina hayo, walitarajia kupata maelezo jinsi UWT ilivyochukua hatua kuhusu madai ya matumizi mabaya ya fedha yanayowakabili baadhi ya viongozi pamoja na nyumba zinazodaiwa kuuzwa kabla ya kufikiria kuwateua na kuwapa nyadhifa mpya.

"Chama chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi, hatuwezi kuendelea kuchagua bora viongozi, tunataka viongozi bora, waaminifu na wenye ubavu wa kutuvusha mwaka 2015 na si kuendekeza urafiki na mchezo mchezo,"alisema mjumbe mmoja.

Mjumbe huyo alisema upendekezaji wa watendaji dhaifu ni kupuuzia ushauri wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. Jakaya Kikwete anayetaka jumuiya za CCM ziwe na viongozi wenye upeo, maarifa ya kiutendaji na amana katika jamii.

"Mwenyekiti uteuzi wako sitaki kuuita ni batili bali ni vyema ukawa na manufaa kwetu na jumuiya yetu, hatuko tayari kujipiga kisu sisi wenyewe, majina uliyotuletea hatuko tayari kuyapisha kwa namna yoyote ile," alisema mjumbe huyo.

Mjumbe mmoja toka Zanzibar alisema ni vyema kukawa na UWT yenye hadhi na heshima kama ile ya kina Titi Mohamed na Sofia Kawawa ambao waliweka mbele maslahi ya wanawake na maendeleo badala ya kupeana madaraka kiushikaji.

"Salama ni Naibu Katibu Mkuu kwa kipindi kirefu Zanzibar, UWT imeshindwa kupambana na upinzani visiwani na kuwaunganisha wanawake, mali za jumuiya yetu zinapotea potea, iweje tuwarudishe tena watu wale wale, hapana Mwenyekiti kwa hilo tunakutaka radhi," alisema mjumbe mmoja maarufu.

Mwenyekiti Simba alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri kuwapo kwa kikao hicho na kukanusha kuvunjika.
Alisema kikao hicho kilichelewa kuanza hivyo walilazimika kukifunga saa 3:00 usiku kutokana na muda kupita. Simba alisema kikao hicho ambacho ni cha utekelezaji hakikuwa na uchaguzi wowote.

"Kilichotokea ni kwamba wajumbe walitegemea katika kikao hichi kungekuwa na uteuzi lakini hili halikufanyika, hatukufikia huko," alisema na kuongeza kuwa:

"Nachoweza kusema ni kwamba ifahamike kuwa sisi hatuna mamlaka ya kuteua zaidi wanaotakiwa kufanya hivyo ni Baraza Kuu la UWT," alisema.

Alisema huyo Salama anayezungumziwa ni naibu katibu mkuu UWT Zanzibar. Alisisitiza kuwa kikao hicho kilifanyika kwa amani na hakuna vurugu wala tofauti zilizojitokeza.

"Huyo aliyewaletea taarifa kuwa tulitofautiana ana manufaa yake binafsi, hivi vurugu zitatoka wapi kwa watu wasiozidi 15," alihoji.
 
"Muwanyime unyuma waume zenu kama hawaisapoti ccm!" - Sophia Simba
 
waache tu wataendelea kulana, kugombana, na kushambuliana mpaka wawe watupu ndipo wtajua kuwa wananchi tunaomba kwa ajili ya ufujaji wao

Back
Top Bottom