Uwezo wa Nyarandu. - Anaweza kuwa kama Mramba

Uwezo wa Nyarandu. - Anaweza kuwa kama Mramba

MchunguZI

Platinum Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,048
Reaction score
2,239
Wana JF,

Tangu kampeni Tokomeza imesimama kumekuwa na matamuko mengi toka kwa waziri kuonyesha kwamba ni mtu Imara sana, labda kuliko aliyekuwa waziri wake. Lakini baadaye magazeti yameanza kufunua taarifa mbali mbali zinazoonyesha kwamba alimuondoa yule profesa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanayama Pori kwa niya mbaya. Najaribu kuangalia elimu yake na uelewa wake Waziri huyu sioni kama ni mtu makini kiasi hicho maana hata hajui lolote juu ya wanyama pori na hata misitu au nyuki, mambo ambayo yako chini ya wizara yake.

Kuna wakati ilisemekana alikuwa na kampuni ya utalii ambayo alitaka kuitumia kujinufaisha wakati kampuni zingine akizigandamiza. Haya ya Nyarandu yatakuja kuwa kama yale ya Basil Mramba. Na kwa maoni yangu haonekani kama ni mtu makini ktk maamuzi yake ambayo yatachangiwa na ukweli kwamba hakutegemea kuwa waziri. Uwaziri kwake anaona kama ni bahati tu.

Sasa anatangaza oparesheni Tokomeza awamu ya pili. Je, kajipanga na watu wake? kweli anaungwa mkono na watendaji wake au anaamini yeye anaweza?

Btw; leo tena imetangazwa shehena nyingine ya meno ya tembo kukamatwa!
 
Anaweza kuwa ameona yale magari yaliyokabidhiwa ikulu na anatumia gear hiyo kuji boost kisiasa na boss wake huku akisahau kuwa Watanzania wanajua fika kulikuwa na magari makubwa na imara zaidi ya hayo yaliyokabidhiwa lakini ndovu 11,000 wametokomea. Asiyewajua ccm afuatilie bunge la katiba!
 
WELL SAID,
namfahamu nyalandu vizuri, ni mtu wa kujikweza, mtu wa inferiority complex. utabiri wako unaweza kutimia katika muda mfupi sana ujao. lets watch and see.
 
Huyu nyalandu si mtendaji kabisa , akihojiwa bbc aliulizwa mshahara wa wale ma game wanaokaa mstuni kulinda hawa wanyama kulinganisha na pay wanayopewa maofisa wajuu ,jamaa akajikanyaga sana akalazimishwa ataje figure akawa hana habari zaidi ya kusema wana scale upya salary scheme, akaulizwa tz imefikia wapi katika mkakati wa kuchoma pembe za ndovu ukiwa ni mpango wa kuziondoa katika economical benefit ili kuwakatisha tamaa maharamia jamaa akajikanyaga tena haja jibu , akaulizwa tena wamejipanga na reources (wafanyakazi na vifaa) za kulinda wanyama jamaa akasema wapo wanaomba misaada kwa sababu mbuga ni kubwa sana , hapa mzungu alimshangaa akamwambia kwa resources mlizonazo inakuwaje mnaomba misaada maanaa ukubwa wa mbuga ndo wingi wa resources ,,hapa napo akaleta story ,,mwisho alinichekesha aliposema wana mpango wa kuleta ndege za dolia yaan drones
 
In actual fact, huyu waziri Nyarandu uwezo wake ni mdogo kuweza kuhandle issues na problems za wizara hii.
Na problem yake kubwa anapenda cheap popularity.Inajidhihirisha tangu akiwa junior minister.

Huyu wakati wake wa kuwa full minister ulikuwa bado ila kwa urafiki na mkuu wa kaya yakatokea yaliyotokea hatuna jinsi ila time will tell.

Hata hii operation tokomeza awali ya pili aliyosema majuzi amekuwa criticised na subordinates wake kwamba anapenda kukurupuka kutangaza vitu kabla ya kushauriana nao.
 
In actual fact, huyu waziri Nyarandu uwezo wake ni mdogo kuweza kuhandle issues na problems za wizara hii.
Na problem yake kubwa anapenda cheap popularity.Inajidhihirisha tangu akiwa junior minister.

Huyu wakati wake wa kuwa full minister ulikuwa bado ila kwa urafiki na mkuu wa kaya yakatokea yaliyotokea hatuna jinsi ila time will tell.

Hata hii operation tokomeza awali ya pili aliyosema majuzi amekuwa criticised na subordinates wake kwamba anapenda kukurupuka kutangaza vitu kabla ya kushauriana nao.

Sijui ni vipi mchakato wa kuwapata mawaziri unavyofanyika lakini nilidokezwa kwamba jamaa kanunua uwaziri. Kabla hajateuliwa aligawa pesa kwa watu wengi sana. sasa sijui ni kwa njia gani!
Kwa jinsi ninavyomuona nahisi hata elimu aliyo nayo haikuiva kabisa maana nasikia aliitoa huko US. Isije ikawa ni hivi vyuo vya ajabu ajabu. Ni kama kijana wa Fomu 4.
 
Back
Top Bottom