Uwezo wa huyu mzee unaonyesha tofauti ya elimu ya dunia ya tatu na ile ya kwanza

UKpound

Member
Jul 26, 2018
79
151
Salam.... Kwanza kabisa nitoe pole zangu kwa yale yanayoendelea hapa kwetu TZ, sina lengo la kulaumu upande wowote lakini kiukweli tunapaswa kujitathimini upya kama taifa katika baadhi ya sekta.. Lakini pia nitoe pongezi kwa wananchi wa TZ bila kujali matabaka, dini, vyeo, elimu, itikadi na ukabila. Ukomavu tunaouonyesha katika kushughulikia matatizo yetu unahitaji pongezi.. Kuna msemo unasema "Mvumilivu hula mbivu" nami nimeuona uvumilivu katikati ya hali duni yenye kukatisha tamaa miongoni mwetu...

Twende moja kwa moja kwenye lengo la thread. Leo katika pitapita zangu mtandaoni nimeperuzi baadhi ya matukio yanayoendelea Bungeni na nimetokea kuvutiwa sana namna ya uendeshaji wa bunge la JMT chini ya mwenyekiti wake(Havard graduate) mzee Chenge... Huyu mtu ni zaidi ya kiongozi... Namna alivyochukulia hoja za Mh. Msigwa(kuhusu hoja yake ya kulitaka bunge kujadili matukio ya utekaji nyara) na namna alivyolichakata kwa umakini wa hali ya juu. kumenifanya niamini kuwa kuna upande hauhusiki moja kwa moja na tukio la utekaji lililotokea hivi karibuni( i stand to be corrected). Baadhi ya niliyoyagundua ni pamoja na
1.Jamaa hazuii hoja..
2.Anaelekeza hoja zijibiwe na serikali SIO KUZIZIMA kama wanavyofanya wasimamizi wengine wa bunge, 3.Anajiamini na anafanya bunge liwe na weledi...
4.Anaishauri serikali bila kung'ata maneno.
5.Hana upendeleo kwa upande fulani wa bunge.
Najaribu kufikiria pengine elimu yake imemsaidia kuondoa uoga kama ule tulionao watanzania tunaojitapata kwa kuwa na elimu ya madaraja fulani fulani Na hivyo basi kuonyesha utofauti wa ELIMU BORA na BORA ELIMU.
AT SOME POINT Nafikiri angefaa zaidi kuwa mkuu wa mjengo ule...(Tukiondoa baadhi ya matukio aliyowahi kufanya hapo nyuma)
NAWASILISHA.
TANZANIA KWANZA
 

Attachments

  • IMG_20190506_201448_665.jpg
    IMG_20190506_201448_665.jpg
    54.9 KB · Views: 19
Back
Top Bottom