Rihana
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 498
- 250
Wakuu juzi nilikuwa ile beach ya ocean road, nimeagiza dafu langu sina hili na lile...akatoke mhindi mmoja na gari aina ya Range rover....kwa kuwa kulikuwa na foleni kuelekea salender mwenye range akaamua kupita kwenye mchanga wa beach....alipita kwa spidi ambayo gari ile ilikuwa kama ina paa vile na ni kwenye mchanga....nilijiuliza maswali mengi...kwa nini haikuzama kwenye mchanga wakati gari yangu ambayo ni saloon nikisogea tu kidogo pale kwenye mchanga inatitia...je Range rover ni nyepesi kuliko gari yangu aina ya Grande Mark II ni kitu gani kinachoipa wepesi gari hiyo ya rangerover kiasi cha kukatisha kwenye mchanga wa beach bila ya kutitia? najua ina four wheel drive lakini ninahisi kuna kitu cha pekee kinachoipa nguvu gari ile......