Uwezo na mapungufu ya ACT pamoja na nguzo zake: Zitto, Kitila na Mwigamba

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Kila chama huanzishishwa kwa makusudi maalumu na kinakuwa na fikra za kuhusu uwezo wao, na kwa nadra hufanya tathmini ya mapungufu yao. Katika dokezo hili ninachambua uwezo na mapungufu ya ACT kwa mtazamo wa nguzo zake yaani Zitto, Kitila na Mwingimba.Katika kujiandaa kuanzisha chama cha siasa, Zitto, Kitila na Mwigamba walibuni mbinu ya kufanya mapinduzi ya siri katika chama cha Chadema. Kwa bahati mbaya kwao na nzuri kwa Chadema waraka wao wa siri ulinaswa na wao wakafukuzwa kwa usaliti huo na wametimkia ACT. Uwezo na mapungufu ya washirika hao watatu, ndio uwezo na mapungufu ya ACT.

Katika waraka wa usaliti, MM alitajwa kuwa na uwezo kama kijana, kuungwa mkono na CCM na kwamba dini yake ilikuwa ni mtaji wa kisiasa kwake. Ndio maana katika harakati hizo, wapambe wa washirika hao watatu waliwashambulia sana viongozi wa Chadema na chama chao isivyo halali wakitumia lugha za kibaguzi za karata ya udini na kabila kama njia ya kujitangaza. Bahati mbaya, uwezo ulioainishwa na nguzo za ACT, ni mapungufu wakati huohuo. Hoja ya ujana haina mashiko kwa sababu uongozi bora hautegemei umri na ndio maana nchi kama marekani huchagua kijana au mtu mzima kulingana na uwezo wa kiongozi husika. Hivyo ujana siyo sifa ya kuwa kiongozi bora. Habari ya kuungwa mkono na CCM nayo ni mapungufu makubwa. Inaonyesha kuwa ACT ni chama cha serikali ya CCM. Moja ya tabia ya vyama vya ‘upinzani’ vinavyoanzishwa na serikali iliyoko madarakani huibuka karibia na uchaguzi ili kujaribu kupunguza kura za wapinzani halisi wa chama kilichopo madarakani, na kwa sasa ni washirika wa UKAWA, ikiwemo Chadema.


Zitto ailishaonyesha kuwa ni mtu wa CCM. Kwa mfano wakati Chadema ikiwahenyesha CCM kule Arumeru Mashariki wakati wa uchaguzi wa ubunge, Zitto alijaribu kuisaidia CCM ipate jimbo hilo bila mafanikio, pale alipotangaza kuwa atagombea uraisi wakati akijua kuwa hakuwa amekidhi kigezo cha kisheria cha umri kugombea urais. Alifanya vile ili wapiga kura wa Arumeru wahamishie mawazo yao kwa Zitto, badala ya kuzingatia kupiga kura za kumwingiza Nasari Bungeni. Zitto pia amenukuliwa akiwaponda UKAWA, muungano ambao unatetea maslahi ya wananchi katika katiba mpya. Hii inaonyesha kuwa Zitto anawaunga mkono CCM na kuwatosa wananchi. Hakuna mzalendo anayewatosa wananchi na kupuuza maslahi yao. Hoja ya dini yake kama karata ya kisiasa nayo ni mapungufu makubwa ya ACT. Chama ambacho kinataka kujinadi kwa uzalendo, kinatumia dini ya Zitto kupata uungwaji mkono. Karata hii ya udini ndiyo hiyohiyo inatumiwa na CCM. Ni kinyume kabisa na fikra za baba wa taifa mwalimu Nyerere. Mwl. Nyerere alipata kusema kuwa mwanasiasa aliyefilisika hutumia udini na ukabika kuungwa mkono. Haya ndiyo wanayofanya Zitto, Kitila na Mwigamba kama walivyoonyesha katika waraka wao wa usaliti wa kuanzisha chama ndani ya chama. Hii inaonyesha wazi kuwa ACT ni chama cha serikali ya CCM. Chama kinachojinasibu kwa uwezo wa udini siyo chama cha kizalendo bali chama chenye malengo ya kuendeleza ukandamizaji wa CCM kwa njia yeyote ile huku kikimomonyoa misingi ya umoja na amani ya taifa aliyoiacha baba wa taifa letu Mwl. Nyerere.
 
Hizi drama za Bavicha zimeishatuchosha hauwezi kufanya mapinduzi kwenye vyama vya siasa mapinduzi yanafanyika kwenye dola peke yake.
Watu wa aina yako huwa siwajibu. Sijui imekuwaje leo!
 
Stabilaiza

Mkuu mimi nawashangaa sana watu kama nyie kwa sababu mnapoitaka na kupigania Demokrasia, basi swala la kuundwa kwa vyama vingine dhidi yenu lisiwe sababu ya udhoofu wao bali kukua kwa demokrasia mloitaka.

Kama Zitto,. Kitila na Mwigamba wameshindwa kuelewana na viongozi wa Chadema na wakafukuzwa hadi uanachama ulitegemea kipi kitokee? yaani udhaifu wa watu hawa unakuja kutokana na wao kufukuzwa Chadema? ama ni udhaifu wa Chadema kufukuza watu hao hao ambao leo wamekuwa mwiba.. Unajua unanikumbusha sana stori ya jamaa mmoja alimtalakia mkewe kwa sababu alikisia mkewe kuwa na mpenzi nje ya ndoa tena na rafiki yake wa karibu. Huyo rafiki yake alikana kutofanya kitendo hicho na kwamba alimchukulia tu kama shemeji na hata kumwambia yeye ndiye mwenye fikra chafu. Ukipenda sana kukisia watu wengine basi ni kutokana na wewe ulikuwa na tabia hiyo. Lakini jamaa hakuamini akatoa talaka na kumkatia hadi rafiki yake akisema lao moja, ndoa ikafa na urafiki ukafa kwa upande wake.

Sasa ajabu ni kwamba kila unapokutana na jamaa huyu hadithi ni za mkewe, oooh jana kaonekana bar akinywa pombe na jamaa moja la Usalama wa Taifa, nilisema huyu mwanamke malaya, sasa wewe mwenyewe ulikuwa bar ukifanya nini hadi ukawaona?. Kwa nini unafuatilia nyendo za mtalakia wako. Haya ikafika wakati mwanamke huyo kachumbiwa na yule yule jamaa wa Usalama wa Taifa jamaa akageuza kuwa ndoa hiyo haiwezi kudumu maana huyu mwanamke ni changudoa! Alaa leo mkeo ni changudoa wakati wameishi pamoja ktk ndoa kwa miaka 20!.

Jamani jamani hivi kwa nini siku zote hatutakiani mema? Mimi nilidhani ukimtalakia mtu utamtakia mema mbele ya safari kumbe tunamtakia shari!. Wewe nani wa kupima uwezo wa mtu kutokana na yale yalopita hata kama ni wewe mwenye mapungufu?

Waacheni Zitto, Kitila na Mwigamba wafanye yao na kama wakikoleza pengine wewe mwenyewe utajirudi na kuwapa support maana kazi yao wote hawa ni moja tu. Kutushawishi wananchi ni mahitaji gani na njia gani zilizo bora ktk kuwatumikia ili wapate maendeleo yao. Chadema ina ushawishi wake, CCM vile vile na acha ACT itupe ushawishi wake ambao wapo watu wanaamini katika UJAMAA watawafuata.
 
Last edited by a moderator:
Hizi drama za Bavicha zimeishatuchosha hauwezi kufanya mapinduzi kwenye vyama vya siasa mapinduzi yanafanyika kwenye dola peke yake.

sio dola tu, hadi kwenye ndoa. sembuse ndani ya vyama
 
Mkuu ni kweli kabisa, katika waraka wao, kulikuwa kuna kipengele kikitumia udini kama mtaji, na kilijieleza wazi bila maficho.


Nakumbuka Press conference ya Zitto Pale Serena Hotel ili ratibiwa na kuandaliwa na Viongozi wa UVCCM. Wakiwemo Mwampamba.
 
Huwezi kuwa na chama kinachohubiri usawa hapo hapo viongozi wake ni watumiaji wazuri wa propaganda za udini na ukabila, falsafa ya unyerere inapingana na ubaguzi huu wa kidini na kikabila.
 
Mkuu mimi nawashangaa sana watu kama nyie kwa sababu mnapoitaka na kupigania Demokrasia, basi swala la kuundwa kwa vyama vingine dhidi yenu lisiwe sababu ya udhoofu wao bali kukua kwa demokrasia mloitaka.

Kama Zitto,. Kitila na Mwigamba wameshindwa kuelewana na viongozi wa Chadema na wakafukuzwa hadi uanachama ulitegemea kipi kitokee? yaani udhaifu wa watu hawa unakuja kutokana na wao kufukuzwa Chadema? ama ni udhaifu wa Chadema kufukuza watu hao hao ambao leo wamekuwa mwiba.. Unajua unanikumbusha sana stori ya jamaa mmoja alimtalakia mkewe kwa sababu balikisia mkewe kuwa na mapenzi nje ya ndoa tena na rafiki yake. rafiki nyake alikana kutofanya kitendo hicho na kwamba alimchukulia tu kama shemeji lakini jamaa hakuamini akatoa talaka a kumkatia hadi rahifi yake.

Sasa ajabu ni kwamba kila unapokutana na jamaa huyu hadithi ni za mkewe, oooh jana kaonekana bar akinywa pombe na jamaa moja la Usalama wa Taifa nilisema huyu mwanamke malaya. Haya ikafika wakati mwanamke huyo kachumbiwa na yule yule jamaa wa Usalama wa Taifa jamaa akageuza kuwa ndoa hiyo haiwezi kudumu maana huyu mwanamke ni changudoa wakati wameishi pamoja ktk ndoa kwa miaka 20. Jamani jamani hivi kwa nini siku zote hatutakiani ema? Mimi nilidhani ukimtalakia mtu utamtakia mema mbele ya safari kumbe tunatakia shari. Wewe nani wa kupima uwezo wa mtu kutokana na yale yalopita hata kama ni wewe mwenye mapungufu?

Waacheni Zitto, Kitila na Mwigamba wafanye yao na kama wakikoleza pengine wewe mwenyewe utajirudi na kuwapa support maana kazi yao wote hawa ni moja tu. Kutushawishi wananchi ni mahitaji gani na njia gani zilizo bora ktk kuwatumikia ili wapate maendeleo yao. Chadema ina ushawishi wake, CCM vile vile na acha ACT itupe ushawishi wake ambao wapo watu wanaamini katika UJAMAA watawafuata.
Udhaifu wa Zitto, Kitila na Mwigamba ulidhihirika kabla hata hawajafukuzwa uanachama. Nimekupa mfano jinsi Zitto alivyojaribu kuwasaidia CCM bila mafanikio. Hapo alikuwa hajafukuzwa. Hata waraka wao wa siri wa kuanzisha chama ndani ya chama wenye mapungufu niliyoyajadili kama karata ya dini ya Zitto waliuandaa kabla hawajatimuliwa. Hivyo udhaifu wao wamekuwa nao kabla hawajafukuzwa na wameenda nao ACT.
 
Huwezi kuwa na chama kinachohubiri usawa hapo hapo viongozi wake ni watumiaji wazuri wa propaganda za udini na ukabila, falsafa ya unyerere inapingana na ubaguzi huu wa kidini na kikabila.
Haoni wasaka tonge tu, ni chama cha serikali ya CCM.
 
Udhaifu wa Zitto, Kitila na Mwigamba ulidhihirika kabla hata hawajafukuzwa uanachama. Nimekupa mfano jinsi Zitto alivyojaribu kuwasaidia CCM bila mafanikio. Hapo alikuwa hajafukuzwa. Hata waraka wao wa siri wa kuanzisha chama ndani ya chama wenye mapungufu niliyoyajadili kama karata ya dini ya Zitto waliuandaa kabla hawajatimuliwa. Hivyo udhaifu wao wamekuwa nao kabla hawajafukuzwa na wameenda nao ACT.
Mkuu Siasa sio Uadui na hizi ni tuhuma tu hakuna ushahidi wowote. Mbona nimeona humu barua ya siri ya Chadema ikizungumzia jinsi mbinu zilivyofanywa juu yao kipi mnataka sisi wananchi tuamini? Mlitupa sababu za kuwafukuza mkasema Zitto atahamia CCM haikuwa, Zitto kajiunga na chama kingine imekuwa yale yale ya usaliti, kila siku hamkosi kutunga hadith utafikiri tamthiria isokwisha!.

Huyu Zitto mnatuambia toka 2008 alikuwa na mbinu na CCM ajabu mkaja kumpa unaibu katibu wa chama, Chacha Wangwe toka miaka ile ni yale yale yaani mtu anayetaka kupanda juu tu lazima ashushwe kwa nguvu zote na kibaya zaidi Mbowe naye haambiliki maana kuna wanafiki hujifanya kujali sana chama kumbe ni wasaka tonge tu, kila siku hutafuta mialiko kwake wapeleke umbeya. Na binafsi namjua vizuri Mbowe toka ujana wake na hata mapungufu yake hivyo huwezi nambia kit mkuu wangu mimi ni mwana saikologia. mengine hayasemeki tuyaache kama yalivyo hayafai ktk ukumbi huu.
 
Stabilaiza tuwekeeni CD nyengine, hizi nyimbo za Zitto mara usaliti wengine zinatufanya post hizo tujibu bila hata kuzisoma, maana tunaona ni yaleyale. Porojo na hofu chadema kwa ACT.
 
Last edited by a moderator:
Hahahahahaaaaaa hapa ndipo vijana wenzangu wa Chadema mnaponiacha taabani kwa mchoko.... Hivi sisi ni wasemaji wa ACT?? Mi nadhani tuna mambo mengi sana ya kufanya....
 
zitto ni mwongo wa kupindukia alafu ni msahaulifu asubuhi alikaririwa akihojiwa na chombo cha habari akisema hato gombea nafasi yoyote ya uongozi act baadae ametweet yeye mwenyewe akiwa anajieleza na picha juu na kusema alikua akiomba kura kugombea nafasi ya uongozi. mtu wa aina hii ni hatari sana.
 
Back
Top Bottom