SoC04 Uwezeshwaji wa wananchi kumiliki uchumi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jengoz

New Member
May 14, 2024
4
2
Kwa majina naitwa Majengo Saidi Swadi.

Nianze kwa kuangazia namna ambavyo maisha halisi ya wananchi yanavyotofautiana na takwimu za kukua kwa uchumi wa nchi.
• Kwa kawaida tunasema kipimo cha uchumi mifukoni ni namna ambavyo watu wanaweza kumudu maisha yao ya kila siku kutokana na kipato chao. Ikiwa watu walio wengi watalalamikia ugumu wa maisha ni tafsiri ya uhalisia wa mzunguko wa pesa kwenye maisha ya kila siku.

Kwangu mimi kipato chochote kinachopungua tsh 10,000/= kwa siku natambua kama ni kipato kidogo na ama kwa hakika hakiwezi kubadilisha maisha ya mtu kutokana na uhalisia kwamba mwananchi mwenye kipato hicho ni vigumu kuweza kujenga mipango ya baadae ikiwa ni pamoja na huduma ya afya yake, elimu ya watoto wake, makazi bora, uwezo wa kujihudumia yeye mwenyewe na ziada kwa ajili ya kushiriki katika matukio ya kijamii kwenye familia yake.

Ili kubadili hali hii ni muhimu kwanza kuzingatia kundi kubwa ambalo kimsingi linaathiriwa na kipato cha chini kutokana na shughuli wanazozifanya.

Kwa maeneo mengi ya vijijini ukweli ni kwamba watu kwa asilimia kubwa wanategemea kilimo kama msingi wa kipato chao kuendesha maisha yao.

Kwa bahati mbaya sana watu hawa hawanufaiki na rundo la wataalamu wanaozalishwa kila mwaka kwasababu za kukosa uwezo wa kuwatumia ili kunufaika nao.

Ikiwa huwezi kumwekea mafuta ya bodaboda na posho ya angalau sh 20,000 kuja katika shughuli zako kutoa ushauri kutokana na kipato chako, kilimo chako kitaendelea kuwa cha kukidhi hitaji moja pekee la chakula na pengine hata kutotosheleza mwaka mzima.

Nini kinaweza kufanyika:
1. Wataalamu wa kilimo wafunge mikataba rahisi na wakulima kwa vikundi au mmojammoja kwa kukubali kukopesha utaalamu wao kwa makubaliano ya malipo ya asilimia kadhaa ya mapato yatokanayo na huduma waliyoitoa.
Aidha licha ya makubaliano hayo, ikiwa mwaka husika mteja wake akikosa tija kwa huduma aliyopatiwa basi iwekwe wazi mteja atalindwa hadi msimu unaofuata ili kukamilisha matakwa ya kimkataba.

Serikali ijikite katika maeneo makuu mawili,
1. Kutoa mbegu kwa ruzuku
2. Kuhakikisha mazo yao yanapata soko stahiki linalokidhi gharama za uzalishaji.
Aidha pia serikali inaweza kutoa motisha kwa wataalamu wote watakaoweza kusimamia vizuri taaluma yao na kufanikisha malengo ya wateja wao.
Tuzo zenye hadhi zitolewe kwa makundi au mtu mmojammoja kwa ajili ya kuwapa motisha wote walioshiriki vizuri na kupata mafanikio.

Huduma za mikopo midogo midogo ya vifaa, viuatilifu na bidhaa zote zinazokuwa vikwazo wakati wa kilimo zipatiwe suluhu kwa wakati sahihi.
Kwa kawaida tatizo kubwa la umasikini linachangiwa na uzalishaji mdogo kwa eneo kubwa.

Mwisho kila hatua iwekewe usimamizi mkubwa na unaokidhi viwango ili kuepusha kupata hasara zinazotokana na ufahamu mdogo wa viashiria vya hatari katika mazao.
 
Wataalamu wa kilimo wafunge mikataba rahisi na wakulima kwa vikundi au mmojammoja kwa kukubali kukopesha utaalamu wao kwa makubaliano ya malipo ya asilimia kadhaa ya mapato yatokanayo na huduma waliyoitoa.
Aidha licha ya makubaliano hayo, ikiwa mwaka husika mteja wake akikosa tija kwa huduma aliyopatiwa basi iwekwe wazi mteja atalindwa hadi msimu unaofuata ili kukamilisha matakwa ya kimkataba.
Nzuri, matokeo yajipambanie menyewe. Tukipata tunapata. Tukikosa tunakosa. Uaminifu na taarifa za wazi baina ya wasirika wa mkataba tu ndio gundi itakayounganisha hapa.

Kuhakikisha mazo yao yanapata soko stahiki linalokidhi gharama za uzalishaji.
Aidha pia serikali inaweza kutoa motisha kwa wataalamu wote watakaoweza kusimamia vizuri taaluma yao na kufanikisha malengo ya wateja wao.
Tuzo zenye hadhi zitolewe kwa makundi au mtu mmojammoja kwa ajili ya kuwapa motisha wote walioshiriki vizuri na kupata mafanikio.
Ahsante sana chief.

Mwisho kila hatua iwekewe usimamizi mkubwa na unaokidhi viwango ili kuepusha kupata hasara zinazotokana na ufahamu mdogo wa viashiria vya hatari katika mazao.
Kila sekta, kila taasisi ifanye kazi yake asee. Tuwajibike.
 
Back
Top Bottom