mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Uwekezaji wa raia wa china unapaswa kuchunguzwa. Imenilazimu niseme hivyo kwani raia hao hawataki kufuata sheria za nchi. Raia hao kila sehemu waliyowekeza ni lazima migogoro na serikali pia wananchi itokee. Kila ukisikiliza taarifa ya habari ni lazima usikie habari zao.
Kwa mfano jana ilisemekana kampuni ya kichina ya ujenzi wabarabara imewafukuza wafanyakazi 300 waliogoma wakiidai kampuni mishahara yao na malimbikizo licha ya kuwa kulikuwa na makubaliano ya nyongeza lakini kampuni hiyo iligoma kutekeleza.
Leo huko Morogoro kampuni ya kichina inachimba mawe ya kutengeneza marumaru licha ya kuzuiliwa miaka mitatu iliyopita na pia kutokulipa kodi. Mahakamani raia wa kichina wamejaa kwa kesi za ukwepaji kodi. Najiuliza kwanini wachina hawa wamekuwa kero ndani ya nchi yetu?
Wanapata wapi jeuri ya kutokutii sheria za nchi?
Tunaiomba serikali ichunguze uwekezaji wao kwani wamekuwa kama watanzania wanajiendea vijijini na kuanza shughuli kama wazawa.