Mimi ni kijana miaka au ukipenda niite mzee miaka 48 si kidogo, sasa wakuu naomba ushauri wenu ni hvi, nimeajiriwa mshahara sio mbaya , nina watoto 3 sasa shida nimewekeza sana kwenye elimu ya hawa watoto nimewapeleka shule bora hapa bongo ada mpaka 3m kwa term watoto wapo vzuri sana masomo yanapanda.
Shida niliyonayo wenzangu tuioajiriwa nao wapo mbali magari nyumba wameshajenga mi hata baiskeli sina hela bado mpangaji hela yote mpaka na mkopo umeishia kusomesha mpaka kiwanja nilinunua zamani nimeuza kwa ajili ya ada. Juzi binti yangu na mama yake wanataka niuze kiwanja changu eti huyu binti aende south africa kumalizia masomo, sasa nashidwa kuelewa nilikosea njia au vpi, hvi kuwekeza kwenye elimu inatakiwa ubaki bila chochote? Naombeni ushauri wakuu presha ipo juu.
Sent using
Jamii Forums mobile app