Ko vituo vya muungano na uwakilishi vilikuwa tofauti???nisaidieni wenye kuelewa
Wadau kuna swali linaniumiza kichwa juu ya uteuzi wa Dr. Huseein Mwinyi kuwa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Hussein Mwinyi ni mwakilishi toka Zanzibar ambapo Uchaguzi umefutwa...kwa tafsiri ya kisheria uwakilishi wake ni wa utata...itakuaje pindi uchaguzi utakaporudiwa na Dr. Hussein Mwinyi kushindwa kutetea kiti chake?
wajuzi wa sheria tunaomba muungozo wenu hapa maana waandishi wetu hawajui kuibua issues wao wana report events..
zec zanzibar ilifuta matokeo ya urais wa zanzibar wawakilishi na madiwan tu.ubunge na ya urais wa muungano hayatorudiwa. kwa hiyo mwinyi tayari yeye ni mbunge uchaguzi wao haurudiwiWadau kuna swali linaniumiza kichwa juu ya uteuzi wa Dr. Huseein Mwinyi kuwa Waziri katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Hussein Mwinyi ni mwakilishi toka Zanzibar ambapo Uchaguzi umefutwa...kwa tafsiri ya kisheria uwakilishi wake ni wa utata...itakuaje pindi uchaguzi utakaporudiwa na Dr. Hussein Mwinyi kushindwa kutetea kiti chake?
wajuzi wa sheria tunaomba muungozo wenu hapa maana waandishi wetu hawajui kuibua issues wao wana report events..
Baada ya kufuatilia kwa umakinini kuhusu mambo ya Zanzibar nimeelewa kuwa: Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015, uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Sheia ulisimamiwa na ZEC ya Jecha. Hata hivyo uchaguzi wa Rais wa Muungano na wabunge wa Muungano huko Zanzibar ulisimamiwa na ZEC kwa niaba ya NEC ya Lubuva. Jecha alipoamua kufanya mambo yake, alifuta uchaguzi wa Zanzibar tu (Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Sheia) na kuacha ule ulio chini ya NEC ya Lubuva. Basi baada ya sarakasi za Jecha, basi matokeo ya uchaguzi wa Rais wa Muungano na wabunge wa Muungano huko Zanzibar yalihalalishwa na NEC na yale ya Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Sheia yaliharamishwa na Jecha. Hivyo basi Dr Hussein Mwinyi aliyekuwa anagombea kiti cha bunge la Muungano ni halali kwa kauri ya NEC. Hapo ndipo hadithi ya kupika nyama ya Kuku na ya Nguruwe chungu kimoja halafu baada ya kuivisha ukasema nyama ya kuku halali na nyama ya nguruwe ni haramu ikaanza. Wataalamu wa sheria na katiba wataweza fafanua zaidi.
Kituo Ni Kimoja,kadi Ya Kupigia Kula Ni Moja Tofauti Ni Masanduku Lakini Pia Wasimamizi Ni Wale Wa Zec
Mbunge wa Bunge la muungano maanake nini?huyo ni mbunge wa bunge la muungano kwa iyo uchaguz wa zenji aumuhusu