Uwazi ndiyo njia pekee ya kuokoa sekta ya mafuta na gesi Tanzania

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
gesi tanzania.jpg

Suala la uwazi linaonekana ni changamoto kubwa katika sekta hiyo nyeti, hususan linapokuja kwenye mikataba ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa usiri mno kama FikraPevu inavyoendelea kuchambua.

Hakuna jambo linaloweza kuleta amani au chuki kama uwazi na usiri hasa katika mambo yanayohusisha rasilimali za umma.

Hata kama si wananchi wote wanaotakiwa kushiriki katika shughuli hizo za ama kusimamia au kuzalisha, lakini kujua nini kilichoandikwa kwenye mikataba walau kwa uchache ni jambo ambalo linaweza kusaidia jamii kutambua namna rasilimali zao zinavyoendeshwa pamoja na jinsi wao wanavyonufaika.

Zamani hali haikuwa hivyo, kwamba wananchi walikuwa wakijionea sawa tu kuhusu mambo yanayoendelea, lakini kadiri miaka inavyokwenda na wananchi kutambua umuhimu wa rasilimali zao na jinsi watakavyonufaika, suala la uwazi limeibuka.

Hali hiyo imechangiwa zaidi na ufisadi na ubinafsi wa baadhi ya viongozi waliopewa dhamana, ambao kwa kujali maslahi yao badala ya umma, wamekuwa wakiingia mikataba mibovu isiyozingatia maslahi ya taifa wala wananchi wenyewe.

Soma zaidi hapa=> Uwazi ndiyo njia pekee ya kuokoa sekta ya mafuta na gesi Tanzania | Fikra Pevu
 
View attachment 356121

Hii nakuunga mkono.. Rais Magufuli aiweke mikataba yote wazi, siyo ya gesi pekee. Tunajuwa siyo yeye aliyoifanya, ni vizuri Watanzania waione, Mali hii ni ya WATANZANIA wote, Na kama Rais alivyoahidi kusema serikali hii ni ya watu kwa hiyo Rais wangu weka mikataba wazi tujuwe ukweli ama sivyo mafisadi watakutupia lawama wewe.
 
Back
Top Bottom