Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Simba SC, Mnyama wanarejea michuano ya kimataifa huku wakiwa na matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara VPL, hali inayoaminiwa na mashabiki na wanachama wao kuwa huenda furaha ikawa chachu ya wachezaji wao kuendeleza furaha.
Utashuhudia pambano hili Live kupitia Azam Sports 2 kuanzia saa 10: jioni. Kaa nasi kukuletea yatakayojiri, usikose ukaambiwa
Vikosi vya timu zote vitakavyotoshana nguvu kwa upande wa Simba SC;
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Asante Kwasi, James Kotei, Yusuf Mlipili, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla, John Bocco, Emmanuel Okwi.
Sub; Emmanuel Mseja, Mzamir Yassin, Mwinyi Kazimoto, Moses Kitundu, Paul Bukaba, Ally Shomari, Juuko Murshid.
Coaches; Pierre Lechantre - Head Coach
Masoud Djuma - Assistant Coach Mohamed Aymen - Fitness Coach Muharam Mohamed - Gk Coach
Timu tayari ipo uwanjani kwa mtanange huu. Na Rais Mstaafu Ndugu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni mgeni rasmi kwenye mchezo huu tayari anakagua timu zote mbili.
Wakati wowote mpira utaanza hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Naam mpira umekwisha ananza uwanja wa Taifa
00' Simba SC 0-0 Gendarmarie Nationale FC.
02 ' Goooooooooaal Said Ndemla amepiga faulo na kutinga wavuni moja kwa moja
Simba SC 1-0 Gendarmarie FC
15' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC 1-0 Gendarmarie Nationale FC
30' uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba SC 1-0 Gendarmarie FC
32 ' Goooooooooaal John Bocco anaandika bao la pili kwa kichwa kazi mzuri kutoka upande wa kushoto.
Simba SC 2-0 Gendarmarie Nationale FC
45' Goooooooooaal goooooooooaal goooooooooaal John Bocco anaandika bao la tatu upande wa Simba SC
Naam mpira umeanza kipindi cha pili uwanja wa Taifa.
50' Gendarmarie FC wanapata penati. Inapigwa Penaltiiiiiiiii lakini golikipa Aishi Manula anapangua mkwaju huo na kuwa konaa.
Konaaaaa inapigwaaaa la la la nje!
65' Simba SC 3-0 Gendarmarie Nationale FC
70' Jezi namba 5 wa Gendarmarie FC anapewa kadi ya njano kwa kuchezea vibaya Kichuyaa
72 ' Kichuyaa anakwenda kwenye benchi na nafasi yake anachukua Mzamir Yassin
75' Said Ndemla anakwenda benchi na nafasi yake anachukua Mwinyi Kazimoto
85' Simba SC 3-0 Gendarmarie Nationale FC
90+3 ' Okwiiiii Okwiiiii Goooooooooaal. Emmanuel Okwi anaandika bao la nne kwa shuti kali la adhabu.
Simba SC 4-0 Gendarmarie Nationale FC
Wakati wowote mpira utakuwa umekwisha hapa uwanja wa Taifa.
Naam mpira umekwisha ambapo Simba SC imeibuka na ushindi wa magoli manne bila majibu dhidi ya Gendarmarie Nationale FC