Uwanja wa Taifa: Simba SC 1-0 Azam FC, ligi kuu soka Tanzania bara

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,828
Simba VS Azam: Leo ni vita kati ya kinara wa ligi kuu, Mnyama Simba dhidi ya Wanalambalamba wanaotaka kurejea nafasi ya pili baada ya jana Yanga SC kuikwea. Azam FC anahitaji ushindi ili kurejea nafasi ya pili pia ushindi utapunguza utofauti kati yake na kinara wa ligi.

Upande wake, Simba SC anahitaji ushindi kujiimarisha kileleni ambapo zitakuwa alama saba kati yake na Yanga SC kama Azam FC atapoteza mchezo wa leo.

Kuwa nami mishale ya saa kumi na nusu kukujuza kitachojiri uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
=======
simba.jpg

Kikosi cha Simba SC:
Aishi Manula, Erasto Nyoni, Yusuph Mlipili, James Kotei, Kapombe, Asante Kwasi, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Emmanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude.

SUB: Ally Salim, Gyan, Bukaba, Kazimoto, Mzamiru, Mavugo, Mohamed Hussein.

Azam.jpg
Kikosi cha Azam FC:
Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Agrey Moris. Stephan Kingue, Iddi Kipagwile, Frank Domayo, Mbaraka Yusuf, Yahya Zayd, Enock Atta.

SUB: Mwadini, Mwantika, Kheri, Hoza, Arthur, Sureboy, Shabani Iddi.


=======

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mpira kuanza, Simba 0-0 Azam.

01' Shiza Kichuya anajaribu kumpenyezea mpira safi John Bocco lakini mwamuzi wa pembeni anashoosha kibendera cha offside.

03' Simba wanapata kona ya kwanza na kipa kuugonga nje, kona pacha kwa simba na golikipa anafanikiwa kuondoa hatari.

05' Okwi anamjaribu kipa wa Azam lakini inakuwa chakula kwake na kuudaka barabara.

13' Azam wanajaribu kuingia kwenye 18 ya Simba kimaridadi lakini Yusuph Mlipili anatibua hesabu zao na kuutoa mpira nje, kona kwa Azam.

14' Aishi Manula anapangua kona ya Azam iliyokuwa inaelekea kuwa goli.

21' Shiza anapiga kona moja kwa moja golini lakini Golikipa wa Azam anautia mikononi.

23' Emmanuel Ikwi anapiga shuti kali lakini unakuwa chakula kwa golikipa wa Azam.

24' Simba wanajaa kwenye lango la Azam, Kapombe anapaisha juuu.

28' Okwiiiii, almanusura Simba iandike bao la kwanza lakini mpira unapita pembeni kidogo mwa goli.

37'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo

Emmanuel Okwi anaitanguliza Simba kwa goli la kuongoza baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa beki Erasto Nyoni na kuunganisha huku akimwacha kipa wa Azam Razak
Abalora akiwa hana la kufanya

40' Faul inapigwa kwenda lango la Simba lakini inadhibitiwa na mabeki wa Simba

42' Faul inapigwa kwenda lango la Azam lakini mipango inashindwa kuzaa matunda

45' Azam wameongeza mashambulizi kweda lango la Simba lakini wanadhibitiwa na beki line ya simba.

Mpira ni mapumziko

Simba 1, Azam 0

Kipindi cha tayari Kimeanza

45' Azam wanamuingiza Shaban Idd Chilunda

50' Jonas mkude anaonyeshwa kadi ya njano kwa mchezea faul mchezaji wa azam

51' Emmanuel anaonyeshwa kadi ya njano, faul inapigwa lango la simba lakini inadhibitiwa

53' Bado azam wanaliandama lango la Simba ili kujipatia goli

56' Anatoka Idd Kipangile anaingia Abubakar Sureboy

57' Asante Kwasi anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kucheza rafu

58' Azam wanafanya shambulizi matat kupitia kwa shaban Chilunda lakini anachelewa kupiga na kujikuta anadhibitiwa.

60'Louis Kangwa anapiga shuti akimtafuta Agrey Moris lakini linakuwa kubwa na kutoka nje.

62' Azam wanapanga mashambulizi kwenye lango la Simba lakini wanachelewa.

64'Emmanuel Okwi anawekwa chini na Agrey Moris, faul inapigwa kuelekea lango la Azam.

65'Simba wanafanya shambulizi kwenye lango la Azam lakini inaharibika baada ya Okwi na Boko kushindwa kuelewana namna ya kuupiga mpira.

67' Daniel Amor anaonyeshwa kadi ya njano

68' Said Hamis Ndemla anatoka na amingia Mzamiru Yasin

71' Emmanuel Okwi anapiga kichwa kimoja hatari lakini kipa wa azam anaipangua

72' Shiza kichuya anapokea pasi na kupiga shuti moja matata lakini anashindwa kuilenga vizuri golini

75' Timu zote zinashambuliana kwa zamu japo simba wanaonekana kufika kwenye lango la Azam mara nyingi zaidi

79' Azam wanafanya mashambulizi kwenye lango la simba lakini yanashindwa kuzaa matunda

82'Kipa simba Aishi Manula anaonyeshwa kadi ya njano kwa kupoteza muda

84' Simba wanamtoa Okwi na kumuingiza Nicolaus Gyan

85' Kona inapigwa kuelekea lango la Simba ila haijazaa matunda

87'Shaban Idd Chilunda anaingiza mpira ndani lakini Aishi Manula anaidaka

90' Azam wanafanya shambulizi la nguvu kwenye lango la simba lakini linakataliwa

90+2' Na mpira umekwisha

Simba 1, Azam 0

Simba inajikita kileleni kwa pointi 41

simba.jpeg
 
Azam akishinda mnaondolewa nafasi ya pili..
Haina Shida Mkuu. Si unajua tena yaani siku Mtani wako akifungwa basi inakuwa burdani yaani Mji unapoa kabisa.

Hakuwi na tambo za kutufanya tukose amani. Hahahaaaa.
 
Leo ni vita kati ya kinara wa ligi kuu, Simba dhidi ya wanalambalamba wanaotaka kurejea nafasi ya pili baada ya jana Yanga kuikwea. Azam anahitaji ushindi ili kurejea nafasi ya pili pia ushindi utapunguza utofauti kati yake na kinara wa ligi.

Upande wake, Simba anahitaji ushindi kujiimarisha kileleni ambapo zitakuwa alama saba kati yake na Yanga kama Azam atapoteza mchezo wa leo. Kuwa nami mishale ya saa kumi kukujuza kitachojiri uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

=======
Azam ni Simba B
 
Back
Top Bottom