Uwanja wa ndege Simiyu kuitwa Serengeti

Uwanja wa ndege Simiyu kuitwa Serengeti

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
3f73d05b87cf6191a9dddbd43825e1eb.jpg

MKOA wa Simiyu unatarajia kupata uwanja wa ndege utakaojengwa mpakani na Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Dk Richard Mayongela amesema sasa ni zamu ya mkoa wa Simiyu kupata uwanja chini ya dhana ya kila mkoa kupata fursa.

Akizungumza katika banda la TAA kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa yanayofanyika mkoani Simiyu, Mayongela amesema uwanja huo utajengwa katika eneo la Igegu wilayani Bariadi ambalo liko karibu na mbuga ya Serengeti.

Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa akizungumzia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege nchini, amesema walishaleta wataalamu wa upembuzi yakinifu na upembuzi wa kina.

Alisema waziri mwenye dhamana, alitoa angalizo kwa mkoa kuhakikisha fidia kwa ajili ya watakaolazimika kupisha maeneo ya ujenzi uwanja huo, inakuwa ndogo.

"Fidia ni jambo linalokwamisha miradi. Tunaomba mkoa uhakikishe fidia inakuwa ndogo," alisema.

Ametoa mwito kwa mkoa kuelimisha wananchi juu ya fursa zilizopo kutokana na ujenzi wa uwanja huo na wazitumie, ikiwa ni pamoja na kuanza ujenzi wa hoteli.

Wakati huo huo, alionya juu ya uvamizi wa viwanja vya ndege unaofanyika katika maeneo mbalimbali na kusababisha migogoro na matokeo yake kukosesha viwanja hati.

Alisema kati ya viwanja vya ndege 58 vinavyosimamiwa na TAA, viwanja visivyozidi 12 ndivyo vyenye hati.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema uwanja huo ukikamilika watataka upewe jina la Uwanja wa Ndege wa Serengeti.

Mtaka aliomba TAA kujenga uwanja katika kiwango kitakachoruhusu ndege kutoka nje kutua moja kwa moja katika uwanja huo irahisishe watalii kufika na kutembelea mbuga.

"Mtalii hana sababu ya kushuka KIA (Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro) au Mwanza," amesema.

Amesema zipo hoteli nyingi katika Ziwa Victoria kwa ajili ya watalii na wataendelea kuhamasisha ujenzi katika maeneo mengine mkoani humo.

Alisema uongozi wa serikali uko tayari kuwezesha malipo ya fidia kuwa chini na wananchi wameridhia juu ya hilo na kwamba Sh bilioni moja iliyotengwa, wataanza mara moja kuitumia kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo.
 
Hili ni la RC au ni jambo la Mkuu wa nchi
 
Hivi mkuu wa mkoa wa Geita ni nani? Mbona yeye yupo kimya
 
View attachment 829374

Kwa hiyo Mkurugenzi kasafiri kwenda kwenye maonesho ya Nane nane, Simiyu kwa ajili ya kutangaza kuwa kuna uwanja wa ndege unatarajiwa kujengwa huko !!!! Mbona angemwandikia barua RC.
 
Back
Top Bottom