Uwanja wa ndege Chato waibua mjadala bungeni

Uwanja wa ndege Chato waibua mjadala bungeni

Joined
Apr 18, 2012
Posts
95
Reaction score
213
pic+chato.jpg


Dodoma. Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Chato mkoani Geita jana ulizua mvutano bungeni baada ya mbunge wa Malindi (CUF), Alli Saleh kuhoji sababu za kujenga uwanja huo.
Akichangia taarifa za kamati za Bunge za Miundombinu na Viwanda, Biashara na Mazingira, Saleh alisema nchi nzuri haiwezi ikawa na njia za kutoka na kuingia ndani ya nchi (gateway).
“Uwanja wa ndege wa Songwe ni gateway (njia ya kutoka) ya Kusini. Lakini leo hii nimesikia kuwa zabuni imetolewa ya kutengeneza taa,” alisema Saleh.
Hata hivyo, Saleh alisema haoni athari ya uchumi za kujenga Uwanja wa Ndege Chato.
“Nimekuwa nikijiuliza hivi Chato ni gateway ya kwenda wapi? Kuleta uwanja pembeni mwa nchi hakuna utalii, hakuna biashara tunatumia fedha nyingi badala ya kuimarisha viwanja vyenye gateway,” alisema.
Hata hivyo, naibu waziri wa Maliasili, Constatine Kanyasu alimpa taarifa kuwa umelenga kufungua utalii kwenye mapori ya akiba yaliyopo mkoani humo.
Alipotakiwa kuendelea, Saleh alisema anafikiri wangewekeza maeneo ambayo yana faida kiuchumi.
Lakini kabla ya kuendelea mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema alimpa taarifa kuwa: “Mobuto (Sese Seko) alijenga kiwanja kijijini kwake na sasa baada ya utawala wake umekuwa nyumba ya popo.”
Hata hivyo, zilisikika kelele za taarifa tena baada ya Saleh kuikubali taarifa ya Lema.
Akitoa taarifa hiyo, mbunge wa Geita Vijijini (CCM) Joseph Kasheku maarufu Musukuma alisema ujenzi wa viwanja upo katika ilani ya chama chao ya kujenga uwanja kila mkoa.
“Mipango ya Mkoa wa Arusha si sawa na Geita, Jiji la Arusha uwanja uko Kia, nilikuwa nadhani wangeachana na uwanja wa Chato huo ni mpango mkakati wa Geita,” alisema.
Akiendelea, Saleh alisema uwanja huo umejengwa kwa ajili ya upendeleo. Hata hivyo, wakati anachangia kelele nyingi za taarifa ziliendelea kutoka kwa wabunge.
Baada ya muda wa Saleh kuchangia kuisha mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alisema sio kila kitu lazima kisemwe ndani ya Bunge lakini kwenye maendeleo ya nchi kuna vitu vingi vinavyozingatiwa kiuchumi na maeneo ya mkakati ya ulinzi.
Awali, akiwasilisha taarifa ya shughuli za Kamati ya Miundombinu mwenyekiti wake, Moshi Kakoso alishauri Shirika la Ndege ATCL kusimamia ipasavyo nidhamu ya watumishi wake kwa sababu kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wateja.
 
Wataijengea Mbeya jpm namwelewa sana

Awamu hii kila kitu nyumbani kwanza kuanzia uteuzi mpaka miundombinu...hivi na SGR inaenda mwanza kwanza au Kigoma?? Maana kigoma kuna Drc, Burundi na Rwanda yenyewe
 
mweee jf bhana. nimecheka hizo comment hapo juu
 
TAFADHALI TUUNGE MKONO JUHUDI ZA MWESHIMIWA...
 
Wasisahua na yule waziri wa nishati kila siku anaenda Chato kuzindua umeme wa REA huku vijiji vingine nchini havina walau hata nguzo moja yaani karibu vijiji vyote vya Chato vina umeme wa rea huku kwingine mradi umesisma pasipo kujua nini kinaendelea. Lakini huko chato mh Kalemani hata usiku anatinga kuzindua umeme.
 
Hata hivyo, naibu waziri wa Maliasili, Constatine Kanyasu alimpa taarifa kuwa umelenga kufungua utalii kwenye mapori ya akiba yaliyopo mkoani humo.
SWALI: hivi kati ya viongozi wote wa ccm kuna MWENYE AKILI!? Mana nina wasiwasi hata ubongo haupo vichwani kama binadamu wengine....
 
Hakili yako ikiwa ndogo kuna tabia ya kufikiri mwenye hakili sana ni kichaaa ndo maana unashangaa wenye hakili sana
SWALI: hivi kati ya viongozi wote wa ccm kuna MWENYE AKILI!? Mana nina wasiwasi hata ubongo haupo vichwani kama binadamu wengine....
 
Back
Top Bottom