Uwanja wa mapambano

Bengalisis

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
1,847
2,768
*KATIKA TISHIO LA KIFO*

*Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?* Esta 4:14.

Matukio ya ajabu yatafunguka mbele za ulimwengu muda si mrefu. Mwisho wa mambo yote umekaribia. Wakati wa taabu umefika karibu kwa watu wa Mungu. Hapo ndipo tamko litakapotolewa linalopiga marufuku wale wanaoshika Sabato ya Bwana ili wasinunue wala kuuza, likiwatishia kwa adhabu na hata kifo, kama hawatashika siku ya kwanza ya juma kama Sabato.

Tamko ambalo litatolewa dhidi ya watu wa Mungu litafanana kabisa na lile lililotolewa na Ahasuero dhidi ya Wayahudi wakati wa Esta Shetani alichochea mpango wa kufutilia mbali wale waliotunza ujuzi wa Mungu wa kweli duniani. Lakini mipango yake ilishindwa dhidi ya mamlaka inayoipinga inayotawala kati ya watu.Ulimwengu wa Kiprotestanti unapolitazama kundi dogo linaloshika Sabato unaliona kama Mordekai akiwa langoni. Tabia na mwenendo wake, inayoonesha heshima kwa sheria ya Mungu, ni karipio kwa wale ambao wametupilia mbali hofu ya Bwana na wanaikanyaga Sabato yake; kwa njia fulani mdukizi asiyependwa sharti aondolewe.

Kiongozi yule yule wa mpango ambaye alipanga dhidi ya waaminifu katika zama zilizopita, bado atatafuta kuwaondoa duniani wale wanaomcha Mungu na kutii sheria yake. Shetani atatibua hasira dhidi ya hawa wachache walio wanyenyekevu ambao kwa kuwa makini wanakataa kukubali desturi na mapokeo yanayopendwa na wengi. Watu mashuhuri na wenye mamlaka watajiunga na wavunja sheria na waovu katika shauri dhidi ya watu wa Mungu.Wakiwa hawana “Ndivyo yasemavyo Maandiko” kama majibu dhidi ya watetezi wa Sabato ya Biblia, wataamua kutumia maagizo yanayokandamiza ili kujazia upungufu wao

*Katika uwanja huu wa mapambano ndipo linapokuja pambano kuu la mwisho la vita kati ya ukweli na uongo.Na hatuachwi katika wasiwasi kulingana na suala hili. Sasa, kama ilivyokuwa katika siku za Mordekai, Bwana atathibitisha ukweli wake na watu wake.*
 
Amina, ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom