Uwanja wa KIA sasa ni mali ya Serikali kwa 100%

Uwanja wa KIA sasa ni mali ya Serikali kwa 100%

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Waziri wa ujenzi mh Kamwelwe amesema kwa sasa Serikali inaumiliki uwanja wa KIA kwa asilimia 100 baada ya kuwalipa wazungu waliokuwepo kiasi cha dola za Marekani 5.6 milioni.

Kamwelwe amesema kwa sasa bodi ya uwanja huo ni ya wazalendo watupu na tayari wameanza kutoa gawio Serikalini na kwamba sifa za pekee zimwendee Rais Magufuli kwa kulisimamia jambo hili.

Chanzo: ITV habari!

==============
Kil Int Air.jpg

Waziri Kamwelwe aliyasema hayo baada ya kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Usimamizi wa Uwanja huo (KADCO).

Alifafanua kuwa awali uwanja huo ulikuwa unaendeshwa kwa ubia na wadau watatu tofauti ambao kwa sasa serikali imewalipa Dola za Marekani milioni 5.6 na kuufanya uwanja huo kwa sasa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100.

Aliipongeza menejimenti ya uwanja huo chini ya kampuni ya KADCO ambayo alisema imekuwa ikifanya kazi nzuri na inayoonekana.

Waziri Kamwelwe alisema pamoja na hatua hiyo, serikali imeanza kufanya ukarabati wa idara mbalimbali za uwanja huo ili kuujengea uwezo zaidi ikiwamo kuzifanyia matengenezo ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kwamba tayari ukarabati wa eneo la kufanyia kazi hiyo unaendelea na ununuzi wa baadhi ya vifaa umeshafanyika.

Kuhusu hatua za kuuwezesha uwanja huo kuvutia mashirika na wadau mbalimbali duniani, pia uko mpango wa kujenga jengo maalumu kwa ajili ya huduma za wageni wanaotaka kuja na ndege zao binafsi, jengo ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi ndege kubwa zikiwamo za Boeing huduma ambayo inapatikana kwenye nchi zilizoendelea.

Waziri Kamwelwe alisema serikali imeanza maandalizi ya kuviwezesha viwanja vya ndege vya Kilimanjaro Songwe na Mwanza kutoa huduma ya usafirishaji wa mizigo ikiwa ni hatua za awali za kuhakikisha kuwa mpango wa serikali wa kununua ndege ya mizigo unakuwa na tija.

Aliitaka bodi mpya ya shirika hilo kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na bodi iliyomaliza muda wake na kuhakikisha kuwa mipango yote iliyoanzishwa ukiwamo wa kuvutia ndege za mizigo unafanikiwa kwa asilimia 100.

Akizungumza baada ya kuzinduliwa kwa bodi hiyo, George Teu na Kaimu Mkurugenzi wa uwanja huo, Mhandisi John Mkoma, aliishukuru serikali kwa kutoa ushirikiano mkubwa wa kuboresha uwanja huo.

Mkoma alisema tayari wameshakamilisha ukarabati wa jengo la matengenezo ya ndege, chumba cha kuhifadhia mizigo na pia miundombinu muhimu ikiwamo mashine za kuzalisha umeme.

Mkoma alisema pamoja na changamoto zilizopo ikiwamo ya ushindani wa kibiashara, uwanja huo umeendelea kujiimarisha katika ukusanyaji wa mapato hatua iliyowezesha mwaka huu, KADCO kutoa gawio la Sh. bilioni moja kwenye mfuko wa serikali.


Chanzo: Nipashe
 
Mwanza uwanja unaojengwa kwa sasa ni terminal ya kawaida tu, pia Mwanza ina wasafiri wengi sana kuliko KIA
Achana na siasa ww, KIA inapokea watu wengi zaidi ya Mwanza tena international visitors ndo wa kutosha. Angalia tu flightradar24.com then angalia arrival/departures ya siku nzima uone inashusha zaidi ya watu 3000 per day. ukoweka idadi ya watu wanao-depart na ku-arrive utajua faida ya KIA ni ipi.
 
Kabla walikuwa na percent ngapi? By the way am all for nationalization lakini inabidi tukubaliane kama privatization au vinginevyo is the way forward sababu kama tunatumia kodi zetu kununua hisa za mali tulizouza wakati huo huo bado tunauza kwa so called wawekezaji, now one has to ask what's the hell is happening.
 
Kujiaminisha kuwa kila kitu mpaka mzungu
Sasa naona tumeanza kuelewa kuwa tunaweza [emoji23]


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
..siyo lazima serikali kumiliki viwanja vyote vya ndege nchini.

..uwanja wa ndege wa Gatwick ulioko Uingereza unamilikiwa na wawekezaji binafsi.
Wazawa Au!?
 
Back
Top Bottom